Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,836
Lowassa akiwa Mkoani Njombe amerudia kauli ya baba wa taifa"amesema"wananchi wanahitaji mabadiliko,wasipoyapata ndani CCM watayatafuta nje ya CCM".

Chanzo: Itv Habari

My take:Kwa kauli hii ni wazi kabisa CCM wakimkata Lowassa yupo tayari kwenda kuyatafuta hayo mabadiliko nje ya CCM.

Nje ya CCM ni wapi? UKAWA hawawezi kumpokea,Kachafuka sana,UKAWA ni sehemu ya watu safi tu.

Nadhani yale yasemwayo kuhusu ACT-Wazalendo na Lowassa yanaenda kutimia before Oktoba
 
yaani nimekuja jamii forum sa hivi kutafuta hii thread,ni ukweli usiopingika,huyu jamaa kajipanga vilivyo
 
lowasa ametoboa sili na kunukuu kauli ya nyerere ya watz wanataka mabadiliko na yeye ni mmoja wao na asipo yapata ndan ya ccm atayatafuta nje ya ccm.
 
Wakati akiwa Arusha, kutangaza nia, alimkariri Nyerere akisema, watanzania wanataka mabadiliko, na wakiyakosa ndani ya CCM watayapata nje ya CCM. Leo tena kairudia. Ni dhahiri, Lowassa akitemwa CCM, atakimbilia upinzani.
Mkuu hata mimi nimeisikia hiyo kauli nikawa na swali kama hilo kichwani mwangu. Ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yeye ndiye anayeweza kuleta mabadiliko ndani ya CCM. Mwaka huu kazi ipo
 
Mwache ahamie ACT ili wagawane kura na miccm ili UKAWA wapate upenyo.
 
Lowassa akiwa Mkoani njombe amerudia kauli ya baba wa taifa"amesema"wananchi wahitaji mabadiliko,wasipoyapata ndani ccm watayatafuta nje ya ccm"
My take:Kwa kauli hii ni wazi kabisa ccm wakimkata lowassa yupo tayari kwenda kuyatafuta hayo mabadiliko nje ya ccm
Ni wapi?Ukawa hawawezi kumpokea
Yale ya ACT wazalendo na lowassa yanaenda kutimia before octoba
Source:Itv Habari
Hakuna chama cha kushindana na CCM, iwe ni Ukawa au iwe ACT ataishia tu kujifia kisiasa, uchaguzi wa rais utakamilika mwezi ujao Dodoma ambapo tarehe 12/07 rasmi rais wa awamu ya 5 atatangazwa.
 
Wakuu, nmemsikia Mamvi kwenye hotuba yake yakuomba wazamini leo. Hakika huyu mzee hana kitu chochote anachotaka zaid ya Urais.


Iwe kwa nguvu au mateke! Hataki habari yoyote ile zaid ya Urais. Si kufanya nini kwa ajili ya watanzania au namna yoyote ile. Yeye ni Magogoni bhaaas!

Amerejea kauli ya Baba wa Taifa kwamba, "Watanzania wanataka mabadiliko. wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta hata nje ya CCM".

Amesema,yeye ndiye pekee mwenye uwezo wakuleta mabadiliko hayo. Na amesema kwamba, mabadiliko hayo yasipopatikana ndani ya CCM, yuko radhi kuyatafuta hata nje ya CCM!!

Hii si kauli mujjarabu kwa kada na mwanachama wa siku nyingi wa CCM ikizingatiwa kwamba, yeye ni sehemu ya shida au kasoro zilizomo ndani ya serikali ya ccm hadi leo. Tena, ame'play part kubwa kwa UFISADI wake miaka nenda rudi ndani ya Chama.

MY TAKE; Ule uvumi wa Lowasa kuhamia upinzani kuendelea na safari yake ya matumaini unazidi kuwa wazi. Na hapa, duru za kishambenga zinanusa kwamba jamaa anaweza kuhamia ACT maana miezi michache ilopita Z.Kabwe alimkaribisha kwenye chama hicho.

Kumekucha!
 
leo waziri mkuu wa zaman mh,edward lowasa amevunja ukimya na kushangaza wana ccm kwa kusema yeye ni mmoja ya watu wanaotaka mabadiliko asipo yapata ndan ya ccm atayatafuta nje ya ccm.
 
Hakuna chama cha kushindana na CCM, iwe ni Ukawa au iwe ACT ataishia tu kujifia kisiasa, uchaguzi wa rais wa awamu ya tano utakamilika mwezi ujao Dodoma.

Nashinda kwenye majumba ya ibada nikiomba mungu ccm wakate jina la mzee EL ili magogoni ukawa waende kama kumsukuma mlevi
 
Acha ushambenga wewe Lowassa hatoki ccm na atakuwa Raisi kupitia ccm..
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom