Ludewa: Kiongozi wa CHADEMA apiga magoti kuishukuru CCM kwa kutekeleza ilani yake. Hii ni baada ya mto Ruhuhu kukamilika

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Diwani wa kata ya Ruhuhu wilayani Ludewa mkoani Njombe kupitia CHADEMA Atanas Haule, amejitokeza katika ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya na kuipongeza serikali kutekeleza Ilani ya CCM kwa kukamilisha ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu.

20220308_205907.jpg

20220308_205920.jpg
 
Hongereni sana wana Ludewa kwa kukamilishwa daraja la mto Ruhuhu. Mimi ni mmoja wa watu wanaofahamu adha ya mto Ruhuhu. Zamani kuvuka pale ilikuwa ni hatari kubwa ya mamba. Mungu ni mkubwa.
 
Hongereni sana wana Ludewa kwa kukamilishwa daraja la mto Ruhuhu. Mimi ni mmoja wa watu wanaofahamu adha ya mto Ruhuhu. Zamani kuvuka pale ilikuwa ni hatari kubwa ya mamba. Mungu ni mkubwa.
Hivi mto Ruhuhu upo ukitoka Lugarawa kuelekea Mavanga? maana mimi nimeishia Lugarawa.
 
..kupiga magoti ni kudhalilishana.

..sijui kwanini Ccm wanapenda huu mtindo wa kupigiana magoti.

..kupongeza sio tatizo, lakini kupiga magoti sio sahihi.
 
Huko ni Manda, kuvuka kuelekea Lituhi.
Ahaa! Manda sijafika nakusikia tu, nimeishia Ludewa Mjini tu. Naona miaka hii wamerahisishiwa usafiri kutoka Manda hadi Iringa.
Nadhani ile lami ikikamilika kutakuwa na usafiri wa moja kwa moja hadi Dar kama wenzetu Makete.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom