Lowassa: Wakenya msijilaumu, nchi yenu iko mbele kiuchumi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki

Wako mbele kila kitu, nilikuwa nao TMA ni watu wasio na unafiki yaani wao kama unajua unajua tu, si wanafiki. Ndio maana hatahata katiba wanayo ss Mzee Sitta samahani marehemu akaiharibu na wenzake.
 
Haya ndio madhara ya kusomea shahada za kiswahili na PSPA. Unashindwa kuelezea tofauti ya ukuaji wa uchumi na uchumi uliokua. Kenya inaspeed ndogo kukuza uchumi ila uchumi wake ni mkubwa zaidi ya tz but tz inakua haraka kiuchumi zaidi ya Kenya.
Mfano uliowazi ni China na USA usiwaze sana.
Au nikuulize mwandishi swali kuwa. Mtoto na kijana au mzee kama utakaa nao kitaa kimoja au nyumba moja, ni yupi machoni pako ataonesha ukuaji wa haraka zaidi ya mwingine?
Probably mtoto kisha kijana na baadae mzee huwezi kumuona akikua bali baadae sana utabaini kuwa naye anakua kwani ngozi yake na muonekano wake utazidi kuonesha uzee zaidi, ndio maana mzee wa miaka 60 hafanani kimuonekano na mzee wa miaka 90 alikadhalika na yule wa miaka 110 ingawaje wote ni wazee.
Uchumi is all around us like an environment

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Exactly kiuchumi Kenya wapo juu hili halihitaji kutoa povu ni LA kitakwimu sema sasa uchumi wetu unaonyesha Steady Growth tuende hivyo in the Long Run tutawafikia tukitengeneza pillars nzuri kwa mfano Kenya kwa sasa vijana wengi wanaomaliza Elimu ya juu wanaajiriwa na sekta binafsi sisi ni kinyume chake

Post sent using JamiiForums mobile app
Mnapata wapi "facts" za kusifia uchumi wenu unakua ikiwa kila siku tunashuhudia business "closure" na retrenchment. Tieni akili nchi haiongozwi kwa matamko au kuchukia sehemu fulani ya watu.
 
Ukuaji wa uchumi wa Marekani unaweza kuwa 0.1% kwa mwaka lakini utakuwa bado ni mkubwa maradafu kuliko uchumi wa Tanzania hata kama utakua kwa 10%.

Hesabu ya kuelezea hilo ni sawa na mtu akiwa na sh. 10,000. Ukuaji wa 10% utamfikisha kwenye 11,000. Lakini mwenye 100,000 ukuaji wa 5% utamfikisha 105,000. Uchumi wa Kenya ni karibia mara 10 ya ukubwa wa uchumi wa Tanzania.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
kulingana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambapo Tanzania inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, Je, Lowassa kadanganya au yuko sahii kusema nchi ya Kenya iko mbele kiuchumi
Huyu ndiye ambaye wamasai woooote afrika mashariki....wamemteu/wamemchagua kuwa laigwanan wao kaupateje huo ulaigwanan wakati yeye ni mmeru! ?kama vip.....ahamie huko kwenye uchumi mzuri
 
soma heading yako na message yako utagundua ni vitu viwili tofauti kuna kuwa mbele kiuchumi na kuongoza katika ukuaji wa uchumi
 
Tutawapita Kenya soon tukipata fedha za makinikia Trillion 108 kila MTU akianza kuwa na Noah yake Africa Mashariki tutakuwa na uchumi ya Noah ambapo sio Jambo dogo kama unajua Bei ya kinguruwe kimoja ambapo kinapiga safari za kila kichwa miatano na moshi Tarekea 3000

Post sent using JamiiForums mobile app
Hahaaa kweli ww mkuu umetuvuruga kabisaaa ndoto za Noah

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Nyie bakin na uchumi wenu wa kwenye magazet na vinywani mwa governor of BOT na wenzake.......Over.....

Post sent using JamiiForums mobile app
 
kulingana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambapo Tanzania inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, Je, Lowassa kadanganya au yuko sahii kusema nchi ya Kenya iko mbele kiuchumi
Mwacheni huyo jamani hajui hata anachozungumza. Bahati nzuri alikuwa akizungumza hayo mbele ya rafiki yake Uhuru ili kumfurahisha. Ukisoma daily nation ya hivi karibuni Kenya ipo hoi imeshapitwa na Ethiopia na Tanzania ipo nyuma ya Kenya ikiwapumulia na wakati wowote ule itapitwa na TZ
 
kulingana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambapo Tanzania inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, Je, Lowassa kadanganya au yuko sahii kusema nchi ya Kenya iko mbele kiuchumi
Speed yetu ni kadi kuliko yao ila tayari wako mbele yetu kwa kitambo. Labda wanaishiwa mvuke.
 
Haja danganya ila hekima yake ni sufuri, wakati anausifia uchumi wa Kenya kama kiongozi wa kaliba yake ange takiwa aweke mambo kwenye mizania, Kwamba wakati Kenya wakishirikiana na makaburu kuwekeza viwanda sisi kama taifa la Tanzania mali na damu zetu zikimwagika kupambana na hao makaburu . Leo Kenya na Wengine Afrika wanafurahia huo Uhuru tulio upigania kwa hali na mali kwa kuwekeza katika uchumi. Tumshukuru Mungu kwa kuendelea kutuepusha na aina hii ya viongozi.

Na washawasha!
 
Tutawapita Kenya soon tukipata fedha za makinikia Trillion 108 kila MTU akianza kuwa na Noah yake Africa Mashariki tutakuwa na uchumi ya Noah ambapo sio Jambo dogo kama unajua Bei ya kinguruwe kimoja ambapo kinapiga safari za kila kichwa miatano na moshi Tarekea 3000

Post sent using JamiiForums mobile app
Kila mtu atakua na Noah yake, sasa abiria utapata wapi wa kulipa hiyo 3000

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Haya ndio madhara ya kusomea shahada za kiswahili na PSPA. Unashindwa kuelezea tofauti ya ukuaji wa uchumi na uchumi uliokua. Kenya inaspeed ndogo kukuza uchumi ila uchumi wake ni mkubwa zaidi ya tz but tz inakua haraka kiuchumi zaidi ya Kenya.
Mfano uliowazi ni China na USA usiwaze sana.
Au nikuulize mwandishi swali kuwa. Mtoto na kijana au mzee kama utakaa nao kitaa kimoja au nyumba moja, ni yupi machoni pako ataonesha ukuaji wa haraka zaidi ya mwingine?
Probably mtoto kisha kijana na baadae mzee huwezi kumuona akikua bali baadae sana utabaini kuwa naye anakua kwani ngozi yake na muonekano wake utazidi kuonesha uzee zaidi, ndio maana mzee wa miaka 60 hafanani kimuonekano na mzee wa miaka 90 alikadhalika na yule wa miaka 110 ingawaje wote ni wazee.
Uchumi is all around us like an environment

Post sent using JamiiForums mobile app
hivi uchumi wa kenya ni sawa na TZ?hata mtoto mdogo anajua kenya wapo vizur POLITICAL,ECONOMICALY na hata sasa wanaanza kutuacha katika mambo ya kijamiii,hebu mtoke walau mara moja mpite nchi jirani huko muone watu walivyp professional na sisi kutwa tunawaza siasa na kukomoana
 
Back
Top Bottom