Lowassa siyo mrahisi kama RA; ni Mtu wa visasi zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa siyo mrahisi kama RA; ni Mtu wa visasi zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Derimto, Jul 14, 2011.

 1. D

  Derimto JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania wengi wanasubiri nani atafuatia baada ya RA kujiuzulu wakimsubiri kwa hamu kubwa Edward Lowassa kuliko hata Andrew Chenge maana hawa mapacha watatu wamepamba sana vyombo vya habari siku za hivi karibuni.

  Lowassa siyo mtu mrahisi kwa kiwango ambacho watu wengi wanamdhania na ni kosa kubwa sana kumweka kwenye kundi la wakata tamaa kama Rostam Aziz anajua amejipangaje na lazima atimize kusudi lake.

  Kusema kwamba Lowassa ni kiongozi mzuri na mchapa kazi mwenye kuweza kufanya maamuzi magumu ni ukweli mdogo sana kulingana alivyo ki halisi na tabia zake binafsi.

  1. Ni mtu mjanja sana na anayejua kutumia karata zake vizuri kwa wakati unaofaa huku akisoma alama za nyakati na kuhakikisha kuwa anawajua adui zake wa ndani na nje.

  2. Huwa hawezi kurudi nyuma akishamchukia mtu atahakikisha amelipa kisasi na hasira zake zimekwisha na hana muda wa kuelewana naye atamtafuta mtu mwingine atayejenga naye urafiki na ili kummaliza yule wa awali.

  3. Ni mtu ambaye hujiwekea usalama wa awali kwa kuwapandikiza watu wa kumfanyia kazi na kumletea majungu juu ya wabaya wake sehemu zote nyeti hasa za serikali na sehemu zote zenye nafasi za ulaji na hapishi hata deal ya 2ml.

  4. Pia ni mnafiki na mjanja ambaye anajua kutumia watu wanaojijua na wasio jijua kwa masilahi yake binafsi na hata kuingiza mamluki kwa viongozi wa dini kulingana sadaka zake haramu wa wachunga kondoo wa Bwana.

  5. Ni mtu ambaye anapenda kuabudiwa kama Mungu mtu na anapenda aogopwe na wale wanomzunguka waitikie na kukubali kila anachotaka
  na ukipingana naye yatakupata makubwa na na utatupwa nje ya madaraka haraka sana kwa kuwatumia mamluki na vibaraka wake aliowapandikiza kila mahali.

  Kwa wanaomjua vizuri Ole Moloimet aliwauliza baadhi ya (Leigwanani) wazee wa kimasai wa Monduli kuwa hivi mbuzi akikaa kwenye zizi la ng'ombe miaka 20 anaweza kubadilika na kuwa ng'ombe? (akimaanisha Lowassa ni mmeru na siyo mmasai na hana tabia za kimasai) Wakamjibu hapana habari zikamfikia Mungumtu Lowassa na ndiyo ulikuwa mwisho wa Ole Moloimet mpaka leo.

  Ole Sendeka anatamaniwa sana ila hajapatiwa mahali pazuri subiri apate madaraka kama utamsikia mtu anayeitwa Ole sendeka tena.

  Kwa kifupi huyu jamaa ana mambo mengi sana ambayo hapa tukiyaeleza kila moja na visa vyake tutachukua muda mrefu sana na hatuwezi kumaliza kulingana na jinsi alivyoenea kila mahali kama soda ya coca cola ni kirusi hatari sana kwa wananchi walio masikini na wenye vipato vya kati na HAFAI KUWA RAIS WA JMT kuna watu kibao kutoka upinzani na hata chama tawala ambao ni wazalendo na wana uwezo wa kuwa Rais yeye siyo malaika wa kumpamba na kusema kuwa anaweza kufanya maamuzi.

  Hi tamaa kubwa namna hii ya na uchu wa uraisi inatoka wapi? Mpaka alifikia hatua ya kuwaapia marafiki zake kile kiti yaani urais lazima apate iwe KWA DAMU AU SANDUKU LA KURA Huyu mtu bado watu wanasema kuwa anafaa kuwa rais na anaweza kufanya maamuzi magumu!?

  Narudia tena kujiuzulu kwa Lowassa ni ndoto na hata kama akifanya hivyo atarudi kwa mlango mwingine au atakuwa anaendesha nchi kwa remote control kitu ambaco siyo sawa
   
 2. I

  Imnyagi Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wa haraka kwa watu wasio mjua kwa undani wanona ndiye kiongozi anayewafaa watanzania lakini nadhani kumchagua huyu ndugu ni kuleta janga lingine kubwa.
   
 3. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe Ulijulia wapi na Tangu Lini?
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili wenye akili wanalijua, jamaa hata hakusatahili kufikia level ya uwaziri mkuu leave alone ubunge. No doubt kuwa he is smart guy who knows to use those around him.

  Lakini tusije kudhani kuwa Rostam naye ni mjinga, hawezi kukubali kuwa bangusilo, nasubiri karata zake. Nina uhakika akicheza karata mbili tu vumbi litatimka na watu watajuta.

  Kama aliweza kuiweka nchi mkononi haiwezekani aamue kuiacha tu hivi hivi, atakuwa amepata njia mbadala.
   
 5. k

  kipanga mlakuku Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Joto la uchaguzi ndani ya CCM linazidi kupanda kabla ya uchaguzi huo mwakani 2012 na tayari vyanzo vyangu vya habari za upekuzi zinafunua juu ya viapo vya Edward Lowassa kuwa amejiapiza atahakikisha kuwa ni wanamtandao wake wanaibuka kidedea kwenye kila ngazi ya uongozi ndani ya CCM.
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,742
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hii tuichukulie kama tetesi tu.
   
 7. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Freedom ov Express
   
 8. W

  Welu JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 786
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Muda wa Lowasa ulishapita atambue hivyo. Kwani muda wote ameongoza kabla wengine hawajazaliwa. Ina maana kitu hakufanya makusudi ndio anataka afanye sasa. Nchi hii ina watu wengi sana nao acha waongoze. Wewe ulishaboronga inatosha.
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 82,452
  Likes Received: 47,196
  Trophy Points: 280
  Noibody cares about ccm anymore..................is it not a party of thieves?

  Ukiwa kinara wa wezi hivi unalo la kujivunia?

  "Whose end is destruction. Whose God is their belly. Whose glory is in their shame. Who set their wicked minds on earthly things." Philippians 3:19
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,014
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  Gamba kuu lililoshindikana kuvuka.
   
 11. h

  hsagachuma Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani muda wa EL kisiasa umekwisha atafute shughuli nyingine. Fedha anazo aende kupumzika Monduli kama waziri mkuu mstaafu.
   
 12. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na sie CUF tutamsimamisha Mtatiro kwenye uchaguzi wa 2015 kama chama chetu bado kitakuwa hai kwa kudra za Muumba.
   
 13. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 680
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  CCM ni mizengwe tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu,nawashangaa sana wanaokisapoti hiki chama. Acha wavurugane hadi kieleweke wakati CDM kinapaa anga ya kukubalika hapa Tz.

  Kama hujui wanaCCM wanamkakati wa kuzunguka nchi nzima kuhakikisha kuwa wanatangaza na kujipongeza kwa ushindi waliopata Igunga. JE pesa zote hizo za kujitangaza siwangewapelekea wanaigunga walau maji kwa kuchimba visima vidogovidogo?. Pia haiingi akilini viongozi wake kuitisha mikutano katikati ya barabara na kufunga barabara eti mikakati ya kujipongeza kwa ushindi wa kifisadi wa Igunga. Kule Mshi huwezi amini ujinga kama huu ulitokea na watu kusumbuka ktk shughuli mbalimbali kutokana na mkutano wao wa kupongeza ushindi wa kifisadi huko Igunga.

  Cha kusikitisha zaidi makada wengi walionekana ni watu wasiokua na uwezo wa kuchambua mambo. Huwezi kuwa kwenye jimbo tofauti na Igunga afu unasema" Igunga huye' kwa wakazi tofauti na Igunga nawe unaitika hoyeeeeeeeeeeee'. Huu ni umaskini wa kufikiri na akili, wengi wa mawshabiki waCCM WAMEPUMBAZWA kisiasa.
   
 14. Panizo

  Panizo Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Magamba imekula kwenu
   
 15. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyewe anadai his past is over, na kwa vile ccm wanatumia masaburi lolote laweza kutokea, tusibiri tuone
   
 16. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nape atalia mbaya! bora iwe uongo cz namuonea huruma..
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwacheni mzee Lowassa apumzike alijiuzulu uwaziri mkuu tetesi hii haimtendei haki. Uamuzi wa kuachia madaraka ni mzito kwa upande wa serikali ndivyo hivyo tunategemea atachukua uamuzi mzito kwenye chama chake kwa kutokuwa nyuma ya kundi lolote ndani ya chama
   
 18. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  sawazisha hapo kidogo sio mstaafu ni Waziri mkuu jiuzulu
   
 19. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  atafichwa mafia na kunyongwa jumla. Teh teh teh
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Aendelee tu kuota ndoto za mchana kwani Lowassa anasahau watanzania wana hasira naye kiama na akiamua kugombea urais akipata kura hata 10% ashukuru mungu. Mie naomba CCM wamchague awe mgombea urais tumsubiri mtaani kumuangusha anguko kuu once a fisadi always a fisadi there is no redemption. Mchagueni CCM anawafaa 2012 sijui 2015 tunamsubiri.
   
Loading...