Lowassa, Rostam waumbuana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Rostam waumbuana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 8, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  Na Saed Kubenea

  MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

  SIRI imefichuka. Vigogo waliojaribu kuiba ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond kabla ya kuwasilishwa bungeni, waliiba “kanyaboya,” MwanaHALISI limegundua.

  Taarifa mikononi mwa gazeti hili na ambazo zimethibitishwa na gazeti la Rai toleo Na. 814 la Alhamisi iliyopita, zinasema kuna tofauti kubwa kati ya taarifa iliyokwapuliwa mapema na taarifa halisi iliyowasilishwa bungeni.

  Gazeti la Rai linalomilikiwa na Rostam Aziz, limeandika kwa mshangao na kulalama, kuwa “…Sehemu ya 7.0 ya taarifa zote mbili inazungumzia ‘HITIMISHO NA MAPENDEKEZO,’ (lakini) taarifa ya kwanza haina mapendekezo yoyote wakati ile ya pili ilikuwa na mapendekezo.”

  “Shabaha kuu ya kutaka kuiba taarifa ilikuwa kuona iwapo wanatajwa kwa majina ili waweze kujiandaa kukabiliana na tuhuma. Lakini katika haraka waliiba kanyaboya na kuanza kujigamba kuwa hawahusiki,” ameeleza mtoa habari kwa gazeti hili.

  Toleo la Rai lililochapisha habari za kuhitilafiana kwa taarifa, lenye kichwa cha habari “Siri nzito Richmond” na kuuzwa katika baadhi ya mikoa ikiwemo Iringa, Lindi na Ruvuma, limelalama kuwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa hayumo katika ripoti ya kwanza lakini anatajwa katika ripoti iliyowasilishwa bungeni.

  Wachunguzi wanasema kuchapisha taarifa zinazolenga kusafisha Rostam na Lowassa, katika gazeti linalomilikiwa na mmoja wao (Rostam), kunaonyesha kuwatuhumu watu hao kuwa ndio wahusika wakuu katika kupatikana kwa nyaraka ambazo zilikuwa siri hadi zilipowasilishwa bungeni.

  Bunge liliteua Kamati maalum kuchunguza mazingira ya rushwa na upendeleo katika mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company LLC. Kamati ilikabidhi ripoti yake Februari 2008.

  Kamati ilitaarifu katika hitimisho kuwa Richmond ilikuwa kampuni feki, isiyo na uwezo kifedha wala kitaaluma na kwamba ilibebwa na ubabe wa Lowassa katika kushinikiza wizara ya nishati na madini.

  Habari ya gazeti hilo iliyochukua ukurasa wa mbele na wa pili – ikibeba picha za Lowassa na Harrison Mwakyembe – inatafuta kujenga utetezi kwamba, kwa vile Lowassa na Rostam hawakutajwa katika ripoti iliyoibwa, basi hawakustahili kuwa katika ripoti ya mwisho na sahihi iliyowasilishwa bungeni.

  Wakati Lowassa alihusishwa na shinikizo kwa wizara, Rostam alituhumiwa kuwa na uhusiano na Richmond na baadaye kampuni ya Dowans ambayo baadaye ilichukua mkataba wa Richmond.

  Zaidi ya mashahidi watano kwenye Kamati teule ya Bunge walitaja Rostam kuwa na uhusiano na Richmond na Dowans kwa vile makampuni hayo yalikuwa yakitumia anwani ya posta na anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Company Ltd.

  Kamati Teule ilipata pia majina ya baadhi ya wafanyakazi wa Caspian ambao pia walikuwa wanaitumikia Dowans Holdings A.A.

  Kuna taarifa kuwa nakala ya taarifa kanyaboya iliangukia mikononi mwa Rai katika mbinu na juhudi maalum za kujaribu “kusafisha majina ya Lowassa na Rostam.”

  Tayari Rostam ametajwa na Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi na Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaam kuwa mmoja wa watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini.

  Ni Rostam ambaye inadaiwa akaunti yake katika benki ya Exim jijini Dar es Salaam ndiyo iliyohamisha fedha kwenda nje kununua mitambo ya kufua umeme ya Richmond na dada yake Dowans.

  Aidha, Rostam amekuwa akituhumiwa kuhusika na kampuni tata ya Kagoda Agriculture Limited ambayo ilikwapua zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) lakini serikali haijamchukulia hatua.

  Chanzo cha habari kinasema wizi wa taarifa isiyokamilika ulifanywa kabla ya mke wa Lowassa, Regina kwenda kwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Mwakyembe na kumpigia magoti akimsihi kumuokoa mume wake na zahama ya Richmond. Dk. Mwakyembe ndiye aliwasilisha ripoti bungeni.

  Naye Spika Samwel Sitta alipoonyeshwa gazeti lenye madai dhidi ta kamati teule, alisema huku akitabasamu, “Ripoti kamili ni ile iliyowasilishwa bungeni.”

  Sitta alisema kuwa alipokea ripoti ya kwanza ya mahali walipofikia na “baadaye wakaniambia hawajamaliza na kuwa wanaomba muda zaidi. Nikawapa muda wakamalizia, na ripoti ya mwisho ndiyo hiyo iliyowasilishwa bungeni. Tatizo liko wapi?”

  Taarifa za ndani ya kampuni ya New Habari Corporation inayochapisha gazeti la Rai zinasema toleo lililojaa malalamiko ya Lowassa na Rostam, lilisitishwa kusambazwa baada ya mmiliki (Rostam) kuhofia Mwakyembe kujibu mapigo.

  Rostam amenukuliwa akimwambia mmoja wa wahariri wa gazeti lake, “Msisambaze toleo hili. Mwakyembe anajua mambo mengi na bado hajayasema. Mkilisambaza Mwakyembe atalipuka na mtakuwa mmenimaliza,” ameeleza mtoa habari akimnukuu Rostam.

  Mwakyembe aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwezi uliopita kuwa “kuna siku nitalipuka na tusiheshimiane kabisa,” akimlenga Rostam ambaye alidai ametumia vyombo vyake vya habari kumchafua.

  Woga mwingine wa Rostam unatokana na taarifa ya gazeti kudai kuwa wabunge waliokuwa wajumbe wa Kamati teule hawakuwa waadilifu, jambo ambalo lingeonekana ni kufufua hoja iliyohitimishwa rasmi ambayo ni kinyume cha kanuni; kuvunja heshima ya Bunge na Spika.

  Hata hivyo taarifa zinasema amri ya kuzuia gazeti kuuzwa haikufika sehemu zote nchini kiasi kwamba MwanaHALISI liliweza kuagiza nakala za toleo hilo kutoka Iringa.

  Badala ya toleo lililozuiliwa na mmiliki, kampuni ilichapisha toleo jingine la tarehe hiyohiyo na namba ileile ya toleo lenye kichwa kisemacho “ Reginald Mengi aivuruga taaluma ya habari nchini.”

  Wachunguzi wa mwenendo wa vyombo vya habari wanasema kitendo cha Habari Corporation kutoa matoleo mawili, kwa tarehe moja na namba ileile ya toleo, kingekuwa kimefanywa na MwanaHALISI, basi gazeti lingekuwa linatishiwa kufungiwa na serikali kama ilivyokuwa siku zote.

  Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge juu ya Richmond aliliambia gazeti hili kuwa katika uchunguzi huwa kuna hatua mbalimbali za kuandika taarifa.

  Amesema kinachoonyeshwa kuwa taarifa tofauti ni moja ya hatua hizo ambayo wahusika na walioitoa katika magazeti walikuwa na nia ya kuingilia kazi za kamati au kutafuta kujinasua kabla ya wakati wake.

  “Hata sisi tulikuwa tunajua kuwa kazi tunayofanya ni muhimu na inawindwa na wengi na hivyo kulikuwa na suala la ‘kutoweka mayai yote katika kapu moja.’ Ndipo wao wakaambulia kitu tofauti,” alisema.

  Kwa takriban mwaka mmoja sasa kumekuwa na juhudi za kutekeleza kile kinachojulikana sasa kuwa ni “kumsafisha Lowassa na washirika wake.”

  Kila kunapotokea upenyo, hoja zinajengwa haraka, “Lowassa alisulubiwa bila makosa.” Lakini hakuna mwenye utetezi ambao hadi sasa umeweza kumnasua kutoka kwa kashfa Richmond.
   
 2. m

  mnozya JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mzee wa vipande vya magazeti nakushukuru sana kwa kutuhabarisha hususani sisi tuliopo ng'ambo ya Tanzania, ukizingatia website ya Mwanahalisi haina cha maana ila ni miongoni mwa magazeti makini ya taarifa za kichunguzi.

  Ombi, ANAYEWEZA AU KAMA UTAWEZA KUKIPATA KIPISI CHA RAI ILIYOSITISHWA NAOMBA UTUBANDIKIE HAPA ili tuwachambue vema hao mafisadi PAPA.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kubenea anayo magazeti yote alionyesha kwenye mkutano wa RA
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  guys this guy Rostam and his company (new habari cooperation) will kill our beloved country. Amani inatoweka kwa kasi sana, Serikali imekalia kumlinda na kunyanyasa wnyonge. why? jamaa huyu.. aghr
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Watu hawana kumbukumbu.. niliandika wakati ule mada ya "Jinsi Lowassa alivyoanguka".. inaelezea jinsi kina RA walivyotegwa wakategeka..
   
 6. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuanguka kwa Lowasa and RA will be just a little shake up for changes we need in Tanzania. CCM bado iko madarakani kwa mda mrefu sana, na suruhisho la mabadiliko tunatioyataka Tanzania yanatakiwa yaanze kwasisi ku i shake CCM, If we can reform CCM and make it better we will move miles ahead than the one we travelling now, Hata kama kina RA WATAFUNGWA Kitakachotokea ni kwamba ttutarudi hapa after few years cying after the same virio with new RA, Lowassa and dowans . Kushindwa kwetu kuishake up CCM na ku push reform ndani ya CCM ndio imekuwa sababu kubwa ya kutuzalishia mafisadi, From Chavda, Mama mkapa and many other, Hii hari imekuwa ikijirudia kwasababu catalyst ya ufisadi bado ipo ndani ya CCM . CCM ni sikio la kufa lisilo sikia Dawa, AND IT IS ONE JOB TO TAKE ON CCM and push for reforms neccesary for changes we want to see in Tanzania
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  If it is found to be true that RA uses his paper for propaganda reasons the people should stop buying his papers on news stands. The less circulated and read his newspapers are the less his propaganda can spread. The only problem is how do we achieve this.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nawasisafishike kamwe watupishe tuanze upya
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  Lowassa, Rostam wazimwa​

  [​IMG]

  • Ni katika sakata la Richmond
  • Bomu la Dk. Mwakyembe kiporo
  Na Saed Kubenea

  MwanaHALISI


  TUNDU la kutokea la Edward Lowassa, ili akwee upya kwenye uongozi wa juu nchini, tena kwa kishindo, limezibwa, MwanaHALISI limegundua.
  Taarifa zinasema ilitarajiwa Lowassa aibukie kwenye mkutano wa 16 wa Bunge ambalo kikao chake cha mwisho kilikuwa Jumamosi iliyopita mjini Dodoma.

  Kama ilivyokuwa Februari mwaka jana, kile ambacho kimeziba tundu la Lowassa ni kashfa ya mkataba wa kufua umeme kati ya Tanesco na kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (LLC).
  Ilitarajiwa baada ya serikali kuwasilisha taarifa inayowaondolea jinai baadhi ya watuhumiwa katika kashfa hiyo, basi Lowassa angeibuka kidedea na huo ndio ungekuwa mwanzo wa kurejea kwenye jukwaa kwa vifijo.

  Wiki mbili zilizopita serikali, kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliwasilisha bungeni uamuzi wa serikali uliosema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika hakuwa na kosa la jinai.

  Uamuzi huo ulimuhusisha pia Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Edward Hoseah na kusema hakuwa na jinai yoyote isipokuwa "mamlaka" imemuonya kwa "kutokuwa makini" katika kupokea na kuchambua taarifa za walio chini yake.
  Wengine ambao walihusishwa na uamuzi wa serikali ni Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Arthur Mwakapungi na wajumbe wengine wa Kamati ya majadiliano kuhusu Richmond chini ya mwenyekiti Singi Madata.
  Uamuzi wa serikali uliamsha hisia tofauti miongoni mwa wabunge wa pande mbili; wale ambao wanajitambulisha na mapambano dhidi ya ufisadi na waliojitwisha au waliopewa jukumu la "kuwasafisha watuhumiwa."
  Taarifa ya serikali "kuwasafisha" watuhumiwa kuwa haikuona jinai, ilichochea juhudi za muda mrefu za Lowassa kuibuka upya.

  "Huu ulikuwa upenye mpya na wa mwisho kwa Lowassa kusafishwa na mamlaka ya nchi. Hakutarajia mabadiliko yoyote ambayo yangesitisha kile ambacho serikali ilikuwa imeweka mkono wake," ameeleza mbunge mmoja wa kambi yake.

  Lakini Jumamosi iliyopita, siku ambayo mkutano wa Bunge wa 16 ulikuwa unafikia tamati, mambo yalibadilika baada ya baadhi ya wabunge kuchukua msimamo mkali dhidi ya hatua ya serikali na jinsi ilivyopeleka taarifa yake bungeni.

  Karibu wabunge wote wenye sauti na ushawishi – Dk. Willibrod Slaa, Christopher ole Sendeka, Stella Manyanya, Hebert Mtangi na Said Mkumba, waliikaba koo serikali wakiikosoa kwa kile walichoita "kusamehe watuhumiwa."

  Wabunge hao walikuwa wakijadili taarifa ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini juu ya taarifa ya serikali kuhusu Richmond na hatua ya serikali iliyowasilishwa bungeni. Taarifa ya Kamati iliwasilishwa na mwenyekiti wake, William Shelukindo.

  Aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Richmond, Harrison Mwakyembe (CCM) hakupata fursa ya kuhutubia bunge juu ya suala hili ingawa jina lake lilikuwa limetajwa miongoni mwa wachangiaji.
  Lakini ni Mwakyembe aliyewahi kunukuliwa akijigamba kuwa ana ushahidi mpya, aliokusanya ndani na nje ya nchi, unaohusu baadhi ya vigogo katika kashifa hiyo ambao sasa waweza kuibuliwa katika mkutano ujao.

  Baada ya piga nikupige ya wabunge wa pande mbili zinazokinzana juu ya suala hilo, serikali ililazimika kuondoa kile ilichoita, "Taarifa ya serikali kuhusu Richmond."
  Kabla ya hayo, Lowassa alikuwa ameanza juhudi za kujisafisha baada ya kuona kile kinachoitwa, "juhudi za kumsafisha" kugonga mwamba.

  Swahiba mmoja wa karibu na Lowassa aliliambia gazeti hili, kwamba Lowassa alitarajia mamkala za juu kumsafisha, lakini kila muda unavyozidi kutokomea ndivyo anavyogundua kuwa hicho alichokuwa akikitarajia kinashindikana.

  MwanaHALISI lina taarifa kwamba baada ya Lowassa kuona hawezi kusafishwa na mamlaka za juu, alikuwa ameamua kuunda mtandao wake wa kumsafisha. Hata hivyo, hatua ya sasa ya serikali kuondoa taarifa yake bungeni, inazidi kumweka katika wakati mgumu.

  Wakati hali katika Bunge ikiwa hivyo, serikali kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo imejitosa na kumtetea Rais Jakaya Kikwete, kwamba hahusiki na Richmond, kauli ambayo inazidi kumtenga Lowassa.

  Huo ulikuwa utetezi wa pili katika wiki mbili, ukifuatia ule wa Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais.

  Salva alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Rais Kikwete hahusiki na kashfa ya Richmond. Alikuwa akijibu taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vilivyosema Kikwete anahusika na kashfa ya Richmond.

  Kuna taarifa za awali kwamba suala la Richmond lilitawala kikao cha Kamati ya Bunge ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika Jumatano, 29 Julai katika ukumbi wa Msekwa.

  Mbunge Peter Selukamba alisimama kidete kuhakikisha suala la Richmond linazimwa.

  "Selukamba alisimama, huku akitoa macho na kuongea kama mwenye uhakika, 'Suala la Richmond limekwisha. Tunatafuta nini? Tayari serikali imetoa taarifa yake na maamuzi yake yalikuwa sahihi…,' ameeleza mtoa taarifa akimnukuu Selukamba.

  Hata hivyo, Selukamba hakufanikiwa kumaliza kilio chake cha kutetea watuhumiwa wa ufisadi, baada ya baadhi ya wabunge kumjia juu na kumtaka anyamaze. "Wewe nyamaza … nyamaza… wewe!" mjumbe mwingine amesimulia.

  Mjumbe huyo alisema baada ya zogo hilo kupoa, katika kikao ambacho kilikuwa chini ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, alisimama na kutaka wajumbe wasijadili suala la Richmond kwa ushabiki.
  "Hapa tunazungumza hoja. Hatuzungumzi kwa ushabiki wa kusema suala hili limekwisha. Tujadili mambo haya kisheria," Masilingi alinukuliwa na mtoa taarifa.

  Mbunge huyo wa Muleba Kusini alichambua taarifa ya serikali na kujenga hoja kwa misingi mikuu miwili. Kwanza, kwamba taarifa ya serikali imejaa mapungufu.

  "Huwezi kusema mtu hana makosa, kisha hapohapo ukasema tumemuonya," alisema. Lakini pili, Masilingi inaeleza kuwa "kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Bunge, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ina wajibu wa kuijadili taarifa ya serikali na kusema tunaikubali au hapana." Alisema, "Kama tunaikataa, basi tuonyeshe mapungufu yake ni yapi? Huu ndiyo wajibu wa Kamati za Bunge."

  Kauli ya Masilingi ilitokana na hoja ya awali iliyojengwa ndani ya kikao cha wabunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shelukindo na mjumbe wa Kamati hiyo, Cristopher ole Sendeka.

  Kwa nyakati tofauti Sendeka na Shelukindo walitaka Kamati yao "iachwe itimize wajibu wake."

  Taarifa ya serikali ya "kusafisha" watuhumiwa imezua maswali mengi. Serikali inadai imechunguza watuhumiwa wote, lakini wafuatiliaji wa taratibu za uchunguzi serikalini wanasema haikuzingatia taratibu.

  Kwa mujibu wa taratibu za serikali, sharti mtu anayechunguzwa asimamishwe kazi kwa muda au ahamishwe kutoka kituo chake cha kazi ili kupisha uchunguzi.

  Kwa mujibu wa suala hili la Richmond, wote wanaodaiwa kuchunguzwa walikuwa kazini na kwenye vituo vyao vya kazi; jambo ambalo linaweza kuwa limeathiri uchunguzi, kama kweli ulikuwepo.

  Taarifa za kuaminika zinasema, hata hivyo, kwamba Lowassa alikuwa amefanya vikao, siku tano kabla Bunge kupigilia msumari juhudi zake za kujisafisha kupitia mkono wa taarifa ya serikali.

  Katika kikao kimojawapo cha Dodoma, Lowassa alikutana na baadhi ya mawaziri, wabunge na waandishi wa habari ili kupanga mkakati.
  Inaelezwa kuwa kikao cha Lowassa na waandishi wa habari kilifanyika nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma. Kilihudhuriwa na mawaziri wawili na mbunge mmoja.
  Mtoa habari anawataja mawaziri waliohudhuria kuwa ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga. Mbunge aliyehudhuria ni Peter Selukamba.

  Mwandishi mmoja wa habari aliyehudhuria kikao hicho amedokezea gazeti hili, "Lowassa hakuzungumza sana; zaidi alitaka kujua kutoka kwetu. Alitaka kujua watu wanamuonaje na mara kadhaa aliponda taarifa za baadhi ya vyombo vya habari, hasa vile vinavyomuandama."

  Miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi kuhusu Richmond ambaye alipata fursa ya kuhutubia bunge, alikuwa Nazir Karamagi ambaye alitetea taarifa ya serikali ambayo baadaye iliondolewa bungeni.

  Lowassa na mbunge wa Igunga Rostam Aziz ambao wamekuwa wakisema kuwa hawajapata nafasi ya kujitetea, hawakuwa bungeni wakati wa mjadala huo mkali.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hawa watu akina EL na RA hawafi???....ah...
   
 11. Baridijr

  Baridijr Member

  #11
  Aug 8, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama bunge litashindwa kufikia maamuzi sahihi kwa hawa mafisadi lazima wananchi tuwaadhibu kama wahujumu uchumi, haiwezekani wabunge wanatumia hela nyingi za wapigakura halafu ukweli unapatikana watu hao hao wanawatetea wezi, hii nchi imeimekosa nini kwa Mungu hadi viongozi tunaowategemea kutetea taifa wanakuwa watetezi wa wezi.

  Kila nikitafakari amani yetu huwa najiuliza kama silaha zingekuwa zinauzwa madukani ingekuwaje
   
 12. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #12
  Aug 8, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 183
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kila nikitafakari amani yetu huwa najiuliza kama silaha zingekuwa zinauzwa madukani ingekuwaje
   
 13. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #13
  Aug 8, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 183
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Braza hawa jamaa kukosa uzalendo na machungu ya nchi hii na wananchi wake, kusikufanye nawe pia ukachoka na amani ya nchi hii.
  Wana mwisho hao
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waandishi , mbona hawajatajwa walio kuwepo maana wakijulikana inasiadia sana .Babile hakuwepo hapo ?
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kwani EL amesahau nini huko serikalini??si apumzike tu jamani??anachokitafuta atakipata....mahakamnindio kwake....
   
 16. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  a dirty game....politics...naamini Kikwete atachafuliwa vizuri sana,very soon..
   
 17. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mdau hapa sijakuelewa. Ninavyofahamu mimi ni kuwa kitu kisafi ndicho kinachoweza kucafuliwa, ila kitu chenye uchafu uliositirika ndio unaweza kudhihirishwa.

  Kwakuwa naamini JK sio safi, badi ni kuwa uchafu wake utawekwa wazi na wala sio kuchafuliwa!
   
 18. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  we tired kusikia haya majina kwenye mavyombo ya habari sasa, nyie waandishi mnawaandka kila kukicha na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa dhidi yao yaani ni kero tupu kwa kweli ni bora mkaandika habari za YANGA labda zitatusisimua kuliko kuendelea kuwaandika watu ambao serikali inawaogopa kuwachukulia hatua
   
 19. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Unajua hii serikali ya kikwete ni ya kisenge sana, hiyo ripoti ya Richmond imechukua zaidi ya mwaka kuifanyia kazi pamoja na kutumi amuda wote huo bado inakuja na utumbo usioeleweka. serikali iliagizwa kuchukua hatua siyo kwenda kuchunguza tena hili nalo pinda anahitaji tumkalishe chini tumweleweshe? majibu ya serikali yanasikitisha sana sijui wanawachukuliaje watanzania. kama swala la richimond limechukua zaidi ya mwaka je hayo mengine yatachukua mda gani. Ipo siku.
   
 20. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwenye proffessional ya accounting kampuni inapochelewa kutoa report ya mwisho wa mwaka ni ishara kuwa wanapika report ipendeze kuliko hali halisi, kwahiyo kuchelewa kwa serikali na kuja na report ya kipuuzi (nasema ya kipuuzi maana siamini kama pinda alifikiria consequences za kuja na report ya aina hiyo kwenye credibility yake na serikali) maana yake walikuwa wanapika kitu kizuri ambacho akiwaumiza washirika wao na kusababisha mfuko wao wa mabaya kufumuka zaidi hasa kwa mkuu wa kaya.

  Natamani EL apewe jukwaa lakini si kwa jinsi hii, kwani hapo tutakuwa hatujafanikiwa kujua ukweli wa RD, apewe jukwaa bila makubaliano na mkuu wa kaya ili amwage sumu yake tujue nani kinara wa RD

  Hii ni report ya kijinga kabisa, au negotiation na wausika zilishindikana, wangewajibisha na kuwapa mafao yao wakakaa pembeni badala ya kuja na kitu ambcho wanajua watanzania hawatakubali, Upishi wao naona ulikuwa mgumu kwani nahisi Hossea na wenzake walikataa kuwa kama EL aliyedangaywa kuwa atasafishwa na kurudi tena kwenye siasa akakubali na sasa anajuta kilichomtuma

  Kabla ya kuchukua hatua unatakiwa kutathmini kama kweli unachofanya ni sahihi au ndio unapotea hii ni kwa serikali na EL.


  Kumbukeni: DESITINY IS NOT LUCK BUT DEPEND ON DECISION YOU MAKE TODAY WHICH OBVIOUS WILL AFFECT YOUR FUTURE
   
Loading...