Kufuatia Cdm kuwapeleka puta CCM na CUF huko Igunga, na baada ya CCM kupeleka timu ya kampeni yenye watu wasio na mvuto kabisa mbele ya wapiga kura wa igunga, nadhan Edward LOWASA angekuwa ni chaguo bora kuwa mratibu wa kampen za igunga. Lakin kwa upepo unavyovuma huko igunga, sifahamu nani atashinda ila nina uhakika kuwa CCM haitavunja rekodi ya oktoba 2011 ya kura 35,000. Na kama CCM ikishinda basi itashinda kwa aibu(ushindi hafifu) kitu ambacho ni sawa na ushindi kwa upinzani. Kwa sasa, CCM wanapumulia mashine si igunga tu, bali nchi nzima. LOWASA angeweza kushawishi wale wana igunga waliochukizwa na R.A kuachia ngazi kurudi kundini.