Lowassa; uhuru wanaoutaka Watanzania ni huu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Lowassa; uhuru wanaoutaka Watanzania ni huu

Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima

NILISOMA taarifa kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, licha ya kuchukizwa, amesikitishwa na kutoandikwa makala za kutosha kuhusiana na uhuru wa Tanzania. Lowassa amekwenda hatua nyingi mbele kwa kuwashangaa wachambuzi walioonyesha wazi kutoridhika na uhuru wa Tanzania wenye umri wa miaka 46. Japo ni haki yake kikatiba, hata wapingaji ni haki yao kadhalika.
Lowassa alikaririwa akisema: "Hivi kweli mtu mmoja anaandika katika makala yake kuwa miaka 46 ya Uhuru iliyopita ni bure, je, kweli hakuna kilichofanyika?' alihoji.

"Hali hii imenisikitisha sana kama Uhuru huu usipoelezewa vizuri historia yake na sisi wenyewe nani atauelezea,"` alisema Lowassa.

Kwa Lowassa uhuru wa Tanzania una mengi na ya maana kiasi cha kushangaa ni kwa nini wenzake hawayaoni. Lowassa na wenzake wanaofaidi matunda ya uhuru wana kila sababu na haki ya kushangaa.

Maana mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Kwa mtu wa kada ya Lowassa ambaye amekulia na sasa kuanza kuzeekea serikalini, uhuru wa Tanzania ni wa maana sana. Kwa Lowassa na wenzake ambao wao na watoto wao ndiyo serikali, wana kila sababu ya kushangaa hata kusikitika.

Nani anatarajia mtoto wa kigogo kama Lowassa anayefanya kazi Benki Kuu na watoto wengine lukuki wa vigogo, uhuru wa Tanzania una kila maana na umuhimu. Je, kwa wale wanaotumika badala ya kutumikiwa na uhuru anatarajia nini?

Badala ya Lowassa kulalamikia na kushangaa, inabidi ajiulize ni kwa nini watu wameandika makala zenye mawazo na misimamo tofauti na yake. Walichoandika wachambuzi wengi kuwa uhuru wa Tanzania si chochote si lolote wana sababu tosha na zenye siha.

Kwa mtu anayeshuhudia madudu yaliyofanyika baada ya Mwalimu Nyerere kuachia ngazi, hawezi kuona maana ya uhuru. Maana uhuru haujakidhi matarajio ya wananchi. Utayakidhije iwapo watanzania wengi wanazidi kuwa maskini huku mafisadi wachache wakishirikiana na wawekezaji wameiteketeza na kuitelekeza nchi yetu?

Ni mtu gani, kwa mfano, anayeshuhudia malori ya mchanga uliojaa madini yakikatiza nchi kwenda Tanga bandarini kuusafirisha nje anaweza kuonyesha matunda ya uhuru? Ni ‘mjinga' gani ambaye mtoto wake anazungushwa kila uchao akihangaishwa kupata mkopo wa kusomea anaweza kusema uhuru umefana?

Kwa akina Lowassa waliosoma bure wakatunga sheria za kulipisha elimu iliyosahauliwa, uhuru ni mafanikio yasiyo kifani.

Kwa akina Lowassa ambao serikali yao imekuwa bingwa wa kashfa na ahadi zizotekelezeka bila kuadhibiwa uhuru ni kila kitu. Wapo wenye uhuru wa kufanya watakavyo bila kushughulikiwa. Rejea kashfa kama zile za BoT, Buzwagi, Richmond, IPTL, Deep Green, Takrima, ununuzi wa rada na ndege feki ya rais, utoroshwaji wa mitaji na wafanyabiashara wa kigeni na uchafu mwingine.

Leo sitashangaa Wahindi na Wachina waliotamalaki nchini wakiwa na utajiri mkubwa kwa kusherehekea na kushangilia uhuru ilhali watanzania wazawa wakiendelea kuwa vibarua.

Ni Mtanzania gani anayepandishiwa bei ya maji na umeme huku serikali na wafanyabiashara wezi kama ilivyotokea Tanga Cement wakifaidi vitu hivi bure, atashangilia uhuru? Hebu arejee kiwanda kimoja cha Dar es Salaam cha kusindika mafuta kilichobainika kujiunganishia maji bila kulipa na kisifanywe kitu.

Hivi Lowassa anatarajia Watanzania ‘wanaoganga njaa' wauone uhuru? Uhuru siyo hotuba za watawala. Uhuru ni shibe, uwajibikaji, maendeleo na mabadiliko. Hivi kweli wazanzibari waliopoteza ndugu zao kwenye vipigo vya FFU wakati wa chaguzi za kubambikiwa watawala wanaweza kuuhisi uhuru?

Hivi wanafunzi wanaokalia mawe karne ya 21 wanaweza kuuona uhuru? Je, wajawazito na wagonjwa wanaolazwa kitanda kimoja wanne Mwananyamala, Amana, Temeke na kwingineko nao ni huru? Je wale waliopasuliwa vichwa badala ya miguu na miguu badala ya vichwa nao ni huru?

Je, wachimbaji wadogo wadogo wanaofukuzwa kwenye ardhi ya nchi yao kama wakimbizi nao ni huru? Wakulima wanaotumiwa walanguzi wa mazao yao au kulazimika kuyauza kimagendo au wavuvi wanaokula mapanki nao ni huru? Kama wako huru basi uhuru huu ni kejeli na fedheha. Bila haki uhuru unakuwa sawa na wendawazimu. Bila nidhamu ya matumizi na uwajibikaji wa watumishi wa umma, uhuru ni matusi.

Tumsaidie Lowassa kuelewa wale anaowaona kama wamekejeli uhuru wanachomaanisha. Leo tuna serikali inayotumia pesa yetu vibaya huku ikishindwa wazi wazi kusimamia raslimali zetu. Je, kwa kuendelea na kuwa serikali zigo iliyojaa mafisadi wanaojulikana tunaweza kujisifu tuko huru? Wako wapi waliotuhumiwa kuliibia taifa pesa na kuwekeza kwenye kuchaguliwa?

Japo tunadanganyana kuwa wanachunguzwa na wenzao, ukweli ni kwamba hakuna la maana la kutarajiwa iwapo watuhumiwa wale wale wamo maofisini wakiharibu ushahidi na kuvuta kamba wajuavyo. Kwao uhuru wa kuharibu na kuneemeka ni jambo la maana wakati kwetu ni hatari na hasara.

Miaka 46 tangu tupate uhuru tunazidiwa hata na nchi tulizozikomboa wenyewe. Hebu Lowassa aangalie Angola na Msumbiji atajua ninachomaanisha. Hebu Lowassa atafute sababu ya shilingi yetu kupitwa na sarafu kama ya Kenya, Rwanda hata Burundi atajua ni kwanini kuna watu tusioona mantiki ya uhuru.

Lowassa inabidi aambiwe hata kama atachukia au kutokubaliana kuwa baada ya kung'atuka kwa Mwalimu watanzania walitumiwa na wasaka ngawira wachache walioalikana na hata kurithishana madaraka kwa mbinu chafu kama ilivyokuja kubainika kuwa uongozi nchini umekuwa ukitafutwa kwa rushwa na kuendeshwa kwa kujuana huku umma ukihujumiwa na kusahaulika.

Hivi Lowassa anaweza kueleza ni kwa nini yeye na wenzake wameshikwa na kigugumizi kutaja mali zao? Anaweza kuelezea pesa wanazotoa kwenye kuchangia miradi mbali mbali huku wakiishi maisha ya kifahari walizipataje? Lowassa atusaidie kueleza ni kwanini tofauti kati ya walionacho na wasionacho inazidi kuongezeka kama kweli uhuru wetu tulioaminishwa ungeleta usawa na maendeleo una maana.

Huwezi kuwa na nchi inayoishi kwa kukopa na kutegemea wafadhili kuendesha maisha yake kwa zaidi ya asilimia 40 ukadai uko huru kwa maana sahihi. Nchi inayogawa hovyo hovyo raslimali zake siyo huru. Nchi inayoendeshwa na sera za kukopa na kuamriwa na Washington na London si huru. Nchi isiyo na sera wala falsafa inayoelewaka kiungozi si huru hata kama itajidanganya na kuwadanganya wengine kuwa iko huru.

Uhuru ni wananchi kuendesha nchi yao kwa kanuni na sera zitokanazo na wao. Uhuru ni kuwa na serikali inayowajibika kwa umma na siyo kwa watu wachache.

Huwezi ukawa na umma wa wananchi zaidi ya nusu uishio chini ya dola moja ya Kimarekani ukajidanganya kuwa uhuru umeleta mafanikio au kukidhi yalitorajiwa. Huwezi ukawa na watawala wasiokwenda na wakati ukasema uko huru. Kama huu ni uhuru basi ni udhuru si kingine.

Wanaokula na kusaza, kupora watakavyo bila kushughulikiwa ni huru. Lakini wale wasiokuwamo kwenye genge hili si huru bali mateka wa genge hili.

Nafasi haitoshi.

Nkwazigatsha@yahoo.com
www.mpayukaji.blogspot.com
 
Tanzania naona kumekucha! Hapa ni kumkoma nyani asubuhi na mapema hata kabla ya mchana kweupe!

Good job! endeleeni kusema kweli pengine masikio yatazibuka kam si bongo zao!
 
Good Job Nkuzi(mwandishi)

Hapa JF kumekuwa na mawazo mengi sana ila na sisi tumekuwa wanasiasa kama hao EL na wenzie. Huu ni mwisho wa Mwaka kwa nini JF isiandike walau kakitabu kidogo chenye chapter walau kumi ya topic ambayo zimekuga gumzo kubwa kwa mwaka huu na kukituma sehemu mbali mbali, Bungeni, Sirikali kuu, na kwa wadau ambao walikosa kuzisoma huku JF

Lengo ni kufikisha ujumbe kwa wadau wengi zaidi ikiwa ni pamoja na sirikali lakini tunaweza kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuboresha JF na kupata recognition kubwa zaidi.

Naomba tusiishie kupiga kelele na kubonyeza keybord zetu bali tuweke historia hata vizazi vyetu vitajua tulisema kama tunavyosoma alichokifanya Nyerere et al, wakati wa ukombozi.

Wakati ndio huu tuutumie vilivyo. Mungu ibariki JF
 
Ndiyo!
Sisi wengine huenda tuna makengeza, ndio maana hatuoni matunda ya uhuru, kwa sababu hata nchi yenyewe iliyopata uhuru haipo!
Matunda ya uhuru (kama yapo) ni kwa wachache, ambao wako madarakani tangu enzi hizo za uhuru mpaka muda huu ninapoandika makala hii na hawataki kuachia ngazi! Sasa sisi wengine tufanye nini kama sio kulalamika?
Asitafute mchawi, aangalie alipojikwaa!
 
Nadhani kwa wenzetu (vigogo) waliobahatika kuila kiroho mbaya hiyo keki ya taifa matunda ya uhuru wanayaona, sisi akina yakhe ambao tunaishia kuuwawa na vipindupindu, malaria na maopresheni ya makosa hospitali tulie tu, na hayo matunda ya uhuru tutakuwa tunayaona bararani wakati vigogo wakipita na migari yao ya nguvu.

Nani atasema hayaoni matunda ya uhuru kama wanae kama hawasomi ulaya basi wanafanya kazi sehemu nyeti kama Benki kuu? Nani atasema hajayaona matunda ya uhuru kama hata kupimwa macho tu inabidi aende majuu?

Tuliobaki tuendelee kumlilia Mungu wetu tu.
 
Big up mwandishi,

Word is Lowassa ana tabia ya kuwaita editors na kuwa scold wakimwandika vibaya.I hope hili gazeti halitaogopa hiyo tyranny na kuendelea kuandika ukweli.

Halafu anakwambia "Nafasi haitoshi"
 
NGOJA nim saidie Lowasa...!!! Kweli Kazi ni Nyingi sana...!! Mimi binasfi sifurahii Mtu Akibeza UHURU Kupita kiasi...Kuna vitu vizuri vime fanyika ndani ya miaka 46...

Nafikuri Tuna jiandaa Kufikia Miaka 50..
eeeeh.... Vingozi wa AFRICA!!!... Tanzania Moja...
 
U must be out of your mind.
 
Lowassa; uhuru wanaoutaka Watanzania ni huu

Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima

NILISOMA taarifa kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, licha ya kuchukizwa, amesikitishwa na kutoandikwa makala za kutosha kuhusiana na uhuru wa Tanzania. Lowassa amekwenda hatua nyingi mbele kwa kuwashangaa wachambuzi walioonyesha wazi kutoridhika na uhuru wa Tanzania wenye umri wa miaka 46. Japo ni haki yake kikatiba, hata wapingaji ni haki yao kadhalika.
Lowassa alikaririwa akisema: "Hivi kweli mtu mmoja anaandika katika makala yake kuwa miaka 46 ya Uhuru iliyopita ni bure, je, kweli hakuna kilichofanyika?' alihoji.

"Hali hii imenisikitisha sana kama Uhuru huu usipoelezewa vizuri historia yake na sisi wenyewe nani atauelezea,"` alisema Lowassa.

Kwa Lowassa uhuru wa Tanzania una mengi na ya maana kiasi cha kushangaa ni kwa nini wenzake hawayaoni. Lowassa na wenzake wanaofaidi matunda ya uhuru wana kila sababu na haki ya kushangaa.

Maana mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Kwa mtu wa kada ya Lowassa ambaye amekulia na sasa kuanza kuzeekea serikalini, uhuru wa Tanzania ni wa maana sana. Kwa Lowassa na wenzake ambao wao na watoto wao ndiyo serikali, wana kila sababu ya kushangaa hata kusikitika.

Nani anatarajia mtoto wa kigogo kama Lowassa anayefanya kazi Benki Kuu na watoto wengine lukuki wa vigogo, uhuru wa Tanzania una kila maana na umuhimu. Je, kwa wale wanaotumika badala ya kutumikiwa na uhuru anatarajia nini?

Badala ya Lowassa kulalamikia na kushangaa, inabidi ajiulize ni kwa nini watu wameandika makala zenye mawazo na misimamo tofauti na yake. Walichoandika wachambuzi wengi kuwa uhuru wa Tanzania si chochote si lolote wana sababu tosha na zenye siha.

Kwa mtu anayeshuhudia madudu yaliyofanyika baada ya Mwalimu Nyerere kuachia ngazi, hawezi kuona maana ya uhuru. Maana uhuru haujakidhi matarajio ya wananchi. Utayakidhije iwapo watanzania wengi wanazidi kuwa maskini huku mafisadi wachache wakishirikiana na wawekezaji wameiteketeza na kuitelekeza nchi yetu?

Ni mtu gani, kwa mfano, anayeshuhudia malori ya mchanga uliojaa madini yakikatiza nchi kwenda Tanga bandarini kuusafirisha nje anaweza kuonyesha matunda ya uhuru? Ni ‘mjinga' gani ambaye mtoto wake anazungushwa kila uchao akihangaishwa kupata mkopo wa kusomea anaweza kusema uhuru umefana?

Kwa akina Lowassa waliosoma bure wakatunga sheria za kulipisha elimu iliyosahauliwa, uhuru ni mafanikio yasiyo kifani.

Kwa akina Lowassa ambao serikali yao imekuwa bingwa wa kashfa na ahadi zizotekelezeka bila kuadhibiwa uhuru ni kila kitu. Wapo wenye uhuru wa kufanya watakavyo bila kushughulikiwa. Rejea kashfa kama zile za BoT, Buzwagi, Richmond, IPTL, Deep Green, Takrima, ununuzi wa rada na ndege feki ya rais, utoroshwaji wa mitaji na wafanyabiashara wa kigeni na uchafu mwingine.

Leo sitashangaa Wahindi na Wachina waliotamalaki nchini wakiwa na utajiri mkubwa kwa kusherehekea na kushangilia uhuru ilhali watanzania wazawa wakiendelea kuwa vibarua.

Ni Mtanzania gani anayepandishiwa bei ya maji na umeme huku serikali na wafanyabiashara wezi kama ilivyotokea Tanga Cement wakifaidi vitu hivi bure, atashangilia uhuru? Hebu arejee kiwanda kimoja cha Dar es Salaam cha kusindika mafuta kilichobainika kujiunganishia maji bila kulipa na kisifanywe kitu.

Hivi Lowassa anatarajia Watanzania ‘wanaoganga njaa' wauone uhuru? Uhuru siyo hotuba za watawala. Uhuru ni shibe, uwajibikaji, maendeleo na mabadiliko. Hivi kweli wazanzibari waliopoteza ndugu zao kwenye vipigo vya FFU wakati wa chaguzi za kubambikiwa watawala wanaweza kuuhisi uhuru?

Hivi wanafunzi wanaokalia mawe karne ya 21 wanaweza kuuona uhuru? Je, wajawazito na wagonjwa wanaolazwa kitanda kimoja wanne Mwananyamala, Amana, Temeke na kwingineko nao ni huru? Je wale waliopasuliwa vichwa badala ya miguu na miguu badala ya vichwa nao ni huru?

Je, wachimbaji wadogo wadogo wanaofukuzwa kwenye ardhi ya nchi yao kama wakimbizi nao ni huru? Wakulima wanaotumiwa walanguzi wa mazao yao au kulazimika kuyauza kimagendo au wavuvi wanaokula mapanki nao ni huru? Kama wako huru basi uhuru huu ni kejeli na fedheha. Bila haki uhuru unakuwa sawa na wendawazimu. Bila nidhamu ya matumizi na uwajibikaji wa watumishi wa umma, uhuru ni matusi.

Tumsaidie Lowassa kuelewa wale anaowaona kama wamekejeli uhuru wanachomaanisha. Leo tuna serikali inayotumia pesa yetu vibaya huku ikishindwa wazi wazi kusimamia raslimali zetu. Je, kwa kuendelea na kuwa serikali zigo iliyojaa mafisadi wanaojulikana tunaweza kujisifu tuko huru? Wako wapi waliotuhumiwa kuliibia taifa pesa na kuwekeza kwenye kuchaguliwa?

Japo tunadanganyana kuwa wanachunguzwa na wenzao, ukweli ni kwamba hakuna la maana la kutarajiwa iwapo watuhumiwa wale wale wamo maofisini wakiharibu ushahidi na kuvuta kamba wajuavyo. Kwao uhuru wa kuharibu na kuneemeka ni jambo la maana wakati kwetu ni hatari na hasara.

Miaka 46 tangu tupate uhuru tunazidiwa hata na nchi tulizozikomboa wenyewe. Hebu Lowassa aangalie Angola na Msumbiji atajua ninachomaanisha. Hebu Lowassa atafute sababu ya shilingi yetu kupitwa na sarafu kama ya Kenya, Rwanda hata Burundi atajua ni kwanini kuna watu tusioona mantiki ya uhuru.

Lowassa inabidi aambiwe hata kama atachukia au kutokubaliana kuwa baada ya kung'atuka kwa Mwalimu watanzania walitumiwa na wasaka ngawira wachache walioalikana na hata kurithishana madaraka kwa mbinu chafu kama ilivyokuja kubainika kuwa uongozi nchini umekuwa ukitafutwa kwa rushwa na kuendeshwa kwa kujuana huku umma ukihujumiwa na kusahaulika.

Hivi Lowassa anaweza kueleza ni kwa nini yeye na wenzake wameshikwa na kigugumizi kutaja mali zao? Anaweza kuelezea pesa wanazotoa kwenye kuchangia miradi mbali mbali huku wakiishi maisha ya kifahari walizipataje? Lowassa atusaidie kueleza ni kwanini tofauti kati ya walionacho na wasionacho inazidi kuongezeka kama kweli uhuru wetu tulioaminishwa ungeleta usawa na maendeleo una maana.

Huwezi kuwa na nchi inayoishi kwa kukopa na kutegemea wafadhili kuendesha maisha yake kwa zaidi ya asilimia 40 ukadai uko huru kwa maana sahihi. Nchi inayogawa hovyo hovyo raslimali zake siyo huru. Nchi inayoendeshwa na sera za kukopa na kuamriwa na Washington na London si huru. Nchi isiyo na sera wala falsafa inayoelewaka kiungozi si huru hata kama itajidanganya na kuwadanganya wengine kuwa iko huru.

Uhuru ni wananchi kuendesha nchi yao kwa kanuni na sera zitokanazo na wao. Uhuru ni kuwa na serikali inayowajibika kwa umma na siyo kwa watu wachache.

Huwezi ukawa na umma wa wananchi zaidi ya nusu uishio chini ya dola moja ya Kimarekani ukajidanganya kuwa uhuru umeleta mafanikio au kukidhi yalitorajiwa. Huwezi ukawa na watawala wasiokwenda na wakati ukasema uko huru. Kama huu ni uhuru basi ni udhuru si kingine.

Wanaokula na kusaza, kupora watakavyo bila kushughulikiwa ni huru. Lakini wale wasiokuwamo kwenye genge hili si huru bali mateka wa genge hili.

Nafasi haitoshi.

Nkwazigatsha@yahoo.com
www.mpayukaji.blogspot.com
MPAYUKAJI, kama lilivo jina lako mimi pia ni mmoja wa wanao washangaa watu kama ww ambaao wana uliza maswali ambayo walitakiwa kujiuliza wenyewe.

HIVI umesahau kauli inayo sema KABLA HUJATOA BOLITI KTK JICHO LA MWENZIO TOA BOLITI KTK JICHO LAKO? hivi mpayukaji jina hili lina maanisha uwezo wako na tabia yako?

Uhuru wa Mtanganyika, na Mtaznzania ambaao sisi leo tuna ujadili si uhuru wako wakusadikika umesahau kua nchi hii ilipotoka kua haina sekondari,Vyuo,wasomi kama wewe barabara,leo unadai wanakaa ktk mawe madarasani huoni kua na DARASA tu ni hatua moja wapo,Ifike mahali usitake kunilazimisha kukutafsiri kwa jina lako kua unapayuka kwani kama unapayuka basi i will not even waste my time ila ikiwa unachotaka tuamini kua lowasa amechanganyikiwa kukushangaa ww na wanao beza UHURU basi sina Budi kukushangaa wewe.

Mpayukaji ulichotaka tuamini ni kua UHURU huu amabao watanzania wamesherehekea hauna maana basi inawezekana unapayuka with no reason au una macho hauoni,una masikio hausikii,leo nchii hii unayodai inaishi kwa kukopa,kutupa rasilimali zao haiko huru.

Si kweli kua tunaendeshwa na washington kama unavofikiri hii ni nchi huru yenye maamuzi yake,leo ni huru kiasi kwamba mpayukaji anapayuka anachotaka,hivi kigezo unavotumia si sahihi kutafsir uhuru wetu kwa vieango vyako,si sahihi kudai nchi hii haijapiga hatua yoyote labda husomi historia tulipotoka ukifananisha na tulipo or unless HUONI then unamatatizo ya macho.

Mpayukajiusipende kupayuka,usinifanye niamini kua uyou always payuka.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Mtoto wa Mkulima, i wonder even that name means anything for you but to tell you the truth uhuru wa Tanzania means nothing and i'm sure millions of my fellow Tanzanians would agree. Wewe unaongea kwa kufuata ushabiki wa hiko chama cha kudidimiza maendeleo na kufumbia macho hali halisi. Kwa mtu yoyote mwenye right senses atakubali na kuguswa na mengi kwa kuona jinsi gap ya matajiri na maskini inavyozidi kuongezeka na jinsi kila siku tunavyodidimia kwenye umaskini wa hali ya juu, rushwa na kila aina ya uozo haukuguzi na unaita hiyo geresha ya kujenga shule kwa michango ya kulazimishwa ni maendeleo. Ni kweli tunaongozwa na mataifa ya magharibi. I will advise u to watch documentary za sorious samura na ya hivi karibuni ya living with corruption, my guy u better be serious and for once feel the pain of millions who are denied a chance of that so called uhuru
 
Eti "mtoto wa mkulima" do you even knw what that name means? and you call yourself that. Hivi unajua kuwa mkulima katika "Tanzania yetu huru" ni kuwa mtu wa chini asiye na maendeleo?

Acha ushabiki wako wa chama and kuwa mtu unayependa kuona hali halisi, your convinced kuwa na madarasa ambayo mengi ni kutokana na sisi wenye kipato cha chini kukamuliwa vya kutosha ni kupiga hatua ya kimaendeleo. Its not the same i'm telling you, for them and us gap inazidi kuongezeka and i dont see the point of that so called uhuru, yaani sometimes i wish labda its better to let hao wakoloni watutawale altogher na kutupa barabara nzuri, education system nzuri, hospitali and all that kuliko kuwaacha hawa wakoloni wa kitanzania wanaotung'ata hata bila kupuliza.

Just find the recently documentary ya Sorius Samura ya Living with corruption and you will knw what exactly Uhuru means for them and as for us, I dont anymore
Ni hayo tu.
 
UHURU AGAIN SEPTEMBER 1ST

Nimeamini what goes around comes around!! ngoja tusubiri
 
Back
Top Bottom