Lowassa usihutubie kumbukumbu ya Nyerere wilaya ya Mwanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa usihutubie kumbukumbu ya Nyerere wilaya ya Mwanga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Oct 12, 2012.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kuna habari ndani ya gazeti la mwananchi kuwa Lowasa waziri aliyejiuzulu kwa ajili ya kashfa atahutubia katika kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha mwalimu huko , lambo islamic high school , wilayani mwanga. tuaambiwa kuwa atatoa mada kuhusu elimu na ajira

  ninamshauri lowasa asishiriki kabisa kwenye hafla hii ya kumkumbuka mtu ambaye watanzania walimliilia sana kwa sababu zifuatazo

  1. MWALImu mwenyewe hakuridhika na uadilifu wa mtu huyu lowasa tangu akiwa hai, alimkataa kata kata asiwe mmojawapo wa wagombea kiti cha urais wakati ule. wakati huo lowasa hakuwa na ukwasi wa kutisha kama alivyo nao leo, lakini jitihada za kujimbilikizia mali mwalimu aliziona dhidi ya mtu huyu.


  2. wakati huu wa kuelekea kumalizika kwa chaguzi ndani ya ccm, lowasa amekuwa gulio kubwa la kununua kura, kuangusha wale ambao ni tishio kwake, mbaya zaidi wale ambao anadhani wanajua uchafu wake huu. lowasa amemaliza safari ya kununua wananchama wake wa ccm, sasa ameanza safari ya kuandaa mtaji wa kununua watazania wote, pesa anazo kupitia symbions anakovuma 145m kwa siku, acha vodacom kupitia alphatel na wizi mwingine kupitia wapambe wake akina rostam, nk

  3. kwa uadilifu wa mwalimu mtu huyu asingethubutu kamwe hata kulisogelea kaburi lake, mbaya zaidi kuhutubia kuhusu mwalimu iltakuwa sawa na wale wahubiri maarufu "wanaohubiri ubora wa kunywa maji wakati wao wanakunywa divai

  ninazo sababu nyingi, lakini naomba WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA WETU TUUKATAE UNAFIKI WA MTU HUYU HATARI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Alitakiwa atumie siku hii nzima kucheza na wajukuu, si kuongea na waTz kwa mgongo wa Mwalimu.
  Hakuna hata milimita moja ambapo anafanana na Mwalimu.
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hakuna matatizo Lowassa akihutubia siku hiyo ya Nyerere Day,sidhani kama kuna mtu yoyote katika Familia ya Nyerere atapinga.

  Lowassa wakati wa miaka 50 ya Uhuru alikua anaongea TBCI, utafikiria siku ile ilikuwa birthday yake.

  Hakuna tatizo kwa Lowassa kuongea katika hiyo siku [from the point of view of the family, kwa sababu ile siku ni National Holiday]
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ahsante mkuu wangu, watu kama nyie tunawategemea sana, ukienda pale udsm utakutana na maprofesa fulani wenye akili fupi, wanampa kichwa mtu huyu, eti tunahitaji kuwa na dikteta rais ajaye..........hata kama kiongozi angekuwa mzuri kias gani, hata kama akihutubia masaa 10 bado mna hamu ya kumsikiliza, hata kama tb joshua amemtabiri, rushwaaaa peke yake, wizi wa kununua kura, mtandao wa wezi,,,unamwondolea sifa zote hizi na hatufai...
   
 5. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Andrew Nyerere

  Tumekuelewa, tunaheshimu sana demokrasia aliyoijenga mwalimu katika nchi na hata katika familia yake, tulitaka tu lowasa apewe muda wa kutubu, pia asitumie mgongo wa mwalimu kuendelea kudanganya watanzania. Ndo maana nikasema "asije akahubiri ubora wa kunywa maji wakati yeye anakunywa divai kama alivyozoea.

  Lowassa na mwalimu ni kama mlima na bonde au giza na mwanga
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Zoote ni mbinu za kusafishana! Kaitwa na Prof. Maghembe????
   
 7. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nyerere alimkataa lowassa 1995,alimwambia wewe kijana mdogo umejilimbikizia mali,umetoa wapi halafu unataka kwenda ikulu,ikulu kuna biashara gani? alisema tumuogope kama UKOMA.
   
 8. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1,267
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  jamani na mimi nawakilisha, kwa kutokuwa na mawazo kama ya msomi mmoja ambaye ni kiongozi ktk nchi hii ikitokea ukihoji utendaji wake kwa umma jibu lake hana muda wa kujibizana na watoa hoja kwani ni darasa la saba. sasa mimi napenda kushauri umma wa watanzania wenzangu, tukazanie, tuilinde na tuitekeleze dhana ya kusikilizana na kujadiliana kwa hoja. mwl nyerere ni kiongozi wa wote si wa watu wa chache na ni kiongozi aliyekuwa na falsafa zake pindi anapoamua jambo lake lifanikiwe , 1995 nani asiyejua kuwa chaguo la mwl lilikuwa mh, ben mkapa , ili apite kuwa mgombea wa ccm, kifanyike nini kikwazo ninini? hapo mwl alijipanga kwa hoja , kuwapangua wagombea wote tishio kwa mgombea wake, haina ubishi nyota ya lowassa ilikuwa kali akatumia mbinu, kumzima kama unavyojua huwezi kubishana na baba wa taifa kijana akapoa na kuelekeza nguvu zake kwa swaiba wake kikwete , naye alipanguliwa kwa hoja za mzee nawakumbusha mzee hakusema na tusimsemee maneno ambayo hakuwahi kuyasema juu ya lowassa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ni mchapa kazi tegemeo kwa taifa kafanya mengi mazuri kwa taifa nawakilisha'
   
 9. S

  Sanare S Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi nyerere ni binadamu kama binadam awaye yote na kila jambo na wakati wake, wakati wa mwalimu ni kipindi tofauti na sasa japo kuna ya kuigwa kwa sasa. Vilevile haki ya kimsingi ya kidemokrasia haimnyimi mtu kugombea au kumchagua yeyote ampendae. Zaidi sana haimnyimi mtu yeyote kutoa aoni au kuzungumza chochote pasipo kuvunja sheria, pasipo shaka lowasa nae anastahili haki hizi. Natambua kuwa 2015 ndiyo shida na sii lowassa, nitampongeza mh lowassa endapo ana nia hii na yeyote mwenye nia hii ajitokeze bila kuogopa ili wawe wengibtupate fursa ya kuchagua kwani kuna ule usemi usemao "nothing is good or bad but by cmparison" mwsho wosia wangu ni kuwa "let democracy lead the way" tuachevdemocrasia ituonyeshe njia.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sifa kuu ya mtu yeyote anayetaka kuwa kiongozi wa nchi ni kuwa MUADILIFU. Kiongozi muadilifu anakuwa mstari wa mbele kutatua kero zinazowakabili wananchi, je Lowassa ana sifa hizo? Wengi wanamsifia kuwa ni mchapa kazi na mtoa maamuzi , inawezekana ni kweli lakini hayo maamuzi na uchapa kazi huo ni kwa faida ya wanannchi walio wengi au kwa kikundi cha watu wachache?

  Tukiangalia utendaji wake wa kazi kabla ya kulazimishwa kuachia ngazi kwa kashfa tunaona kwamba kweli alihusika na uanzishwaji wa sekondari za kata ; shule hizi ndizo hizo zinazotoa wanafunzi wanaohitimu wakiwa na elimu duni kwa kukosa waalimu na nyenzo nyingine za kujifunzia. Alitoa maamuzi juu ya uzalishaji wa umeme kwa kushinikiza kampuni ya Richmond ipewe tenda ya kuzalisha umeme ambayo haikustahili na ikagundulika kuwa yeye binafsi alikuwa mnufaika katika tenda ile!!

  Sasa kwa mifano na vigezo vyote hivyo ,je Taifa letu linamhitaji mtu kama huyu kuliongoza baada ya kupata dhiki ya utawala wa kifisadi wa Kikwete wa miaka kumi? Jibu lake ni hapana, tunahitaji kiongozi atakayetuletea maendeleo kwa kuwa na ZERO TOLERANCE ON CORRUPTION badala ya kiongozi wa kuwalinda wala rushwa na Lowassa hana qualificatios hizo!!
   
Loading...