Lowassa vs Magufuli: Nani anagusa maendeleo? Changia

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Muda wa kampeni umeanza kuisha na kama kawaida ya wananchi wa nchi hii ya Danganyika na Zanzibar wamekuwa kama wale dada zetu toka mkoa ulee wanaosema jiangusiage tu, sambi zako mwenyewe!

Hakuna mwananchi anayetaka kutambua nini hasa package iliyoandaliwa na vyama na mgombea pia nafasi zao katika kutekeleza yale ya vyama na haya ya wananchi!

tumabakiwa na wiki 2 + tu kufikia siku ya uchaguzi, hadi sasa agenda inayotamba ni wingi wa watu ktk kampeni, so kila team inatengeneza mbinu, watu wa coverage na wapiga debe kuwa wananchi walifurika hadi pakukaa pamekosekana.

katika kujenga nchi, lazima kuwe dira, ambayo inategemewa zaidi kuelezewa na sera na ilani za vyama huku wagombea wakiainisha mipango mkakati waliyonayo kufikia malengo ya muda mfupi na muda mrefu.

vitu ambavyo vinakosa mikakati ni pamoja na:-

Kukosekana kwa plans za maendeleo

vitu kama havijawa kwenye plans hata vikiwa vizuri namna gani hakuna jinsi utekelezaji wake utafanyika kwa ufanisi.
Mfano vitu kama elimu, afya, miundo mbinu na mipango miji, maji na umeme nadhani muhimu sana, hakuna mpiga kura au kiongozi asiyejua umuhimu wake kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja.

katika kampeni za mwaka huu au hata kipindi cha kikwete vitu vyote hivi vilikuwa vinagusiwa kwa kiwango kikubwa kama kero za wananchi au mikakati ya wagombea.

tatizo kubwa jinsi wagombea wanavyoa address hoja husika ni kwamba wote wamejikita katika kuonesha tatizo, jambo ambalo hata kijana wa miaka 9 anaweza kukuonesha kero hizo!

Muda na speed ya mabadiliko haviko realistic

Ahadi zao nyingi ni kati ya siku 100 - miezi 6, sasa hatujui kama hii mipango inafikiwaje ktk kipindi kifupi hivyo na sustainability plan ikoje?
Nahisi kama kampeni bado hazijaanza kwani bado hatujasikia dira yetu ni kuelekea wapi, lini na kwa kasi ipi?
Hatujajua wagombea wetu wanazungumzia mikakati ya miaka mitano, 10, 20, au 50?

Kushindwa kuainisha vyenzo za kuboresha viashiria muhimu vya maendeleo

Maendeleo yanapimwa kwa indices ambazo zinajieleza na tunaweza kuziwekea mikakati!

Wagombea wote wa ccm na ukawa bado wameshindwa kuzirejea indicators husika na kujibu kama wameridhishwa na speed ktk maeneo hayo, au wameshagundua kwanini hatukufikia viwango au kwanini tulivuka viwango na tunataka kumaintain nini, na kureview ikiwezekana kuboresha maeneo gani?

katika miaka 10 ya kikwete Tanzania imekuwa sana ktk viwango vya maendeleo (Human Development Index) kama inavyoainishwa na UNDP. Tanzania imefanya vizuri sana ktk miaka 15 iliyopita. Kwa nchi za uchumi wa kati na wa chini Tanzania imekuwa na average annual HDI growth ya 2% ambayo ni kubwa ktk makundi yetu ya watu maskini. lakini 2% sio ukomo wa growth, kwanini tunakuwa kwa speed ndogo namna hii wakati tuna rasilimali za kutosha?

je kuna matumaini yeyote kwa hawa wagombea wetu?

Kuna kigezo cha elimu kimegusiwa vema ingawa hakina mikakati, ukuaji wa uchumi na pato la taifa magufuli analizungumzia zaidi lakini naye haoneshi ana mikakati gani, usawa wa kijinsia na afya hakuna mikakati iliyowazi. kupunguza umaskini Lowasa analiongea kila kukicha ingawa plan anaijua yeye mwenyewe!

Je, tunaweza kuwafanya wagombea wawajibike kuelezea mipango yao?

Kuna namna wagombea wetu wanaweza kutuelezea mipango yao?

au wale wazee wa kuhudhuria mikutano au wasikilizaji wazuri mnaweza kuwatolea maelezo jinsi walivyofafanua namna watavyoweza kukuza uchumi na kufikia vigezo vya juu vya maendeleo ndani ya miaka 5 na beyond?

my take:
uchaguzi Tanzania umekuwa hauna tija miaka yote kwa kuwa wagombea na vyama vyao wana build ktk personalities za wagombea na kuishia kupigana vijembe tu vya uhandsome, ugonjwa, ushababi wa kazi etc! nadhani watanzania tushtuke kuwa tunataka brain, tunamuhitaji mtu mwenye mikakati inayoendana na mahitaji ya wananchi, dira ya taifa letu, sera za chama chake na uwezo wake binafsi ktk kusimamia utekelezaji!
 
Back
Top Bottom