singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa tume hiyo ipo huru na haijawahi kuingiliwa kimaamuzi na kiongozi yeyote.
Alisema hayo jana Ikulu, Dar es Salaam baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, na kumpa taarifa ya yaliyojiri katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kampala, Uganda, na kujadili kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Februari 18, mwaka huu.
Alisema, katika kikao hicho ambacho alikuwa Mwenyekiti, wamezungumzia umuhimu wa Tume ya Uchaguzi kuwa huru huku wakichukulia mfano wa Tanzania ambayo imetoka katika Uchaguzi Mkuu miezi michache iliyopita.
Jaji Lubuva alifafanua kuwa Tume ya Uchaguzi inapaswa kuwa huru katika maamuzi yake na kwamba jambo hili limekuwa likifanyika wakati wote hapa nchini. Alibainisha kuwa, wanaosema Rais anapaswa kuingilia kati masuala ya uchaguzi iwe Tanzania Bara ama Zanzibar wanafanya makosa, kwani kwa namna yoyote hana mamlaka hiyo.
“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya Tume,” alisema Jaji Lubuva.