Lowassa, Rostam kumzima Kikwete; CCM hatihati kuvunjika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Rostam kumzima Kikwete; CCM hatihati kuvunjika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h][HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 June 2011

  Waahidi kumlipua vikaoniCCM hatihati kuvunjika

  [​IMG]  HATUA yoyote ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kuwafukuza ndani ya Chama Chaa Mapinduzi (CCM) wanaowaita “watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini,” yaweza kumuumiza mwenyewe, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa kutoka ndani ya serikali na chama hicho zinasema watuhumiwa hao ambao Kikwete wiki mbili zilizopita waliitwa mbele ya makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na kuhojiwa, wamejipanga kuzuia mpango huo na ikibidi watamgeuzia kibao kwa hoja kuwa yeye “ndiye tatizo kuu” katika chama na “chanzo cha serikali kuzorota.”

  Wanaotakiwa kuondolewa kwenye uongozi ndani ya chama kwa hoja kwamba “wamechafua sura” ya chama hicho mbele ya wanachama na wananchi, ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge.

  Lowassa anatuhumiwa kufanya upendeleo katika kuipa zabuni ya kuzalisha umeme kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (LLC), ambayo imethibitika kuwa haikuwa na uwezo, sifa wala fedha za kufanya kazi iliyoomba.

  Rostam ametajwa mara kadhaa katika ufanikishaji wa mikataba tata ya kufua umeme ya Richmond/Dowans, pamoja na wizi wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd., katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) iliyoko Benki Kuu ya Taifa (BoT).

  Chenge, aliyelazimika kujiuzulu uwaziri, anatuhumiwa kuingiza nchi katika mikataba mbalimbali ya madini, ununuzi wa ndege ya rais na kujipatia mlungula katika ununuzi wa rada kama ilivyothibitishwa na shirika la uchunguzi wa makosa makubwa la Uingereza (SFO).

  Mtoa habari wa gazeti hili ambaye yuko karibu na viongozi hao watatu anasema, “Lowassa, Rostam na Chenge wameapa kutoondoka CCM.” Anasema wameapa kukabiliana na yeyote anayetaka kuwaondoa.
  Anasema, “Wewe unajua kwamba Rostam ametoa fedha nyingi sana kwa chama hiki. Sasa anasema wanaotaka aondoke lazima waseme aende wapi. Anasema lolote na liwe, lakini hakuna atakayejiuzulu wala atakayekubali kufukuzwa.”

  Mtoa taarifa hizi ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya Rais Kikwete.

  Kuvuja kwa taarifa kwamba Lowassa, Rostam na Chenge wameapa “kufa na Kikwete” iwapo ataendelea na kinachoitwa msimamo wake wa kutaka kuwaondoa ndani ya uongozi wa juu wa CCM, kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa watuhumiwa hao wa ufisadi walikutana kwa faragha na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Msekwa na kugoma kujiuzulu.

  Katika mkutano huo, Rostam alisisitiza kuwa hawezi kujiuzulu kwa kuwa hana hatia. Hakukuwa na habari yoyote kuhusiana na mazungumzo kati ya Chenge na Msekwa.

  Bali Lowassa alihoji sababu ya kutakiwa kujiuzulu na baada ya kuelezwa kuwa ni tuhuma za mkataba tata wa Richmond, haraka alijibu, “Kuhusu Richmond, ukweli unafahamika… Rais anafahamu hilo na kila mmoja anajua hilo.”

  Mtoa taarifa anasema Lowassa katika kuhakikisha anabaki ndani ya chama hicho amepanga kueleza mkutano wa NEC, hatua kwa hatua, jinsi kampuni ya Richmond na Dowans zilivyoingia nchini na jinsi zilivyopewa mkataba.

  Inadaiwa kuwa hatua hiyo ya Lowassa inatokana na Kikwete kuvunja kinachoitwa “makubaliano ya awali” ya kumsafisha kuhusiana na sakata hilo.

  “Unajua Kikwete na Lowassa walikuwa na makubaliano, kwamba yeye ajiuzulu (uwaziri mkuu Februari 2008) ili kulinda serikali na chama. Kisha wakakubaliana kuwa Kikwete atafanya kazi ya kumsafisha kupitia chama na Bunge.

  “Lakini Kikwete hakutekeleza makubaliano hayo kwa kisingizio kuwa ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa. Sasa yeye ameamua kujisafisha mwenyewe,” taarifa zinaeleza.

  Bali si siri kwamba Rais Kikwete, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, alifika Monduli, katika jimbo la Lowassa, kumshika mkono, kuuinua na kumtangaza mkutanoni kuwa ni kiongozi shupavu anayestahili kupigiwa kura.

  Lowassa anasemekana kutoridhishwa na kauli hiyo katika harakati zake za kurejea ulingo wa juu wa siasa nchini.

  Katika mkutano kati ya Lowassa na Msekwa, habari zilinukuu viongozi hao, kila mmoja akishupalia mwenzake.

  Wakati imeripotiwa Msekwa akisema, “Lowassa acha mbio za urais,” Lowassa yeye alijibu mapigo kwa kusema, “Lini nimetangaza kugombea urais? Je, (kama nilitangaza) haramu kufanya hivyo, au kuna mliowaandaa?”

  Imeelezwa kuwa Msekwa alikana kuwapo mtu aliyeandaliwa, lakini akasema, “ndivyo wanavyosema, kwamba wewe unataka urais,” na kwamba “…haya mambo ya urais yatatuvuruga.”

  Wakati Lowassa akipanga kujisafisha kwenye NEC, taarifa zinasema Rais Kikwete amepanga kuitumia Kamati Kuu (CC), “kuwafukuza watuhumiwa” ili kujenga sura ya uwajibikaji.

  Ni ndani ya kikao hicho maalum cha CC, ambamo inadaiwa Rais Kikwete amepanga kupeleka hoja ya kuwafukuza watuhumiwa hao, halafu kuijulisha NEC kwa njia ya taarifa.

  Inadaiwa mara hoja hiyo itakapoingia NEC, Kikwete atawaeleza wajumbe kuwa CC imetekeleza maagizo ya NEC iliyopita ambayo inadaiwa iliagiza kufukuzwa chama watuhumiwa wote wa ufisadi.

  Hata hivyo, kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ndani ya CCM amesema, iwapo Kikwete ataamua kutumia njia hiyo, basi ajiandae kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa kundi la Lowassa na wafuasi wake; jambo ambalo linaweza kusababisha kugeuziwa kibao na kuishia kujadiliwa utendaji wake ndani ya chama na serikali.

  “Hapo ndipo hata ile hoja ya kutenganisha kofia mbili inaweza kuibuka. Unajua ndani ya CCM kuna viongozi wengi wanaomuona Kikwete ni dhaifu na hivyo wanataka kutenganisha kofia ya mwenyekiti wa chama na rais wa nchi. Sasa akifanya mchezo hapa kunaweza kutokea makubwa,” ameeleza mmoja wa viongozi wa CCM ambaye ni mwanasheria.

  Anasema, “Kamati Kuu ya chama haina uwezo wa kuwafukuza wale jamaa. Ni lazima kama wanataka kuwafukuza, hoja iletwe NEC, kwani hiyo ndiyo inayofanya kazi kwa idhini ya mkutano mkuu. Sasa mle NEC, hawa jamaa wako vizuri. Kikwete akileta hoja hiyo, anaweza kujikuta anaingia katika mgogoro na pengine chama kugawanyika.”

  Nguvu ya Lowassa inatarajiwa kuegemea viongozi wastaafu, hasa Rais Benjamin Mkapa ambaye wachambuzi wa mambo wanamchukulia kuwa hawezi kukubaliana na mpango wa Rais Kikwete wa kufukuza wenzake katika chama.

  Mkapa ambaye amejitosa katika kesi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, anachukuliwa na wengi kuwa hafurahishwi na hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama na hata serikali chini ya Rais Kikwete.
  Kwa mujibu wa watu waliokaribu na viongozi wa juu CCM, hoja ya kumfukuza Lowassa na wenzake tayari imeiva na kwamba azimio la kuwafukuza litafikishwa CC “kwa ajili ya kubarikiwa tu.”
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona EPA haizungumziwi katika hizo tuhuma?
   
 3. i

  issenye JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Lowassa, Rostam kumzima Kikwete

  Waahidi kumlipua vikaoni
  CCM hatihati kuvunjika

  HATUA yoyote ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kuwafukuza ndani ya Chama Chaa Mapinduzi (CCM) wanaowaita “watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini,” yaweza kumuumiza mwenyewe, MwanaHALISI limeelezwa.

 4. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  lini hiko kikao cha cc?
   
 5. M

  Masuke JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Imetajwa rudia kusoma utaiona vizuri.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm nawaogopa kwakua wanafitiniana wenyewe kwa wenyewe, hata mwenyekiti wao alisema inafikia pahala hata vinywaji hawaachiani, ccm ni sawa na simba mla watu
  [​IMG]
   
 7. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao mafisadi warudishe hizo hela walizokwapua ili zitumike kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  i can't wait to watch this movie
  kweli fitina mbaya .
  pamoja na udokozi wa EL sidhani kama move ya jk ni kwa manufaa ya taifa
  kama sio haraka za mzee rukusa kumuingiza ikulu mwanaye
  sisi tunataka tanzania safi sio ya wakwapuwaji
   
 9. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa ccm!
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani Rostam na Lowasa wakitoka CCM, si ndio mwisho wao, wao ndo waliosimamia azimio la Zanzibar barabra. halafu pesa za EPA atakwenda kuchukua nani? na kanga, fulana, mabango na kofia watapata wapi. Una hatari wewe RA na EL? hatoki mtu. na wote wanaowasumbua shauri yao, wamuulize Chitanda na Azam.
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Siku 90 alizotoa Nepi zimekwisha hakuna gamba lolote lililotoka mwilini mwa CCM, sasa tuone atakwenda kudanganya nini kwenye mikutano yake?
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  Kujivua gamba si mchezo! lazima chama kisambaratike na gamba bado liko mwilini. Ngoja tuangalie sinema hii ili tujue hatima yake.
   
 13. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  magambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hivi siku tisini bado??
   
 15. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  fanyeni kweli basi.tumechoka na maneno maneno yenu..kila siku mara lowasa hili mara mapacha watatu,vipi wakuu mnataka kutuzuga wakati mnajua wazi hamna ubavu wa kufanya hayo mnayoyanadi??
   
 16. NAIPENDA TANZAN

  NAIPENDA TANZAN Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo patamu kwelikweli. Sasa naona Tanzania mpya iko mikononi mwa EDWARD LOWASSA, CHENGE NA ROSTAM. Kwa hili namaanisha kuwa hawa wenye uwezo wa kuisambaratisha CCM ndio watakao ikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi.
  Kama shetani anasikia sala za binadamu na kuzifanyia kazi, sasa ni wakati muafaka.
   
 17. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakimtoa Lowassa kwa mabavu (Kitu ambacho SIDHANI KAMA KINAWEZEKANA) basi Kikwete atatumia muda wote and I MEAN IT uliobaki kumaliza term yake kuhakikisha yupo safe from Lowassa and co.

  Kumuondoa Lowassa ni high risk kwa Kikwete, serikali na hata chama. Akikataa kuondoka Lowassa by choice, Kikwete hana cha kufanya.
  P.S. Lowassa alishakubali kujiuzulu ili kukinusuru chama, serikali na JK kwa ahadi kwamba angesafishwa na JK, na hiyo ahadi haikutekelezwa, what makes you think he will resign this time around by choice ? Huu moto sidhani kama utakuwa na maji ya kuuzima.
   
 18. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  I said it again ...and repeat it now...!

  Jk is feable and cant make it happen!!
   
 19. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  ​Hiyo ni trela, movie yenyewe bado!
   
 20. M

  MPG JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anguko la CCM limetimia,dhuruma walioifanya kwa miaka mingi sasa imewaguka hiyo ni laana yao kutuka kwa Muumba
   
Loading...