Elections 2015 Lowassa: Serikali yangu itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba wa bandari ya Bagamoyo

Rejea hoja ya mleta mada nimeandika hivyo kumjibu! Kuhusu bandari ya Bagamoyo hata mimi mwenyewe sioni umuhimu wake kwa sasa na siuelewi vizuri huu mradi kuhusu gharama zake ni nani atalipa? Kama ni mkopo masharti yake yakoje, na faida yake hasa ni nini ikilinganishwa kuwekeza fedha kwenye labda kwenye kuunganisha bandari ya Mtwara na Ziwa Nyasa (Mtwara corridor) mradi ambao ulibuniwa tangu enzi za Mkoloni Mjerumani ila alishindwa kuutekeleza kwa sababu ya muda na ukafufuliwa na Raisi Ben Mkapa lkn na yeye kushindwa kuukamilisha kwa sababu ya muda!

Hivyo kwa kifupi hata mimi sielewi mantiki ya hii Bandari (Bagamoyo) ni lazima niwe mkweli!
Umekiri vyema huo ni mradi wa hovyo kabisa... bila hata kujali majirani tulihitaji kuboreshaa bandari zetu tanga..dar mtwara kwa faida ya watu wetu kwanza...imagine mtu yuko mtwara an clear gari bandari ya dar..mwee shidaa
 
Anachunguza jambo kwa undani kisha anaongea kwa ufasaha,lazima ushangae! Machozi yatakulenga tu!
Kwa haraka Mheshimiwa Edo ni mchunguz mzuri na anafamu mambo mengi khs Tanzania hasa yale yaliyo jificha.

Ni jukumu letu watanzania
 
Rejea hoja ya mleta mada nimeandika hivyo kumjibu! Kuhusu bandari ya Bagamoyo hata mimi mwenyewe sioni umuhimu wake kwa sasa na siuelewi vizuri huu mradi kuhusu gharama zake ni nani atalipa? Kama ni mkopo masharti yake yakoje, na faida yake hasa ni nini ikilinganishwa kuwekeza fedha kwenye labda kwenye kuunganisha bandari ya Mtwara na Ziwa Nyasa (Mtwara corridor) mradi ambao ulibuniwa tangu enzi za Mkoloni Mjerumani ila alishindwa kuutekeleza kwa sababu ya muda na ukafufuliwa na Raisi Ben Mkapa lkn na yeye kushindwa kuukamilisha kwa sababu ya muda!

Hivyo kwa kifupi hata mimi sielewi mantiki ya hii Bandari (Bagamoyo) ni lazima niwe mkweli!

Navhoweza kusema, bandari ya Bagamoyo ni siasa tupu. Kulikua na mradi wa Bandari ya Tanga( eneo la Mwambani sijui-spelling) lakini kimyaaa. Siasa inaamua mambo mengi(political will).
Kama professionalism ingekua inaheshimiwa, huwez kuiacha project ya Mtwara Corridor halafu kipaumbele kikawa ni kuanzisha bandari mpya wakati ile ya corridor la kusini ambako traffic congestion pale bandarin na hata barabaran ni ndogo na hivyo ni rahisi kusafirisha bidhaa. Bagamoyo bado ni shida kwani iko jiran na Dar es Salaam na hivyo baada ya miaka 10,shida ya msongamano wa magari itajitokeza kwa haraka. Political Will ndiyo mpango mzima!
 
Sio wewe tu mkuu...

Ukisoma maoni mbalimbali ya watu wa uchumi juu ya mradi huo wa bandari, wanaeleza bayana kuwa ni mradi pata potea...

Ni uwekezaji ambao hauna uhakika wa kurudisha faida na wameshauri ni vyema kupanua bandari zilizopo...

Na mbaya zaidi unawekeza pesa za mchina ambaye huwezi kulipa pesa yake.

Ili akusamehe inabidi alete makampuni yake yaje kufanya biashara bure bila kulipa kodi.

Biashara kichaa hii.
 
Aisee kanigusa sana. Halafu lowassa ana hekima
sana. Kajiepusha ku msema ovyo jk. Yaani huyu
ndugu ni muungwana sana. Ana bahati mbaya
kuwa alikuwa na rafiki mnafiki
. Hilo jambo la bandari ya bagamoyo kama magu
ni kidume alizungumaie

Magufuli yupo pale kama boksi, hawezi kuongoza nchi bila maamuzi ya CCM.

Magufuli hata kaa awaze kuzima hii bandari.
 
Sasa naanza kuelewa kwanini serikali na CCM kwa ujumla wanajitahidi kwa kila mbinu kumkandamiza na kumdidimiza Lowassa, hakuna jiwe litakaloachwa bila kugeuzwa!

Watu wengi sana wanaoinyonya Tanzania hawatampenda Lowasa kabisa.
 
Kutoka Dar to Bagamoyo ni Km 45. Dar kuna Bandari tena kubwa, then leo hii unataka kujenga bandari nyingine Bagamoyo. Hiyo ni akili au matope
 
Mkuu maelezo yako yanaeleweka. Nadhani Lowasa asiingie madarakani na kusnza kulipiza visasi.
Kuna mambo mengine sio ya kuyaongelea sasa hivi. Angoje hadi awe rais.mpkaka hapo kura za bagamoyo hajazikosa?

Nadhani anaangalia kwenye picha kubwa.

Anaweza kukosa kura za wana bagamoyo (anaweza asipate pia hata kama hajaongelea kuhusu huu mradi) lakini akapata za wengine wenye nia njema na hii nchi.
 
Kutoka Dar to Bagamoyo ni Km 45. Dar kuna Bandari tena kubwa, then leo hii unataka kujenga bandari nyingine Bagamoyo. Hiyo ni akili au matope

Moja ya sababu za kufeli kwa plans alinifundisha mwalimu wangu wa economics 101 ni kama hii hapa "political allocation of resources".
 
Kutoka Dar to Bagamoyo ni Km 45. Dar kuna Bandari tena kubwa, then leo hii unataka kujenga bandari nyingine Bagamoyo. Hiyo ni akili au matope

Hiyo Bandari ya Dar unaweza kuipanua mara 4 zaidi na hiyo hela na ukaanza kujenga reli ya kati kwa SGR hadi dodoma.
 
Safiiiiii Lowassa... Very intelligent...!!!

Nimefurahi sana, sbb hakuna sababu ya kuwa na bandari Bagamoyo wakati ya Tanga inaachwa bure... Ingetakiwa tuboreshe na kujenga bandari kubwa Tanga.. sio Bagamoyo...!!

Tetesi ni kuwa BANDARI YA BAGAMOYO ITATUMIWA BUREEEEEE NA CHINA KWA MIAKA 50 IJAYO...!!!

Kama China watatumia hiyo BANDARI YA BAGAMOYO miaka 50 bure.... nchi yetu Tanzania itabakia HAKUNA KITU...CHINA WATAKOMBA KILA KITU... TENA NASIKIA NI JESHI LA CHINA...!!! HIVYO NI MKATABA HATARI SANA SANAAA...!!! China wataimaliza nchi hii jamani...!!!

Lowassa tukomboe...!!!

Nimeona bora muwekezaji mzungu kuliko mchina.
 
Magufuli yupo pale kama boksi, hawezi kuongoza nchi bila maamuzi ya CCM.

Magufuli hata kaa awaze kuzima hii bandari.

Magufuli hana ubavu kuhusu Katiba Mpya, hana ubavu na miradi mfu isiyo na tija kama huu. Atabaki kuwa bubu milele na kulialia tu sitawaangusha wakati anatuangusha kwa kukaa kimya mbele ya mambo ya ovyo kama haya!
 
Leo katika taarifa ya habari ya Channel Ten nimemsikia Rais mtarajiwa wa awamu ya tano Ngoyai Lowassa akisema kwamba Serikali yake itaangalia jinsi ya kuuvunja mkataba wa bandari ya Wachina Bagamoyo.

Amesema haoni mantiki ya kutumia mabilioni kujenga bandari moja Bagamoyo wakati bandari za Tanga na Mtwara ziko ovyo.

Kama kawaida wananchi wa Tanga wamesema kura zao zote ni kwa UKAWA na adui CCM lazima asome namba mwaka huu.

VIVA UKAWA!

NOTE: Kwa msio fahamu kuna umbali wa kilomita 1200 kutoka Tanga mpaka Kampala (Uganda) ukilinganisha na kilomita 1500 kutoka Mombasa (Kenya) mpaka Kampala.

Lakini Waganda wanatumia bandari ya Mombasa sana kwa sababu Tanga hamna kitu.
Bandari ya Bagamoyo si muhimu sana kama ni kujenga Bandari wangejenga kule mkuranga au lindi kisha kuzijenga Bandari za mtwara na Tanga, kisha kujenga Bandari maalum ya magari tu kule Kigamboni nyuma Kimbiji iwe Bandari maalum ya magari pekee kama wanavyofanya South Africa wana Bandari maalum ya magari pekee kule Darban.
 
Umekiri vyema huo ni mradi wa hovyo kabisa... bila hata kujali majirani tulihitaji kuboreshaa bandari zetu tanga..dar mtwara kwa faida ya watu wetu kwanza...imagine mtu yuko mtwara an clear gari bandari ya dar..mwee shidaa

kweli wewe zaga x2, unategemea meli itatoka japan ina shehena ya magari kwa maelfu na muelekeo ni dsm tz. itie nanga mtwara kushusha magari pengine haya zidi 20.
 
kweli wewe zaga x2, unategemea meli itatoka japan ina shehena ya magari kwa maelfu na muelekeo ni dsm tz. itie nanga mtwara kushusha magari pengine haya zidi 20.

Kwani magari yanayoshuka bandari ya DSM yanabaki Dar yote?
 
Kwa wenye akili zetu tulimwelewa mapema mzee kingunge, tangu 2005 Uchumi WA Tanzania ulisimama, kwa mana nyingine tumerudi nyuma.mwaka 2004 uchumi ulifikia kukua kwa 7% Leo uchumi unakuwa 2015 kwa 7%.Akili matope.Lowassaaaaaaaaaaaaaaaaamabadiliiiiiiiikoooooo
 
Back
Top Bottom