Lowassa: Silijui shamba la Lukuvi, asema hakuna ardhi ambayo anaimiliki kinyume cha taratibu

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Lowassa-na-Lukuvi.jpg


Baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza Bungeni kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha ardhi iliyotolewa kwa wananchi wilayani Monduli mkoani Arusha na kuahidi kuirejesha, Mwanasiasa huyo amejibu tuhuma hizo.

Lowassa amesema kuwa halijui shamba alilolizungumzia Waziri huyo na kwamba hakuna ardhi ambayo anaimiliki kinyume cha taratibu.
Alisema kuwa hana taarifa kamili kuhusu maelezo ya Waziri Lukuvi na kwamba ameomba Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA) kulifuatilia kwa karibu na kumpa taarifa ili aweze kulitolea ufafanuzi.

“Nashindwa kutoa maelezo kuhusu taarifa hizo kwa sababu sifahamu lolote kuhusu shamba hilo,” Lowassa anakaririwa na gazeti la Jambo Leo lililofanya nae mahojiano kwa njia ya simu. “Mimi sipo Bungeni, nimesikia hizo habari, lakini sijui zimetolewa lini na nani. Mbunge wangu analifanyia kazi kwa sababu sina shamba nilalolimiliki ambalo liko kinyume na taratibu,” aliongeza.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Monduli kuhusu umiliki na uporaji wa ardhi unaofanywa na vigogo jimboni humo, Waziri Lukuvi alieleza kuwa kuna shamba ambalo lilidhaminiwa na Rais Benjamin Mkapa ili wapewa wananchi jimboni humo, lakini Lowassa alijimilikisha.

“Lile Shamba la Makuyuni lilitolewa kwa wananchi litarudi kwao na ukae ukijua litakuwa kwao kwa sababu aliyejimilikisha ni Edward Lowassa,” alisema Lukuvi na kuahidi kulirejesha mikononi mwa wananchi hao.
 
Hata RICHMOND alikuwa haijui.

Ni huyu huyu alisema hana mpango wa kuhamia upinzani kwani maisha yake tangu mwaka 1977 alipohitimu chuo kikuu yamekuwa ni ndani ya CCM.

Unadhani anaweza kulijua shamba?

Mbona mnakuwa kama hamfahamu kuwa Lowassa ana shahada ya usanii kutoka UDSM.

Kuna uwezekano pia atawakana CHADEMA.
 
Viongozi wa siasa kutafuta Kiki Kupitia huyu mzee sijui kutaisha lini#Kweli ukiona wanakuongelea sana ujue unawakuna
 
Back
Top Bottom