Lowassa wao, Dkt. Slaa wao na Tundu Lissu wao. CHADEMA wana nani?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
685
1,000
Huwezi amini lakini prominent figures zote zilizogombea Urais kupiti CHADEMA zilihamia kutoka vyama vingine hasa hasa CCM. Dr Slaa alikuwa CCM kabla ya kuhamia huko, Lowassa alikuwa CCM kabla ya kuhamia huko na Tundu Lissu alikuwa NCCR kabla ya kuhamia huko.
Sasa CHADEMA ni nani bila CCM?

Imekuwa ni kawaida sana wahamiaji hao kupewa vyeo vikubwa sana kwenye chama kama ujumbe wa kamati kuu, uenyekiti wa kanda ukatibu mkuu. Vyeo vyote hivyo hiwafanya wahamiaji hao kujua siri zote za ndani na mikakati ya CHADEMA bila pingamizi.

Je CHADEMA wana ndoto ya kushika dola siku moja kwa mikakati yao hiyo? Je CHADEMA wako serious na siasa za nchi hii?

Leo Lazaro Nyalandu nae karudi zake tena kwa kejeri kubwa na ni mwaka jana tu kidogo CHADEMA wampitishe kuwa mgombea wao.

Kama sio ujio wa LISSU pale CHADEMA hapakuwa na prominent figure ambaye angepeperusha bemdera ya CHADEMA kugombea urais. Siasa za CHADEMA na set up yake kuna shida somewhere.

Kuna siku utasikia hata Mbowe na Mnyika nao wamehamia CCM. Ni mawazo yangu tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom