Lowassa: Utajiri wangu usitumike kwa lengo la kuchafuana katika siasa, ndugu zangu aliyepata amepata

zinc

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,392
1,066
Ndugu wana JF,

Mkubwa wa kazi ambaye amewahi kushika nafasi kubwa za uongozi katika taifa hili na mwenye kasi ya ajabu katika medani za siasa, uchumi katika chama chake, amekuwa akiwaonya wapinzani wake kutotumia kete ya mali zake kama njia ya kumchafua ki siasa.

Amesema hapendezwi na hilo, na jambo hilo halina tija kwa siasa zetu za Tanzania, kuna mijadala mingi ya ki taifa ya kujadili kwa maendeleo yetu na siyo mali zake kwani anazo mali za kawaida kuliko inavyozushwa.

Kakazia kwamba wapinzani wake wasijikite katika mali zake kwani "ALIYEPATA AMEPATA".

Haya wadau hizi ndiyo siasa za bongo watu wamewekeza kwenye kuchafuana tu. Chama cha CCM kazi ipo.
 
Ndugu wana JF,

Mkubwa wa kazi ambaye amewahi kushika nafasi kubwa za uongozi katika taifa hili na mwenye kasi ya ajabu katika medani za siasa, uchumi katika chama chake, amekuwa akiwaonya wapinzani wake kutotumia kete ya mali zake kama njia ya kumchafua ki siasa. Amesema hapendezwi na hilo, na jambo hilo halina tija kwa siasa zetu za Tanzania, kuna mijadala mingi ya ki taifa ya kujadili kwa maendeleo yetu na siyo mali zake kwani anazo mali za kawaida kuliko inavyozushwa.

Kakazia kwamba wapinzani wake wasijikite katika mali zake kwani "ALIYEPATA AMEPATA".

Haya wadau hizi ndiyo siasa za bongo watu wamewekeza kwenye kuchafuana tu. Chama cha ccm kazi ipo.

so the end justifies the means
 
Wapinzani uchwara ndani ya chama kama joka la mdimu wanataka kuchafua watu wakati wanajua kabisa kuwa hawakubaliki kwa wananchi kwa sababu ya udhaifu wao....we tokea lini rais wa wananchi zaidi ya watu millioni 46 achaguliwe na mtu moja eti mke wa rais....na organization yake ya WAMA...sifa kubwa ya mwanaume ni kupigana vita iwe jangwani au baharini
 
We hujui jinsi Lowasa alivyomnyonyoa Mwakyembe nywele?
Naona umesahau huyo jamaa yenu alichomfanyia Ulimboka, Kibanda...na leo kuna uzi umeleta details ya kambi yenu kuhusu jamaa yenu mwanza Dialo kuhojiwa polisi kwa mauaji ya katibu msaidizi wa CCM (rejea uzi wa AL Sadat)...kambi yenu naiogopa kama ukoma ni watu wa vitendo vya kuangamiza kabisa aisee....Hata Mwakyembe ni jamaa yenualifanya mipango ili ionekane kuwa ni maadui zake wa kipindi kile (saga la Richmond) kumbe mgombea wenu ndio aliratibu mambo yote....aisee nyie watu hatari sana sana, ni wa kuogopwa kama ukoma
 
Kama ALIYEPATA KAPATA ndiyo slogan yenyewe basi mali hizo za Lowassa haziwezi kuwa za kawaida; na kama sio za kawaida ndio maana wenye nchi wanadadisi huo utajiri ni wa halali au haramu?
 
Labda sijakuelewa lakini nafikiri suala la uwezo wa mgombea kiuchumi na jinsi alivyopata ni muhimu kama uadilifu wa mgombea bado ni sifa ya uongozi.

Kama mgombea fulani anasemekana kutajirika kwa muda mfupi au mrefu lakini katika utumishi wa umma anao wajibu wa kuuridhisha umma anouomba ridhaa namna alivyozipata ili uadilifu wake upimwe.

hivi kuna kipimo kipi kwamba Lowassa anakubalika na watu? Ameushiriki uchaguzi upi uliompatia kura za kumpa matumaini hayo. Mbona aligwaya uchaguzi wa NEC na akakimbilia Monduli wakati wenzake wakipanda kwenye kapu? Populairty unaipimaje?
 
Kama mali zake zilitumika kuupata huu URAHISI sidhani kama aliyesaidiwa pia hatakuwa ni wale wale.Waswahili wanasema hivi...Nionyeshe rafiki zako nitajua Tabia yako.
 
Naona umesahau huyo jamaa yenu alichomfanyia Ulimboka, Kibanda...na leo kuna uzi umeleta details ya kambi yenu kuhusu jamaa yenu mwanza Dialo kuhojiwa polisi kwa mauaji ya katibu msaidizi wa CCM (rejea uzi wa AL Sadat)...kambi yenu naiogopa kama ukoma ni watu wa vitendo vya kuangamiza kabisa aisee....Hata Mwakyembe ni jamaa yenualifanya mipango ili ionekane kuwa ni maadui zake wa kipindi kile (saga la Richmond) kumbe mgombea wenu ndio aliratibu mambo yote....aisee nyie watu hatari sana sana, ni wa kuogopwa kama ukoma

Makubwa haya hebu tupeni news
 
Ukwel mchungu maadui wengi wasiopenda kuusikia,well said our coming prezda
 
Back
Top Bottom