Loyalty ya wabunge wetu ipo kwa chama au kwa wananchi?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kwa sheria zetu mbunge anachaguliwa na wananchi lakini lazima adhaminiwe na chama. Chama kikimuondolea udhamini mbunge, hata kama alichaguliwa na 100% ya wananchi wake, anapoteza haki ya kuwawakilisha. Kama zipo, naomba kujulishwa faida za wagombea kulazimika kudhaminiwa na vyama vya siasa.

Kwa maoni yangu hili ni tatizo kubwa sana katika utendaji wa bunge letu na uhuru wa bunge. Unakuta chama kimeunda serikali. Mbunge anatakiwa kuisimamia serikali iliyoundwa na chama kinachoweza kumuondolea udhamini! Huku ni kama kumfunga bondia mmoja mikono. Kinachotokea ni mbunge kuamua kuwa loyal zaidi kwa chama kilichomdhamini kuliko wananchi waliomchagua, na anaowawakilisha. Anatanguliza maslahi ya chama mbele. Ikitokea maslahi ya chama na wananchi yanapingana, atachagua maslahi ya chama.

Nafikiri hili jambo si la bahati mbaya bali ni muendelezo wa chama kushika hatamu, kwa hila. Kuingia kwenye demokrasia nusunusu ni hatari kuliko kutokuwa nayo. Nchi inaingia kwenye deadlock ambayo inagharimu miaka mingi kutegua. Kwa maoni yangu huu utaratibu wa wagombea kulazimika kudhaminiwa na chama unapaswa ufe, si utaratibu wa kidemokrasia. Chama kisipewe nguvu ya kumuondolea madaraka muwakilishi wa wananchi, na zaidi ni kuwa mtu asilazimike kudhaminiwa na chama ili kugombea nafasi yoyote.

We una maoni gani juu ya loyalty ya wabunge wetu?
 
Back
Top Bottom