Lowassa: Wakenya msijilaumu, nchi yenu iko mbele kiuchumi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki

Sisi huku private sector zinakufa
..sasa sijui hiyo growth inaokea wapi

Post sent using JamiiForums mobile app

Tuko kwenye nchi zinazoongoza kwa kupika tafiti duniani... siwezi shangaa kama hata data zetu ni za kupika...
 
Kenya ni habari nyingine katika Nchi za Afrika Mashariki,kwa tunaoifuatilia kwa makin.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ukiangalia gdpya Tanzania ni dolaza kimarekani 943 kwa mwaka kwa kila mtanzania . na Kenya kila RAIA ana 1420 dola kwa mwaka . na wastani Wa uchumi Wa Kenya ni 6% na Tanzania ni 7% .MTU anayependa kujua Tanzania ataipita link Kenya afanye hizo hesabu juu atueleze ni link Tanzania ataipita Kenya kwa kutarajia kuwa miaka yote hiyo kila kitu kitabaki kama kilivyo. Tanzania ilikuwa na fursa ya kuipita Kenya laki tulishindwa kutumia fursa. Miaka ya 1970 Tanzania ilikuwa inakua haraka kuliko Kenya lakini vijiji vya ujamaa vilipoteza uelekeo na hili Mwalimu alikiri baadaye kuwa katika makosa aliypfanya ni kuwahamisha wazalishaji kwa njia ya ujamaa na jingine alikiri ni kuvunja serikali za mitaa ambazo wananchi waliziamini na kuziendesha kwa faida yao. Sasa tukirudi kwenye mada tukubali kuwa Kenya kiuchumi wanatuzidi. Ila kwa ubora Wa maisha Tanzania tunawzidi Kenya ndiyo maana wastani Wa maisha ya mkenya ni miaka59 na mtanzania wastani Wa miaka 62. Sababu take Tanzania tunakula vizuri kwa sababu tuna Ardhi nzuri na mvua nzuri mikoa mingi lakini Kenya maendeleo yao yote yako majimbo mawili central na Rift valley lakini Kle kaskazini karibu nusu yote ya Kenya ni shida tupu.Hii inanikumbusha miaka hiyo (1975) kulifanyika mashindno ya riadha afrika mashariki kwa kweli wanafunzi Wa Kenya walionekana wachovuna kushangaa eti hivi high school nzuri hivi inaweza kuwa interior kam iringa? Kwao ukiongea Kenya fikiria kisumu /eldoret/ Mombasa/kericho/. Pale panapopita reli na maeneo yanayozunguka karibu ndiyo hiyo Kenya inayotuzidiNa kwli wanatuzidi kwa huo uchumi mnaoongea kwenye mitandao ila kama tungehesabu kila mwananchi Wa Kenya na Tanzania anakula calories ngapi nadhani tunawzidi .ninaweza kuelimishwa.( I stand to be corrected.) Mchango wangu kama ninamkwaza mzalendo kipofu Wa mahali popote anisamehe sio dhamira yangu. Maana hakuna njia tuliyopewa na MUNGU kuelimishana ispokuwa kwa mawasiliano kama haya.

Post sent using JamiiForums mobile app
mkuu sasa inakuwaje Kenya watuzidi kipato kwa mwaka halafu sisi tuwazidi ubora wa maisha? Kenya walichotuzidi ni viwanda tu mambo mengine tumewazidi
 
Hili la OMO AU KOMESHA?
cjakataa kutuzidi kiuchumi ila speed yetu ni kubwa kuliko wao hebu rudia kusoma kwa makini sana utanielewa

Post sent using JamiiForums mobile app
Hiyo kas unayoizungumzia ni ya nini? mkuu,dadavua hapo

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Tufike mahali watanzania tukubali ukweli..ubishi waki.pu..mv tuache

Kenya iko mbele kiuchumi na wametuzid mambo mengi zaid...tusijitie moyo kuona fly ove mmoja inajengwa tz ndo tuanze kupata kibur..
Wakenye wanachapa kazi sana..tanzania bado hatuna roho ya kuthubutu...kila mtu yuko after business za mwezie..huku ni kufatiliana badala ya kufanya kazi...tunamaliza mda mwingi kwenye majungu badala ya utendaji kazi....
Wajinga mtabisha ila fact ndo hiyo
Acheni tuonwe maboya maana tumekalia majungu tupu...
Shame on us
 
Mimi nikiangalia media zao tu napata picha halisi kwamba hawa sio wenzetu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Traffic wakikazana kwenye kukusanya faini kwa bidii na moyo wa dhati kabisa,,kenya atatukamatia mbali sana kiuchumi
 
Mnapata wapi "facts" za kusifia uchumi wenu unakua ikiwa kila siku tunashuhudia business "closure" na retrenchment. Tieni akili nchi haiongozwi kwa matamko au kuchukia sehemu fulani ya watu.
Sasa huyu wa retrenchment nae sijui ina uhusiano gani na uchumi lakini retrenchment unaweza kufanya kama unataka ku down size the company!!! haina uhusiano na kufilisika, hata hivyo uchumi wa Tz wakati wa JK ulikuwa unakua kwa 7% lakini yote sababu ya madawa ya kulevya. Sasa hivi ndio kuna uchumi halisi kila senti ina thamani
 
Hii kauli yà lowasa iko kikampeni zaid. Mwenye macho matatu kashaona

sent from kitochi using jamii forum
 
Back
Top Bottom