Lowassa tunakusubiri utuambie ukweli unaokufa nao moyoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa tunakusubiri utuambie ukweli unaokufa nao moyoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Hunter, Oct 13, 2011.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wanajamvi wenzangu, nimekuwa nikijiuliza sababu na chanzo cha haya yote yanayotokea leo kuhusiana na Dowans, ambayo ni zao la Richmond, na nikajiuliza maswali kadhaa hususani ni ipi nafasi ya serikali kwani toka hili swaga lilipoanza serikali imekuwa kimya na isiyotoa majibu muafaka.
  Tulishuhudia waziri mkuu Lowasa akijiuzulu pamoja na mawaziri wenzake, na toka hapo serikali ya ndugu JK, haijaweza kutoa majibu muafaka ktk yote yaliyotokea mpaka tulipofikia.
  Labda tujiulize
  1. Mnamo tarehe 25June 2008, alipokuwa akitoa mchango wake bungeni Dr. Mwakembe alisema haya '' Kama wapo wasioridhika na maamuzi ya Richmond tutengue kanuni hizo ili tuendeshe mjadala mwingine kusudi watu waseme na sisi (kamati) tuseme yote hata ambayo hatukuyasema kwa heshima ya serikali'' Je hapa Dr. alimaanisha heshima ya serikali ipi, na huyo serikali ni nani? kama walimtaja Lowasa, serikali aliefichiwa mathambi yake ni nani huyo?
  2. Je tunaweza kuacha kumuhusisha JK na Dowans ikiwa alifahamu na hata kumjua aliye jiita mmiliki wa Dowans?

  3. Vipi yule balozi wake aliemwamisha uingereza akampeleka marekani, na wakati huohuo balozi huyo huyo kwa kupitia kampuni yake ya uwakili ya Rex Attorneys akapata dili la kuisimamia Tanesco ktk michakato ya mikataba.
  4. Kama kweli Lowasa ndo muhusika mkuu anapata wapi dhamira ya kutaka kuwa raisi?

  Naamini Lowasa anavumilia sababu hataki kumwanika boss wake wa zamani lakini naamini uvumilivu una mwisho na ipo siku atafunguka.
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nadhani maombi ya kinigeria yakikolea atafungua moyo. Mpe muda, 2015 siyo mbali na tutasikia mengi.
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  UMIBISA KILELWE MANYUNKO GALA MUBISURA
  Yeye aendelee kuficha kama ana ukweli anahojua kwa kuwa mwisho wa yote jamii itamuhukumu hata kama alificha kumfurahisha mtu kwa kuwa kuwekwa wazi kwa taarifa hiyo kunaisaidia jamii kutoa maamuzi sahihi na kwa mtu sahihi.Jamii inaangalia nyakati na sio bora taarifa.
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kila mtu kafunga moyo wake..Lowassa, Mwakyembe, Sitta, Msabaha kila mtu anamuogopa Rais ndiyo maana tunataka katiba mpya huu urais wa kimungu mungu ni upuuzi mtupu..Lowassa aliwajibika na huyu JK angeanikwa tu ndiyo maana anafanya mbinu amrithishe mtu wake kiti ili asipate matatizo, anawagombanisha akina Sitta na Lowassa ili wamsahau na ajiongezee nguvu kwao.
   
 5. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  kweli urahis wa bongo ni robo ya umungu wa tanzania
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tangu Lowassa akataliwe na Mwalimu mwaka 1995 tumelichukulia swala lake kiushabiki sana. Mimi binafsi kipindi chote hicho nasubiri mtu yeyote aje atuambie huo utajiri wa "kupindukia" wa Lowassa uko wapi? Mbona tunaishia kuambiwa "huyu jamaa ni balaa ana hela kuliko serikali" lakini hizo hela wala mali anazomiliki hatuambiwi na mwisho wake tunafikia kudhani huenda huyu jamaa ana fedha nyingi hata kuliko wakina Bakhressa ambao wana biashara kubwa zinazojulikana.

  Lowassa anamiliki nini hasa hadi cha kumfanya aonekane ni mwanasiasa mwenye ukwasi wa kupindukia. Wenye kujua mali anazomiliki Lowassa ebu tuambieni maana humu Jamvini wakati mwingine inaonekana hela alizonazo Lowassa ndizo zinawanunua wanasiasa wote wa Bongo pamoja na wapiga kura wao.
   
 7. t

  tito majala Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jk ni ndumilakuwili anauma na kupuliza ndo maana anashindwa kuwaambia EL na EC wajiuzulu moja kwa moja kwani naye ni muhusika katika dili la kuanzia richmond hadi dowans na kama gamba kuu wa kujivua ni yeye ila akina EL wanaogopa kumvisha paka kengele lakini ukifika wakati watafunguka na kusema tusubiri tuone"time will tell"
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hatutaki uturudishe nyuma na kwa nini umesubiri hadi aliyemtuhumu amefariki? Kwa nini mwenyewe amekaa kimya asieleze nini anacho na nini hana? Kama huna cha kujadili ni bora ukatulia maana suala la utajiri wake sasa siyo la kubishaniwa.
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu hata mimi nashangaa hivi kuna biashara gani pale IKULU? mwalimu amekaa pale miaka 25 lakini hakutoka na hata na ndururu, akastaafu akaenda zake Butiama Kulima tena kwa jembe la mkono, lakinisasa hivi mtu anakaa pale miaka 5 tu, ukimwekea tathmini utakimbia kama kichaa.

  Ngoja na mimi nikausomee u ikulu ili niingie nikaprove -- ha ha ha
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Muasisi wa kujivua gamba ni Rais mwenyewe na kama angekuwa hataki kuanikwa basi asingeiasisi maana ingekuwa ni suicide mission. Ukweli ni kwamba kuna watu wanataka kulikwepa hili kwa kumhusisha Rais lakini watanzania siyo mabwege. Wanajua kila kitu kuhusu uchafu na na usafi wa viongozi wao na kwa hili wameshapitisha hukumu. Tatizo la hawa watu ni kudhani kwamba hawastahili kuumbuliwa na ikitokea hivyo ndo unaona sasa watu wanavyotishiwa kuondolewa duniani. Anyway nisiseme sana maana wenzetu wako Apollo tayari.
   
 11. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwanae amenunua nyumba ya bilioni moja katikati ya jiji la london(sio kariakoo dsm)
  Sasa na wewe wataka kutuambia nini?
   
 12. Makenya

  Makenya Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mm binafsi nimeanza kujua chanzo cha richmond n nn! Time will tell
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mzee mbona unaongea kama unawakilisha kundi fulani hivi. Hamtaki wewe na nani na kwa nini hamtaki niwarudishe nyuma?

  JF imeanza 2006 Mwalimu Kafariki 1999 tofauti ya miaka saba. Sasa wewe utajuaje kwamba kabla ya kuanzishwa kwa JF nilishawahi kuuliza swali hili mahali kwingine?

  Hata mahakamani anayethibitisha Kosa si yule aliyeshitakiwa bali aliyeshitaki. Watu wanaosema Lowassa ana utajiri wa kupindukia ndiyo wenye wajibu wa kutuambia utajiri wake uko kwenye kitu gani au kama wanaweza watuonyeshe makampuni anayomiliki hisa zake na hisa hizo ni za kiasi gani cha fedha. watutajie ana nyumba ngapi, magari, mashamba, mifugo na vitu vingine wanavyovifahamu

  Mimi najadili mada iliopo mbele yetu. Na kanuni yangu ni ile ya Mao. " No Research No right to speak!!" Leta data acha kulalama
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sasa nime elewa kwa nini Mwanaidi ni Balozi .Maana miaka kadhaa ulizuka ubishi hapa .Taratiiiiiiiiiiibu picha ina anza kuja .Hongereni CCM na JK wenu .Poleni sana Watanzania na Tanzania yetu .
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakati bado, mimi na kwambia tukikaribia 2015!! Utaona!! Usanii ule ule uliowamwaga wenzao 2005 ndo utaaamua 2015!!
   
 16. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  LOWASA hawezi kuwa Rais hata iweje,labda mbingu ipinduke wote tugeuke wendawazimu ndo tumchague MVI nyeupe fisadi,kudhihirisha kauli hii hata Wamasai tumemuondoa kwenye cheo cha UZEE maarufu wa kimasai yaani LEGWANAANI!
  imekula kwake time has gone,
  tunasubili KATIBA MPYA ili tutaifishe MALI zetu toka kwa mafisadi tena tunaanza na huyo fisadi mnaemtetea LOWA-USAHA.
   
 17. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hilo la Mwanaidi mzee umenichanganya kidogo. Mwanaidi anahusiana nini na hii thread?
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Haya ni matumizi mabaya na yasiyostahili ya hicho unachoita kanuni ya Mao. Hoja kama hii imejadiliwa tena siyo mara moja na kama wewe ungekuwa mfuatiliaji usingeibuka sasa na kuufufua mjadala ukiwa huna hoja mpya. Ni kweli mimi nawakilisha kundi la watanzania wanyonge ambao wanakwazwa na hili lakini hawana namna ya kushiriki mjadala huu.

  Wewe unayedai kwamba "conviction" ya Lowassa siyo sahihi ndo uende mahakamani ukaombe clearance. narudia tena, yeye mwenyewe Lowassa hajasema kitu kwa sababu ukwasi wake anaujua na kuujadili kutamuweka pagumu maana hawezi kujustify hata robo yake.
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii kali!
   
 20. A

  Ame JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Ole ni kwao wawaaminiawo wanadamu na moyoni mwao wamemwacha Mungu....Alivumilia kwa nia ya kumcover ili iweje? Kusudio lake lilikuwa kwa upendo wa huyo aliyemcover ama imani yake kuwa kwakufanya hivyo baadaye naye atamsaidia kufikia malengo yake? Someni Isa:30 na 31 chapter nzima ndo mtaelewa nini maana ya Mungu kukukataa kwakumfanya Pharao/ukuu wa dunia/mwandamu kuwa kinga yako na moyoni umemwacha Mungu. Utajiri na heshima vyote vya toka kwa Mungu naye kwa mapenzi yake humpa huyu na kumnyima yule.

  Tukumbuke kwamba hata dhambi asipoiruhusu Mungu ikuangamize haiwezi kwasababu tu Mungu nimwenye haki basi shetani anapata leagal authority ya kumwangamiza mtu kwakutumia dhambi. So hata wale ambao kwa kutumia njia za shetani wamepata mafanikio makubwa wakumbuke kuwa hata hilo ni Mungu ameliruhusu kwa kusudi lake mwenyewe...So naasijisifu binadamu yeyote yule kwamba ni kwa ujanja amepata heshima/utajiri yote hayo in a minute vyaweza toweka kama havijatokana na haki ya Mungu. Tena inaleta generation curse...

  So kwaujumla kama huyu bwana ameamua kurudi kwa Muumba wake kwa toba ni bora akamsikiliza yeye 100% akiwa vugu vugu Mungu atamtapika. So far sauti ya wengi ni sauti ya Mungu miyo ya watanzania inauchungu sana na yeye akubali kulipa garama ya njia zake mbaya kwakurudi na kutulia i.e Isa 30:15-17 ili kwa majira na wakati Mungu apate ku mwinua....Asema nabii wa Tanzania!
   
Loading...