Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 296
Ufisadi mkubwa tena: Dawa hizi ni hatari kwa Binadamu
-----------------------------------------------------------------
Hiki ni kipindi pekee cha vugu vugu la kuhanika ufisadi. Hivi mtumishi wa serikali anapoagiza nje na kuuza dawa kwa wananchi za kuhatarisha maisha ya wanawake wakati wa kujifungua , eti kwa kuwa kapewa dau kubwa toka kwa Mhindi(mtengenezaji), huo ni ufisadi au ufirauni?
Mambo haya yanafanyika Medical Stores Department (MSD). Krugenzi ya ununuzi imekuwa inafanya mambo yasiyo ya kibinadamu kwa Watazania, kwa kuingia mikataba yenye maslahi yao tu, na hivyo kupelekea upungufu mkubwa wa dawa katika Zahanati na vituo vya afya. Ni asilimia 60% tu upatikana kwa wananchi na si kwa wakati muafaka.
Mkurugenzi Mkuu ambaye alipatiwa kazi hiyo akitokea Marekani ambako aliishi kwa miaka mingi, hana ufahamu mzuri juu ya shughuli zote za MSD, na hivyo anapodanganywa chochote hawezi kujinasua. Amekubali ushauri mwingi potofu, na hivo manunuzi mengi yanafanywa kwa matakwa ya mkurugenzi wa ununuzi na maofisa wake! Director General(DG) wa MSD ambaye ni mototo wa aliyekuwa IGP, Phillemon Mgaya alibebwa sana na fisadi wa kimataifa Mh. Edward Lowasa( Lowasa ni rafiki wa karibu wa Phillemon Mgaya) ili kuogezewa mkataba wa miaka miwili tangia Januari 2008.
Manuanuzi ya ajabu yaliyofanyika:
NB: Hii posting imetoka kwa pntimba ambaye bado ni jr member. Ilikuwa misplaced.

- Maji ya uchungu(Oxytocin Injection) ambayo ni dawa ya kuongeza uchungu kwa kinamama wakati wa kujifungua, ilinunuliwa kwa wingi na ki maajabu toka India kwa Vital Healthcare(mojawapo ya batch ni V7137). Zilinunuliwa container 3. Dawa hii hivi sasa ni sumu, maana zimetunzwa kwenye joto la kawaida la 30oC badala ya 2-8oC, hii ni kutokana na kwamba MSD ina uwezo wa kutunza vitu katika ubaridi si zaidi ya robo container. Hata hivyo wafisadi wa krugenzi ya ununuzi walimshauri Vital healthcare afute (kwa mark pen) kwenye kasha la nje, maagizo juu ya utunzaji katika ubaridi. Dawa hizi sasa hivi zinauzwa kwa vituo vyote vya serikali, zinatunzwa katika joto la Dar, ila chupa za ndani zinaonyesha mahitaji kamili ya joto la 2-8oC. Ubadhilifu huu ulimwingizia mkurugenzi wa ununuzi dolla za marekani 27,000.
- Mwishoni mwa Mwaka jana zilinunuliwa container 150 za futi 40 za maji ya kuwawekea wagonjwa mwilini. Ujazo huu unazidi uwezo wa MSD kutunza mizigo hii kwa asilimia 100, na unazidi mahitaji ya nchi kwa miaka mine.Maji haya yalikaa juani kwenye ma container kwa miezi kadhaa baada ya bohari zote kujaa sana na mengine yalilazimishwa kwenda kanda zote za MSD bila mafanikio.Inakisiwa maji haya yataisha mwaka 2010, ingawaje muda wake wa kuisha matumizi ni 2009. Fununu zilizopo ni kwamba ufirauni huu ulifanywa baada ya kampuni inayotengeneza maji hayo kutoa dau la dolla za marekani 120,000 kwa mkurugenzi na ofisa wa ununuzi. Mwenyekiti wa MSD tender bodi ambayye si mtaaluma kabisa wa madawa au manunuzi yalimpita pembeni.
- Madawa ya kupunguza makali ya virus ya ukimwi(ARVs imekuwa chanagmoto mpya kwa DG na MSD. Mpaka leo hii DG ajui kwamba kukosekana kwa dawa hizi ni kazi ya ufirauni wa krugenzi ya ununuzi . Dawa hizi zimepungua sana tangia November 2007, hadi leo hii, Global Fund na PEPFAR wanajua fika kinachotokea MSD , ila DG haelewi kuwa anaingizwa mtatani. Tender na mikataba vinatolewa kwa watu waliokwisha jijenga kwa Krugenzi ya Ununuzi. Mikataba ikishatolewa na maofisa uchukua chao, na kwaida mtu akisha kupa ongo ataleta dawa kwa wakati anapotaka na quality anayotaka. Sababu hiyo imesababisha dawa kutokuja kwa wakati. Imefikia wakati wanapigwa vita vikali sana watengenezaji wa dawu hizi wa hapa nchi wasiuze dawa zao katika soko la nchi hii. Mfano mzuri ni Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical industries (TPI) ambacho licha ya kupewa changamoto na serikali kuanza kuzalisha dawa hizi hapa nchini ili kuuwanusuru wananchi, kimekuwa kikiwekewa vikwazzo vingi sana na krugenzi ya ununzi.
NB: Hii posting imetoka kwa pntimba ambaye bado ni jr member. Ilikuwa misplaced.