Lowassa: Urafiki wangu na Kikwete utaendelea mpaka kifo kitakapotutenganisha

Ni kweli kabisa anavosema mh lowassa ukifatilia kwa makini ndio utagundua anachosema, ukirejea inayoitwa kashfa ya richmond wakati kina mwaykembe wanamshushia tuhuma lowassa ya kuitia hasara serikali rais kikwete kamtetea mbele ya wazee yalompata lowassa ni ajali ya kisiasa. Ukirudia vua gamba wakati nape mishipa ya shingo inataka kumtoka pamoja na kina chiligati msekwa na mukama na wakajiapiza baada ya siku 90 kama hajaondoka atafukuzwa ilipofika wakati wa maamuzi rais aliomba ushahidi dhidi ya lowassa alokuwa nao aulete nape akabaki kutoa macho kina chiligati na mukama msekwa wakavuliwa wao gamba mwenyekiti akalinda urafiki wake rudia kufungiwa kwa makada sita lakini mlengwa ni lowassa nape akawa anatumika kupiga kelele pamoja na viapo vya uongo kwamba lowassa anakiuka taratibu na anakiburi kuna uwezekano wa kuongezewa adhabu ulipofika wakati wa vikao hakukutwa na hatia yoyote na akaruhusiwa akagombee yote hiyo kazi ya rafiki yake laiti mwenyekiti angekuwa mangula na katibu nape lowassa asingekuwa mmoja wa mgombea na hata hiyo nguvu inayosemwa lowassa anayo ni kwa sababu rafiki yake anataka awe nayo.
 
Akizungumza jana Bagamoyo alipokwenda kutafuta wadhamini, Lowassa alisema,"Bagamoyo ni nyumbani kwangu kwa pili, kwa sababu ni nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni rafiki yangu. Nataka niwaambie kuwa mimi na Jakaya ni marafiki wakubwa, na urafiki wetu utaendelea hadi Mwenyezi Mungu atakapotuchukua."

Chanzo: Mtanzania, Jumatatu, 29.6.2015, Lead story.

MY TAKE: Lowassa hapa anatuma ujumbe kwa Kamati Kuu kwamba, Jakaya ambaye ni rafiki yake mkubwa hivi, hawezi kukubali kuona jina lake linakatwa, NI LAZIMA liingie katika tano bora!

Inaelekea keshamtupa tayari! Ila kwa kuwa hataki lawama kamkabidhi kwa wazee wastaafu halafu yeye aseme "Mimi Simo"! Ni hawa wazee ndio wamekuangusha! Halafu ukimwambia si uliwapa maelekezo atajibu: Si wangechanganya na za kwao!
 
Ndani na nje ya JF, Mh. Lowassa kaandikwa sana lakini bahati mbaya hakuna bandiko la wazi linalobainisha waziwazi pasi na shaka mazuri au mabaya ya Kiongozi huyu. Halipo hilo. Kwa hiyo sitegemei kwamba kelele hizi zitakuwa ni spring board kwa wana ccm kumtosa mtu kama huyu hata asiwemo kwenye top five.

CC. Pasco na Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Ndani na nje ya JF, Mh. Lowassa kaandikwa sana lakini bahati mbaya hakuna bandiko la wazi linalobainisha waziwazi pasi na shaka mazuri au mabaya ya Kiongozi huyu. Halipo hilo. Kwa hiyo sitegemei kwamba kelele hizi zitakuwa ni spring board kwa wana ccm kumtosa mtu kama huyu hata asiwemo kwenye top five.

CC. Pasco na Salary Slip
Nyerere tu ndie angeweza kumaliza hili jambo kwa kuweka wazi pumba na mchele ila hawa wa leo hamna mwenye huo ubavu kwani wote ni wale wale tu.
 
Last edited by a moderator:
Hili ni swali muhimu kwa kuwa tunaelekea kwenye uteuzi wa mgombea urais kupitia ccm.
Tumesikia mengi lakini kubwa ni kuwa hawa mabwana hawakujutana barabarani yaani ni maswahiba waliosaidiana.

Inawezekana kuwa EL ana siri nzito dhidi ya Jk ndio maana EL anaonesha matendo na maneno ya kumblackmail Jk.

Inawezekana Jk anatafuta mbinu za kuntisa EK na inashindikana.

Je tuamini marafiki hawa wamekosana?


Je Mh Jk ameamua kumtosa El lakini anaogopa matokeo?
 
kweli inawezekana anamuongopa maana nasikia hata kwenye vikao vyao wameongeza nafsi kutoka 5 adi 7 maana yake ni ni ni? kikwete anapanua mlango ili mende, sisimizi, na panaya buku waingie, akufanya hivyo si tu tutamkubuka bali atakuwa kiongozi wa historia miongozi wa marais ktka chama cha ccm,
 
Kitendawili cha siku nyingi kuhusu urafiki wa viongozi hawa waiwili utateguka baada ya uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015, watakaoanguka, watakao pata mshtuko, watakao furahia kuanguka himaya ya chama kwa ajili tu ya kuuthibitisha urafiki wao wa kweli utakapo juulikana

Tusubiri na kuona mwenye mapengo kayatafute meno ya pembe ubandike. usijkuchekwa!
 
Kwani Lowasa na Kikwete ni maadui sasa hivi?
Kikwete ana marafiki na ndugu wengi, je wote wangegombea urais angewapitisha?
Anayeweza kusema urafiki wao una matatizo ni wao wenyewe!
 
Mbio za sakafuni huishia ukinoni. Kile kitendwili cha uda mrefu cha kuhalalisha usemi kuwa Lowassa na Kikwete, urafiki wao hawakutana barabarani sasa kitateguka tarehe 25 O ktoba baaada ya uchaguzi. Masahiba hawa wawili watakapokumbatiana na kupongezana na kupokezana urais.

Mishtuko na huku sherehe ndipo umma utakapoona kuwa umechezwa shere kipindi chote.

Tujiandae na matokeo
 
Nakumbuka 1998 kwenye Msiba wa Mzee Mrisho Kikwete, aliyekuwa akinawisha mikono waombolezaji kwenye Msiba walikuwa ni Samuel Sitta na Edward Lowassa na aliekuwa mwenyekiti wa Shughuli za Msiba alikuwa Rostam Abdurasul Aziz. Hawa jamaa wametoka Mbali sana Wizi na Uroho wa Madaraka ndo uliwaunganisha na vitu vivyo hivyo ndo vimewatofautisha

upo sahihi.
 
Nakumbuka 1998 kwenye Msiba wa Mzee Mrisho Kikwete, aliyekuwa akinawisha mikono waombolezaji kwenye Msiba walikuwa ni Samuel Sitta na Edward Lowassa na aliekuwa mwenyekiti wa Shughuli za Msiba alikuwa Rostam Abdurasul Aziz. Hawa jamaa wametoka Mbali sana Wizi na Uroho wa Madaraka ndo uliwaunganisha na vitu vivyo hivyo ndo vimewatofautisha

upo sahihi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom