Lowassa: Wakenya msijilaumu, nchi yenu iko mbele kiuchumi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki

Mwacheni huyo jamani hajui hata anachozungumza. Bahati nzuri alikuwa akizungumza hayo mbele ya rafiki yake Uhuru ili kumfurahisha. Ukisoma daily nation ya hivi karibuni Kenya ipo hoi imeshapitwa na Ethiopia na Tanzania ipo nyuma ya Kenya ikiwapumulia na wakati wowote ule itapitwa na TZ
Utakuwa umesoma vijarida vya pale mtaa wa Lumumba vilivyo haririwa na Dr. wa maganda ya Korosho almaarufu kama Sizonje!
 
Duuh watu wamebanwa hadi wameamua kuhamia nchi jirani..Ngosha endelea kukaza hivi hivi tutaheshimiana tu taratibu. Tukifika 2020 heshima itakua iko juu, chapa kazi ngosha, hapa kazi tu hatuangalii unatembea kwa haraka au pole pole.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kwa tuliofika kenya.Hata kuanzia leo waseme wasimame kufanya lolote,itatuchukua miaka 20 kuwafikia.Sisi tubaki tu kujidanganya tu eti Tanzania ya viwanda,wakati haijulikana hivyo viwanda vitajengwa na nani,ni serikali au wageni.Serikali yenyewe hata hela ya kununua paracetamol mahospitalin haina
 
Wako mbele kila kitu, nilikuwa nao TMA ni watu wasio na unafiki yaani wao kama unajua unajua tu, si wanafiki. Ndio maana hatahata katiba wanayo ss Mzee Sitta samahani marehemu akaiharibu na wenzake.
Sitta aliharibu katiba na wakacheza dansi ndani ya ukumbi wa bunge na wakaangusha na party wakidhani wanawakomoa ukawa!! (Shame on us)

Cairo's
 
Kenya iko mbele kiuchumi na kwa kipato cha mwananchi

Watanzania wangapi wana uwezo wa kufanya utalii,,,,Wakenya wengi wanatembea mbuga za wanyama Tz kama Ngorongoro, Kilimanjaro etc Pasaka na Christmas Wakenya wanafanya utalii mkubwa sana...

Viwanda...Kenya iko mbele sana.....Bidhaa za Kenya ni bora sana

Blue band, Colgate, Nivea, Sabuni za kuoga, mafuta ya kupikia....etc Kenya wana export bidhaa hizi...Je Tanzania ni lini mtaanza kupeleka Kenya bidhaa zenu kama hizi?

Kenya Ina budget kubwa zaidi ya Tanzania na wanajitegemea

Uchumi kukua kwa % kubwa sio uchumi mkubwa...Vilaza wa Lumumba wana comment upumbavu...

Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa % kubwa kuliko USA, Ulaya, Je ....Tanzania ni tajiri kuliko USA....Think before you comment...If you don't know...go away without comment
Acheni ujinga...

Uchumi wa kenya ni mkubwa lakini wananchi wa halo ya chini wana hali mbaya kuliko wakenya.

1. Kenya mwananchi wa kawaida hawezi kumiliki ardhi hata milele...

2. Viwanda vyote ulivyovitaja hapo ni vya wazungu, wahindi na mafisadi walioitafuna kenya baada ya uhuru, na wananchi wa kawaida hawanufaiki navyo kivyovyote...

Dizaini za ukuaji wa uchumi wa kenya ndio zile zile za ukuaji wa uchumi wa nchi kama ethiopia, nchi zinasemwa zina uchumi imara alafu wananchi wanazikimbia nchi zao...

Wakenya wamejazana bongo wanafanya kazi za bar na ualimu wa nursery, waethiopia wako tayari kuwekwa kwenye Kontena ili wakimbie nchi.

Takwimu za benki ya dunia zinatoa kipaumbele kwa sekta binafsi kwa sababu sekta binafsi ndio mwanya wa matajiri kukwiba rasilimali za nchi.... Unaporuhusu sekta binafsi kwenye maswala muhimu ni kama umeruhusu matajiri wale matunda ya nchi kwasababu mwananchi wa kawaida hatokua na mtaji wa kujiingiza kwenye ushindani huu. Huku huku sekta binafsi bado hazijakwepa kulipa kodi!!

Maendeleo halisi ni yale nchi inapoendelea kwa pamoja, haachwi mtu nyuma.

Kenya haina maendeleo yoyote zaidi ya maendeleo ya wawekezaji na madalali wa uwekezaji.

Nawasilisha.
 
hata Tanzania mwananchi wa hali ya chini ana hali mbaya sana mkuu.....bora Kenya wana viwanda afadhali kuna watu wana ajiriwa huko ,....huku Tanzania viwanda hakuna..ajira hakuna wasomi wanazagaa tu mitaani sekta binafsi ndio kiungo cha maendeleo.......bila sekta binafsi maendeleo hakuna
 
Leo Mh. Lowasa anaisifia Kenya na kuendelea kusema wasiogope. Sio miaka mingi alikuwa Waziri mkuu wa Tz. Je, anakumbuka takwimu zilivyokuwa zinasema? Je, Kenya kuwa na uchumi mzuri anavyousema, anajua ni wananchi wangapi wanaofaidika na uchumi huo?
 
Kulingana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambapo Tanzania inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, Je, Lowassa kadanganya au yuko sahii kusema nchi ya Kenya iko mbele kiuchumi?
Kenya nawapa heshima kwa vitu viwili

1. strong labour union
vyama vya wafanyakazi vikitoa tamka Hon Kenyatta anaitisha kikao na magavana wa county's kuwajibu unlike huku mlingwa na msukuma wakiongea wanasauti kuliko CWT na OTTU

2.democracy
hapo hakuna maelezo tunaona NASA walifanya IEBC yote ikaenda huku sasa mkurugenzi wa NEC anaunyamazisha upinzani na unatii
yani akiongea Msajili wa vyama, lubuva ,Jecha, IGP, RC na waziri utafikiri speech zao kaandika mtu mmoja

3. finaly independence of judiciary na katiba bora africa mashariki na ya kati
 
Duuh watu wamebanwa hadi wameamua kuhamia nchi jirani..Ngosha endelea kukaza hivi hivi tutaheshimiana tu taratibu. Tukifika 2020 heshima itakua iko juu, chapa kazi ngosha, hapa kazi tu hatuangalii unatembea kwa haraka au pole pole.

Post sent using JamiiForums mobile app

tuta heshimiana zaidi tukiwa kwenye makambi ya wakimbizi nchi za watu

mxiieeeeuu
 
Back
Top Bottom