Lowassa: Urafiki wangu na Kikwete utaendelea mpaka kifo kitakapotutenganisha

Acha kujipendekeza unafikiri ukisema hivyo ndio cc haitalikata jina lako kwa kuwa eti ni rafiki wa jakaya Mkuu hakuna cha urafiki hapa
 
Hatuna tatizo na urafiki wao, inakuwa ni tatizo pale EL anapotaka kuutumia urafiki kama tiketi ya kuingia ikulu, hilo kamwe haliwezekani badala yake sifa/vigezo 13 ndivyo vitatumiwa na CC kupata tano bora.
 
gumegume

...uswahiba wa jinsi hii kuhusishwa na zile kuta takatifu za Magogoni ni janga la kitaifa. haishangazi kuona for the past 10 years nchi hii imekuwa ikienda kwa auto-pilot na mwelekeo wa upepo.
 
Last edited by a moderator:
mkuu,ule usemi unao sema kilichokupandisha ndio hicho hicho kitakushusha

Mkuu tunakubali una mahaba na EL na ni haki yako..

Lakini hayo mameno aliyatoa Lowasa baada ya kusemwa na Rizone..

LOWASA ni mwanasiasa aliyekomaa na hahitaji huruma ya mtu mmoja.

Hakuna mtu wa kukata jina la Lowasa ndani ya wanaCCM halisi kama Kinana ,Kingunge na JK.

Nape na mamluki wengine ndani sio wanachama wa CCM kama sio kuhongwa vyeo walishajitoa na kuunda CCJ.Hawa hawapo pale kujenga chama kama taasisi ndio maana muda wote wanazungumzia majina ya watu.

Waliokipigania chama kwa miaka mingi hawatakuona chama kikiuawa na Nape.Hawatakubali kumwacha Lowasa achukue nchi nje ya CCM eti tu kwa sababu ya chuki za watu wenye uanachama wa mashaka wanaotumika kukiua chama na kuchochea chuki ndani na nje ya chama .
 
haa haa lowasa amesema ukweli. jeuri yote ya lowasa ndani ya ccm inatokana na urafiki wa jk na kikwete. hakuna mwenye ubavu wa kumkemea lowasa ndani ya ccm kamwe. sio nape wala kinana..
Urafiki utabaki kuwa Urafiki na NCHI ITABAKI KUWA NCHI!HAIWEZEKANI NCHI KUKABIDHIWA KWA RAFIKI SABABU NI RAFIKI,HUYU MZEE EL ATENGANISHE URAFIKI NA NCHI,NCHI NI YA WATU MORE THAN 45,000,000 LAKINI URAFIKI NI WA WATU WAWILI!
 
Kwa hiyo JK anakosa sifa za kusimamia vikao vya uteuzi ndani ya CCM kama mwenyekiti kwa vile mmoja wa watangaza nia Bwana Edo ni swahiba wake wa kudumu na kifo tuu ndio kitawatenganisha. Edo sasa anatia mashaka na reasoning yake katika kupanga maneno yakusema na wakati wa kuyasema.
Hapa bila kujua anampa wakati mgumu "rafiki" yake katika kusimamia vikao hivyo mbele ya wajumbe wengine. Edo anasahau kuwa CC, NEC na Mkutano mkuu ni vikao vya kichama sio kiserikali hivyo mwenyekiti anatakiwa aje na nguvu ya hoja sio hoja ya nguvu. Wajumbe wanaweza kutumia nafasi hiyo kukataa kushinikizwa kwa kusema " usimtetee rafiki yako"
 
Nakumbuka 1998 kwenye Msiba wa Mzee Mrisho Kikwete, aliyekuwa akinawisha mikono waombolezaji kwenye Msiba walikuwa ni Samuel Sitta na Edward Lowassa na aliekuwa mwenyekiti wa Shughuli za Msiba alikuwa Rostam Abdurasul Aziz. Hawa jamaa wametoka Mbali sana Wizi na Uroho wa Madaraka ndo uliwaunganisha na vitu vivyo hivyo ndo vimewatofautisha
Kuongezea hapo ulipoishia Samuel sitta huyu huyu ndio mjumbe pekee wa NEC aliemvaa nyerere na kupambana nae vilivyo kwa hoja mkutanoni akimtaka mwalimu awape maelezo ya kina kwanini alishinikiza jina LA lowassa lisiletwe NEC kuja kupigiwa kura,licha ya ukali Wa nyerere alibanwa na sitta vilivyo kwenye eneo hilo.
 
Siasa ina sarakasi za aina yake. Na ni Samuel Sitta huyu huyu akiwa spika wa Bunge la tisa aliyepigilia msumari sakata la Richmond lililomng'oa Lowasa kwenye uwaziri mkuu.
 
Wanabodi saalamu mujarabu kwenu,

Akizungumza jana Bagamoyo alipokwenda kutafuta wadhamini, Lowassa alisema,"Bagamoyo ni nyumbani kwangu kwa pili, kwa sababu ni nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni rafiki yangu.

Nataka niwaambie kuwa mimi na Jakaya ni marafiki wakubwa, na urafiki wetu utaendelea hadi Mwenyezi Mungu atakapotuchukua."

SOURCE: Mtanzania, Jumatatu, 29.6.2015,

MY TAKE: Lowassa hapa anatuma ujumbe kwa Kamati Kuu kwamba, Jakaya ambaye ni rafiki yake mkubwa hivi, hawezi kukubali kuona jina lake linakatwa, NI LAZIMA liingie katika tano bora!

Nawasilisha.
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Kuna shughuli mwaka huu. Lowassa alishasema hakuna wa kukata jina lake ccm, ana wasiwasi gani wakati yupo na apson mwang'onda na mafaili machafu ya kila mtu ndani ya ccm. Mbona kazi mnayo mwaka huu
 
Sasa anazidi kujiharibia, kwa maana hiyo atafanya yale yale aliyofanya rafiki yake!?
 
Anajifaragua tu na kuwadanganya wasiojua. Tunaoujua ukweli, ukweli ni kwamba urafiki wao ulishakufa siku nyingi. Mara ngapi amejaribu kutaka kumwona JK pale ikulu na akakataliwa? Pia maongezi yaliyonaswa ya whatsapp kati ya Ridhiwani na rafiki yake mmoja wakati wa kampeni za Ubunge huko Chalinze maneno mazito aliyokuwa anayaongea Ridhiwani dhidi ya Lowasa ni ushahidi tosha kabisa kuwa familia ya JK na Lowasa ni paka na panya. Lowasa na kundi lake la akina Rostam na Chenge si ndo walianzisha move ya kumtoa Kikwete kwenye uenyekiti wa CCM ili wampe Lowasa nao ni ushahidi tosha kabisa kuwa urafiki wao ulishakufa. Aaache kutudanganya
 
Una ushahidi na haya unayotulisha hapa mkuu
 
wanabodi saalamu mujarabu kwenu

Akizungumza jana Bagamoyo alipokwenda
kutafuta wadhamini, Lowassa alisema,"Bagamoyo
ni nyumbani kwangu kwa pili, kwa sababu ni
nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni
rafiki yangu. Nataka niwaambie kuwa mimi na
Jakaya ni marafiki wakubwa, na urafiki wetu
utaendelea hadi Mwenyezi Mungu
atakapotuchukua."
SOURCE: Mtanzania, Jumatatu, 29.6.2015, Lead
story.
MY TAKE: Lowassa hapa anatuma ujumbe kwa
Kamati Kuu kwamba, Jakaya ambaye ni rafiki
yake mkubwa hivi, hawezi kukubali kuona jina
lake linakatwa, NI LAZIMA liingie katika tano
bora!

nawasilisha.
wote si wanajua kitu kuhusu ile richmond
 
Hizo mbwembwe za kisiasa tu.
Mda utakapofika tutajua tu.
 
Back
Top Bottom