Lowassa sio shujaa, ni mfano mbaya kwa vijana wa Tanzania!

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
WanaJF nimepandisha hapa kauli ya Chadema juu ya kile kilichoelezwa na viongozi wa CCM kuwa kujiuzulu kwa Lowassa ni ushujaa.

Nimeiattach taarifa hiyo hapa. Nimejaribu kuitazama maeneo mengine sijaiona.
Tuko pamoja

*************​

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- (Chadema) – Bavicha, linakemea jitihada zozote za kumtangaza waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa kuwa shujaa katika taifa letu.

Hali hii ikiachwa kuendelea inatoa mfano mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote katika taifa letu, mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya mafisadi (list of shame) kuenziwa kama shujaa wa taifa letu kwani ni kuharibu maana nzima ya ushujaa katika uwajibikaji.

Tumefuatilia jitihada za hivi karibuni za Lowassa, kupita akijitetea kuanzia katika hotuba yake alipokwenda Jimboni Monduli (yeye ni mbunge wake) na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na hata mahojiano yake maalumu na Televeshioni ya Taifa(TvT).

Aidha, tumeshangazwa na uamuzi wa Lowassa kuanza kujitokeza hivi sasa kujitetea kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond, kwani ni ishara ya unafiki wa kisiasa.

Baada ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilisha taarifa yake, Lowassa alipata nafasi bungeni takribani mara mbili kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni wakati akiwa waziri mkuu kuzungumzia suala hili, lakini hakutoa utetezi ambao sasa anajaribu kuutoa kwa umma.

Kadhalika, tumefarijika kwamba katika kujitetea kwake, Lowassa amethibitisha wazi uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ambayo aliyafanya alipokuwa waziri mkuu wakati wa sakata zima la Richmond.

Hivyo, tunatoa mwito kwa vyombo vya dola kuweza kumkamata, kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria dhidi ya uzembe na matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Badala ya Lowassa kuendelea kupita akijitetea kuwa Kamati Teule haikumuita kuweza kujieleza; vyombo vya dola vimkamate akatoe maelezo yake panapohusika. Vyombo vya dola vimekuwa vikiwakamata raia wa kawaida wenye taarifa za uhalifu kuweza kuisadia polisi, inashangaza Lowassa amejieleza wazi kuwa alikuwa anafahamu uhalifu uliokuwa ukitendeka lakini bado yuko nje akijitetea.

Tunaamini akikamatwa yeye, atawezesha watuhumiwa wakuu wa kashfa ya Richmond kuweza kupatikana. Jitihada zozote za kumlinda na kumtetea zinaweza kuathiri mwekekeo wa hatua ambazo zitanatarajia kupendekezwa na Timu ya Waziri Mkuu iliyoundwa kupitia ripoti na hatimaye kupendekeza adhabu kwa wahusika wote wa sakata lile.

Lowassa akiwa waziri mkuu amethibitisha kwamba maneno yake mwenyewe kuwa alikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na Sheria ya Makosa ya Udhibiti wa Uhujumu wa Uchumi wa nchi ya Mwaka 1984.

Pia Lowassa amekiri kwamba alikuwa anafahamu kwamba Richmond ni kampuni ya kitapeli, lakini katika kipindi chote cha uongozi wake aliinyamazia hali hii na kwa kiasi kikubwa aliitetea kampuni hiyo mbele ya macho ya umma.

Wakati wa viongozi mbalimbali wa upinzani walipoweka bayana kwamba Richmond ni kampuni isiyo na uwezo, serikali ilitetea kampuni hiyo. Vyombo mbalimbali vya habari vilimtuhumu Lowassa mwaka 2006 na 2007 kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, kwamba alishiriki ‘kuwaziba midomo' wabunge wa CCM wasijadili suala hili.

Ni huyu huyu Lowassa alinukuliwa akiwa Arusha akiwataka Watanzania wasiijadili kampuni ya Richmond baada ya mvua kuanza kunyesha. Kama Lowassa wakati wote huo alijua kama ni kampuni ya kitapeli kama anavyojaribu kujitetea sasa, uamuzi wake wa kuwaasa Watanzania wasiijadili ulikuwa ni wa kulinda ufisadi ambao aliufahamu.

Inashangaza pia ni Lowassa huyo huyo anayesema alijua kuwa Richmond ni kampuni ya kitapeli; ni Lowassa huyo huyo anasema kwamba alishauriwa vibaya na watumishi wa umma aliowataja kuhusu uwezo wa Richmond; Ni Lowassa huyo huyo anayesema kwamba alijua kuwa Tanesco, chini ya Menejimenti ya Net Group Solution, walitaka kuhujumu mchakato wa zabuni na hivyo ‘kuwanyang'anya'.

Lakini ni Lowassa huyo huyo aliyekuwa waziri mkuu ambaye angeweza kuviagiza vyombo vya dola kumwezesha kuthibitisha ‘utapeli wa Richmond'; hivyo, maelezo ya sasa ya Lowassa katika utetezi wake yanaonyesha kuwa ameanza kufinyanga ukweli kwa lengo la kujitetea, kupotosha umma na kujaribu kutafuta huruma.

Tumeshangazwa na Lowassa kutumia utetezi wake kueleza tu nia yake ya kutaka mkataba wa Richmond usitishwe; nia ambayo kama ni kweli alikuwa na uwezo wa kuitekeleza na hakuitekeleza.

Lakini tumemshangaa kwa kutokuzungumzia kabisa ni kwa vipi Richmond ilipewa zabuni hiyo na kwa shinikizo la nani.


Lowassa ameacha kuyazungumzia haya kwa kuwa anajua kabisa kwamba ni yeye aliyetumia madaraka yake vibaya alipokuwa kiongozi kwa kukiuka Sheria na Taratibu za Ununuzi kwa ‘kupora' mchakato uliokuwa ukiendeshwa na Tanesco, ‘kuunda kamati yake' na kuzisukuma mamlaka za ununuzi hali iliyopelekea Richmond kupewa tenda ili hali haikuwa na uwezo uliotakiwa.

Ni uzembe huu ambao umelisababishia hasara taifa kwa kulipa milioni 152/- kila siku kwa kampuni ya Dowans iliyohamishiwa mkataba wa kitapeli wa Richmond; na takribani bilioni 172 kwa ujumla ambazo taifa linawajibika kuzilipa kutokana na kukodisha mitambo hiyo.

Kwa vyovyote vile, jitihada za Lowassa za kuhamasisha ujenzi wa Sekondari Kata, na utumishi wake kama waziri mkuu katika kipindi cha miaka miwili, haviwezi kuzidi hasara aliyosababisha katika uchumi wetu kipindi chote tulichokosa umeme wa dharura na wala hailingani na hasara ambayo tunaendelea kuilipa kila siku iendayo kwa Mungu.

Maamuzi haya ya Lowassa yanaendelea kuwaumiza wananchi wote ikiwemo wa jimbo lake la Monduli ambao wanataabika kwa mzigo wa gharama za umeme.

Tunapenda kumkumbusha Rais Jakaya Kikwete kwamba Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma: kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.

Kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma. Hivyo, tumefadhaishwa na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwamba Lowassa amepata tu ‘ajali ya kisiasa', na kumsifu kwa utumishi wake.

Tunategemea baada ya Lowassa kukiri mwenyewe hadharani kuhusu uzembe wake na matumizi mabaya ya madaraka Rais Kikwete ataelekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yake badala ya kuendelea kumpamba kama "shujaa wa uwajibikaji', kinyume na hayo tutaamini kwamba serikali yake inaendeshwa kwa ‘ubia wa kulindana'.

Aidha, tunatoa rai kwamba Rais Kikwete kuwafukuza kazi watumishi wote wa umma waandamizi ambao wametajwa na Lowassa kushiriki uzembe na matumizi mabaya ya madaraka; watumishi ambao walitajwa pia na Kamati Teule ya Bunge, lakini mpaka sasa wanaendelea kutumikia nafasi zao mbalimbali.

Kadhalika tunapenda kuvikumbusha vyombo vya dola kwamba Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kuhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi ni pamoja na yale yote yenye kusababisha hasara kwa mamlaka za serikali.

Pia Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inatamka kuwa ubadhirifu na/au ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na watumishi wa umma na Matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi, ni sehemu ya ufisadi.

Lowassa amethibitisha kwamba maneno yake kwamba wapo viongozi waandamizi wa serikali ambao amewataja kwa majina wamefanya maamuzi ya kifisadi, kitendo chake cha kunyamazia ufisadi huo- kinafanya iwe vigumu kwa yeye kutenganishwa na tuhuma za ufisadi zilizomo katika mchakato mzima wa kupewa tenda kwa kampuni ya Richmond na mambo yote yaliyotokea baada ya mkataba huo kuhamishiwa kwa kampuni ya Dowans.

Aidha, tunamuonya Lowassa kutoendelea kujifananisha na Ali Hassan Mwinyi kwani kufanya hivyo ni kumchafua rais huyo mstaafu wa awamu ya
pili.

Lowassa akumbuke kuwa Mwinyi hakujiuzulu kwa tuhuma za ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka aliyofanya yeye katika nafasi yake bali watumishi katika eneo lingine kabisa ingawa walikuwa chini yake.

Mwinyi hakujiuzulu kwa shinikizo kama Lowassa. Tunamkumbusha kwamba tangu sakata la Richmond lilipoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita, tulimtaka Lowassa kujiuzulu kulinda heshima yake, lakini alikaidi na kuitetea kampuni ya Richmond.

Uamuzi wa yeye kujiuzulu baada ya kashfa yote kuwa hadharani, umesaidia tu kuilinda serikali ya CCM, lakini katu hauwezi kumpatia heshima ya uwajibikaji aliyoionyesha Rais Mwinyi.

Wakati huo huo, Lowassa ameibua ushahidi mwingine kwamba alivieleza vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu ‘utapeli' wa kampuni ya Richmond; kama maelezo yake ni ya kweli ni sababu nyingine ya imani ya vyombo hivi kuendelea kupungua.

Tunarejea tena rai yetu kwa Rais Kikwete ya kumtaka kuvunja Kamati ya Kuchunguza ufisadi wa Bilioni 133 katika akaunti ya Kulipia Madeni ya Nje(EPA) kwani wakuu kadhaa wa kamati hiyo, ikiwemo wa vyombo vya usalama wametuhumiwa kuwemo kwenye kashfa ya Richmond na hata
ufisadi katika BOT.

Badala yake, iundwe Tume Huru ya Kuchunguza Ufisadi wote kama ambavyo ilitakiwa na viongozi wakuu wa ushirikiano wa vyama vya upinzani nchini.

"Inasikitisha vijana wamachinga kuendelea kukosa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara; wanafunzi wa elimu ya juu wakipandishiwa ada na wengine kukosa mikopo- huku fedha za walipa kodi zikiendelea kuteketea kwa ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kutamba hadharani"

* Imetolewa na Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema John Mnyika.
 

Attachments

  • LOWASSA SIYO SHUJAA.doc
    52 KB · Views: 113
Wengi mtaponda lakini ukweli haufichiki. Katika viongozi Lowasa ndiye aliyeonyesha sio utendaji mzuri tu hata uwajibikaji. Waulize waliofanya kazi katika wizara enzi zake ubabaishaji haukuwepo. Njama ya kuondolewa uwaziri mkuu hata western wameshiriki kwa kiasi kikubwa kwa kuwa alokuwa kama threat katika maslai yao.
 
Naona mnazidi kumpaka MAFUTA na MANEMANE...............!

Subirini 2015, ukweli utajulikana kama maharage ni mboga au futari............. LOL
 
Wengi mtaponda lakini ukweli haufichiki. Katika viongozi Lowasa ndiye aliyeonyesha sio utendaji mzuri tu hata uwajibikaji. Waulize waliofanya kazi katika wizara enzi zake ubabaishaji haukuwepo. Njama ya kuondolewa uwaziri mkuu hata western wameshiriki kwa kiasi kikubwa kwa kuwa alokuwa kama threat katika maslai yao.
Nikweli kabisa hujakosea lakini Kama unampenda sana kawe mpishi wake
 
Nasikiliza DW hapa kipindi cha MTU NA MAZINGIRA. Mtangazaji Alfred Kiti anawahoji wakulima huko Arusha ambao kutokana na njia bora za kilimo hususani "rutuba udongo", mavuno yameongezeka mara dufu. Lakini hawana soko.

Lowasa alipendekeza njia rahisi sana ya kumnyanyua mkulima ambayo ni kuuza mazao nje ya nchi bila urasimu, ukwasi wala vikwazo. Hili linalalamikiwa pia na wakulima wa Korosho Mtwara ambao wanakopwa na Serikali !!! Kama walivyofikisha malalamiko yao kwa Kinana.

Inatakiwa nguvu ya soko itawale, sio wanasiasa kuingilia every aspect of our life, especially when their policies are a proven failure.
Ni aibu tunazungukwa na nchi zenye migogoro na majanga ya kila aina ambazo tunaweza kuzilisha lakini wakulima eti hawana soko !!!!
Lowasa atawaokoa wakulima wa nchi hii.
 
Nasikiliza DW hapa kipindi cha MTU NA MAZINGIRA. Mtangazaji Alfred Kiti anawahoji wakulima huko Arusha ambao kutokana na njia bora za kilimo hususani "rutuba udongo", mavuno yameongezeka mara dufu. Lakini hawana soko.

Lowasa alipendekeza njia rahisi sana ya kumnyanyua mkulima ambayo ni kuuza mazao nje ya nchi bila urasimu, ukwasi wala vikwazo. Hili linalalamikiwa pia na wakulima wa Korosho Mtwara ambao wanakopwa na Serikali !!! Kama walivyofikisha malalamiko yao kwa Kinana.

Inatakiwa nguvu ya soko itawale, sio wanasiasa kuingilia every aspect of our life, especially when their policies are a proven failure.
Ni aibu tunazungukwa na nchi zenye migogoro na majanga ya kila aina ambazo tunaweza kuzilisha lakini wakulima eti hawana soko !!!!
Lowasa atawaokoa wakulima wa nchi hii.

...........ndo basi tena ! Watz wamemkataa kabisaaaa!
 
El si tu shujaa bali ni kiongozi mfano wa kuigwa tz kwa kazi nzuri na usimamizi mzuri ktk uongozi wake mfano bila yeye sekondari za kata hazingekuwepo lakini pia ni kiongozi asiye ogopa kuchukua maamuzi magumu kiongozi asie penda kulalamika kama akina zito slaa mbowe munyika mdee na wengine wanaofanana hao wapenda kuuza sura kwenye tv ambao mnawafahamu hivyo muungeni mkono lowasa awe RAIS WA AWAMU YA NNE TZ mungu mbariki lowasa mungu ibariki Tz
 
Kichuli shule za kata zilikuwepo sema wakati ule zilikuwa zinaitwa shule za kutwa na zilikuwa chini ya centra govt. Mimi nimesoma shule hizo. Wilayani kwetu kwenye kila kata mbili kulikuwa na shule moja sema ujenzi wake haukuwa direct kwa wananchi kwani walikuwa wakisubiri fedha kutoka serikalini na wao walikuwa wanachangia kidogo tu. Shule niliyosoma ilikuwepo tangu 1989. Ilikuwa shule yenye walimu wa kila somo japokuwa ilikuwa porini lakini leo hii ni ndoto kuwa na mwalimu wa physics na hesabu shuleni hapo. Alichofanya lowasa ni kuongeza msukumo wa ujengaji na kuwaambia waongeze idadi ya ya wanafunzi japokuwa madarasa mengi yapo hoi mpaka leo. Walosoma kipindi hiki hawatamsahau lakini ni mwizi. Labda kuwe na sera ya taifa kwenye kila kitu ambapo ukienda tofauti unaondoka! Hapo ndipo lowasa atafaa, vinginevyo duh! Another ten years of suffering ambapo yeye na wahuni wenzie kina kinana wanakuwa wanashangilia
 
el si tu shujaa bali ni kiongozi mfano wa kuigwa tz kwa kazi nzuri na usimamizi mzuri ktk uongozi wake mfano bila yeye sekondari za kata hazingekuwepo lakini pia ni kiongozi asiye ogopa kuchukua maamuzi magumu kiongozi asie penda kulalamika kama akina zito slaa mbowe munyika mdee na wengine wanaofanana hao wapenda kuuza sura kwenye tv ambao mnawafahamu hivyo muungeni mkono lowasa awe rais wa awamu ya nne tz mungu mbariki lowasa mungu ibariki tz

ni upofu tu wa tz wachache ambao huwa hawataki siku zote kufahamu ukweli kuwa el hafai na amechafuka sana na hata ukimuosha vipi bado hawezi kutakata. Muulizeni mwakyembe awajulishe zaidi.
 
Haya bana kila siku lowasa lowasa jamani huyu alishashindwa siku nyingi sema ndo ivo tena jamii yetu imeshaharibika kwa ufisadi kwa hiyo tunaona kawaida mamboi ya msingi yakiharibiwa na wachache kwa manufaa yao.
 
El si tu shujaa bali ni kiongozi mfano wa kuigwa tz kwa kazi nzuri na usimamizi mzuri ktk uongozi wake mfano bila yeye sekondari za kata hazingekuwepo lakini pia ni kiongozi asiye ogopa kuchukua maamuzi magumu kiongozi asie penda kulalamika kama akina zito slaa mbowe munyika mdee na wengine wanaofanana hao wapenda kuuza sura kwenye tv ambao mnawafahamu hivyo muungeni mkono lowasa awe RAIS WA AWAMU YA NNE TZ mungu mbariki lowasa mungu ibariki Tz
Du hii thread mbona ya 2008 ni kweli haikuchangiwa hadi leo? ilikuwa wapi?

@Kichuli hizo Sekondari za Kata naona huko kwenu Kondoa hazikuwepo na Umasaaini (Manyara na Arusha) lakini Mkoa wa Kilimanjaro, Mbeya nk zilikuwepo miaka ya 80' na kwa sasa ni kila kijiji huko Kilimajaro wana Sekondari za kata hadi A level na ni za Serikali hapo hujahesabu za Mashirika ya DINI

LOWASSA CHENGE.jpg LOWASSA CHENGE.jpg
 

Attachments

  • Lowassa.jpg
    Lowassa.jpg
    18.2 KB · Views: 56
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom