Lowassa siyo mrahisi kama RA; ni Mtu wa visasi zaidi

Watanzania wengi wanasubiri nani atafuatia baada ya RA kujiuzulu wakimsubiri kwa hamu kubwa Edward Lowassa kuliko hata Andrew Chenge maana hawa mapacha watatu wamepamba sana vyombo vya habari siku za hivi karibuni.

Lowassa siyo mtu mrahisi kwa kiwango ambacho watu wengi wanamdhania na ni kosa kubwa sana kumweka kwenye kundi la wakata tamaa kama Rostam Aziz anajua amejipangaje na lazima atimize kusudi lake.

Kusema kwamba Lowassa ni kiongozi mzuri na mchapa kazi mwenye kuweza kufanya maamuzi magumu ni ukweli mdogo sana kulingana alivyo ki halisi na tabia zake binafsi.

1. Ni mtu mjanja sana na anayejua kutumia karata zake vizuri kwa wakati unaofaa huku akisoma alama za nyakati na kuhakikisha kuwa anawajua adui zake wa ndani na nje.

2. Huwa hawezi kurudi nyuma akishamchukia mtu atahakikisha amelipa kisasi na hasira zake zimekwisha na hana muda wa kuelewana naye atamtafuta mtu mwingine atayejenga naye urafiki na ili kummaliza yule wa awali.

3. Ni mtu ambaye hujiwekea usalama wa awali kwa kuwapandikiza watu wa kumfanyia kazi na kumletea majungu juu ya wabaya wake sehemu zote nyeti hasa za serikali na sehemu zote zenye nafasi za ulaji na hapishi hata deal ya 2ml.

4. Pia ni mnafiki na mjanja ambaye anajua kutumia watu wanaojijua na wasio jijua kwa masilahi yake binafsi na hata kuingiza mamluki kwa viongozi wa dini kulingana sadaka zake haramu wa wachunga kondoo wa Bwana.

5. Ni mtu ambaye anapenda kuabudiwa kama Mungu mtu na anapenda aogopwe na wale wanomzunguka waitikie na kukubali kila anachotaka
na ukipingana naye yatakupata makubwa na na utatupwa nje ya madaraka haraka sana kwa kuwatumia mamluki na vibaraka wake aliowapandikiza kila mahali.

Kwa wanaomjua vizuri Ole Moloimet aliwauliza baadhi ya (Leigwanani) wazee wa kimasai wa Monduli kuwa hivi mbuzi akikaa kwenye zizi la ng'ombe miaka 20 anaweza kubadilika na kuwa ng'ombe? (akimaanisha Lowassa ni mmeru na siyo mmasai na hana tabia za kimasai) Wakamjibu hapana habari zikamfikia Mungumtu Lowassa na ndiyo ulikuwa mwisho wa Ole Moloimet mpaka leo.

Ole Sendeka anatamaniwa sana ila hajapatiwa mahali pazuri subiri apate madaraka kama utamsikia mtu anayeitwa Ole sendeka tena.

Kwa kifupi huyu jamaa ana mambo mengi sana ambayo hapa tukiyaeleza kila moja na visa vyake tutachukua muda mrefu sana na hatuwezi kumaliza kulingana na jinsi alivyoenea kila mahali kama soda ya coca cola ni kirusi hatari sana kwa wananchi walio masikini na wenye vipato vya kati na HAFAI KUWA RAIS WA JMT kuna watu kibao kutoka upinzani na hata chama tawala ambao ni wazalendo na wana uwezo wa kuwa Rais yeye siyo malaika wa kumpamba na kusema kuwa anaweza kufanya maamuzi.

Hi tamaa kubwa namna hii ya na uchu wa uraisi inatoka wapi? Mpaka alifikia hatua ya kuwaapia marafiki zake kile kiti yaani urais lazima apate iwe KWA DAMU AU SANDUKU LA KURA Huyu mtu bado watu wanasema kuwa anafaa kuwa rais na anaweza kufanya maamuzi magumu!?

Narudia tena kujiuzulu kwa Lowassa ni ndoto na hata kama akifanya hivyo atarudi kwa mlango mwingine au atakuwa anaendesha nchi kwa remote control kitu ambaco siyo sawa

Kwa hili hata mm nilishawahi kusikia kuwa jamaa (EL) siyo Mmasai ni mtoto wa kufikia kwenye familia ya marehemu mzee Lowasa Senior.
 
Edo Lowassa kuwa rais wa JMT ni ndoto...hatokuwa rais hata akisema atumie nguvu za ajabu...za giza wala za kimungu (ambazo hatozipata) hawezi kuwa rais wa nchi hii asilani
 
Tatizo waliomzunguka wapewa upofu na hawajui kwamba wanapigana vita ambavyo hawatashinda! Wako busy kutukana watu hata waliowasaidia suti za harusi zao!
 
Back
Top Bottom