Lowassa: Siwezi mhukumu Kikwete, yeye mwenyewe ajihukumu. Magufuli anafanya vizuri baadhi ya maeneo

kidaganda

JF-Expert Member
Aug 26, 2013
2,991
2,564
Kipindi kimeanza...

Lowassa: Rais Magufuli anafanya vizuri ila ningekuwa mimi nisingefanya hivyo, ningefanya zaidi, kama nilivyosema kipaumbele ni ELIMU, ELIMU, ELIMU, nisingeanza na madawati, ningeanza na maslahi ya walimu. Serikali ishughulike na mambo makubwa, mambo ya madawati ni ya makatibu kata.

Lowassa: Siwezi muhukumu Kikwete, yeye mwenyewe ajihukumu, na sijamuona hivi karibuni, ila sina tatizo naye.

Lowassa: Rais Magufuli ashughulikie suala la Zanzibar. Wakae chini na kuongea kama alivyofanya Amani Karume na kuleta maridhiano.



===========
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Edward Lowassa leo amehojiwa ndani ya Azam tv na kutoa maoni mbalimbali juu ya mwenendo wa serikali ya Rais Magufuli kama ifuatavyo:

Kuhusu swala la kipaumbele cha madawati kwa kila shule amesema kuwa hilo ni jambo dogo sana kufanywa na serikali kuu. Hiyo ni kazi ya makatibu Kata na watendaji wa serikali za mitaa. Yeye angejikita kuboresha maslahi ya waalimu na madarasa yawe ya kisasa zaidi. Amesifu pia shule za kata alizoanzisha na zinatoa matunda mazuri.

Kuhusu swala la wabunge wa upinzani kugomea bunge amesema kuwa walikuwa sahihi kutokana na mfumo wa madaraka uliowekwa ndani ya bunge. Aidha amesema hayo yalifikiwa kutokana na spika Ndugai kukosekana kwani ana imani naye kuwa ni mtendaji mahiri na mwenye kurdhia mazungumzo. Amesema kuwa Tulia hakustahili kuongoza bunge kutokana na uzoefu wake.

Kuhusu swala la ma DED na DAS amesema kuwa rais Magufuli amekosea uteuzi kwani ameteua makada wa CCM waziwazi bila hata kufanyiwa vetting. Amesema kuwa DAS ndiyo wasimamizi wa uchaguzi wilayani hivyo kuteua makada waziwazi siyo sahihi na ni kuminya haki.

Kuhusu swala la katiba mpya amesema kuwa mambo matano muhimu yafanyiwe mardhiano kwani ni ya kitaifa bila kujali vyama. Amesema kuwa endapo kutakuwa na uvyama basi CCM ndiyo itakuwa mshindi kutokana na mfumo uliopo.

Kuhusu swala la Zanzibar amesema kuwa taifa limegharamika kutokana na kunyimwa misaada mfano fedha za MCC ambazo amesema kuwa zina msaada mkubwa kwa taifa hasa kule vijijini. Amesema kuwa kwa swala la Zanzibar hakubaliani na ubabe ubabe unaoendelea kwani wananchi wanaumizwa.

Kuhusu swala la serikali kuhamia Dodoma amesema kuwa kila kiongozi alikuwa na dhamira hiyo ingawa waliangalia kwanza vipaumbele vya taifa kwa wakati huo. Amesema kuwa serikali ya Magufuli wasiende Dodoma mbiombio kwani watavunjika miguu huku akisema kuwa fedha za miradi ndizo sasa zinatumika kama dharura ya kuhamia Dodoma jambo ambalo siyo sahihi.

Amesema kuwa kama taifa tunahitaji zaidi kuzungumza na kuridhiana kuliko ubabeubabe hapa akigusia serikali ya rais Magufuli.Mfano ikiwa rais anaenda Kahama kushukuru wapiga kura kwanini yeye asiende Iringa na Mbeya? Nini tatizo? Huku akisema kuwa kufanya siasa ni haki ya kikatiba ya kila mtu. Rais Magufuli anavunja katiba.

Aidha amesema kuwa jambo la ajira bado halifanyiwi kazi huku akiponda serikali ya rais Magufuli kuajiri kwa kuangalia vyeti bila kufanya vetting kiasi cha kuwapata watendaji wasio na weledi wala uzalendo.
 
Kipindi kimeanza
Lowassa ni mwanasiasa makini sana. Lowassa ni mwanasiasa mkomavu sana. Lowassa ni mwanasiasa anayejitambua sana. Lowassa ni mwanasiasa ambaye hana kinyongo kabisa moyoni mwake.

MOYO/ROHO YA LOWASSA NI NYEUPE KAMA THELUJI. NI NYEUPE KAMA NYWELE ZAKE.

Lowassa hana kinyongo. Tazama jinsi alivyojibu swali kuhusu "Urafiki wake na Kikwete"

Tazama jinsi asivyotaka kuongelea maisha ya wanasiasa wengine waliokuwa wakimpinga kama Membe, Prof Lipumba na Dr Slaa.

Lowassa ni mwanasiasa
 
Back
Top Bottom