Lowassa: Ninamuunga Mkono Kenyatta na nipo tayari kutoa msaada wakati wowote

Ndugu yake na uburu omolo ni mkazi wa chato, wakenya mkikosea hesabu itakuwa kagaraimagu empire.
 
Odinga alipompigia tu kampeni Magufuli akamchefue Lowassa. Nasikia Odinga na rafiki wa Magufuli. Tunamsapoti Kenyatta. Odinga abaki na Magufuli wake.
 
Wageni kutoka Jamhuri ya Kenya wakiongozwa na wabunge 13, Madiwani, Machifu na Maleigwanan kutoka Kenya mchana wa leo wamemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake kijijini Ngarash, jimbo la Monduli wakiongozana na vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali kutoka Wilaya mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Manyara.

ad4201fe7625d5d7c37da96b853f43c5.jpg

Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA na waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa leo ameuambia ujumbe wa wabunge kutoka Kenya kuwa anamuunga mkono mgombea Urais ambaye pia ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

"Niseme hivi, sisi watu wa Monduli tumeamua kumuunga mkono Rais Kenyatta.

Tuko tayari kumsaidia pale wakati utakapofika, tunafanya hivyo kwa sababu tunampenda na yeye pia anatupenda. Tunaamini yeye pekee ndiye mtu sahihi ambae anaweza kuendeleza mshikamano na umoja uliopo baina ya mataifa yetu haya mawili"

Edward Lowassa
27 April 2017
Monduli, Arusha.
hao watu wa monduliwalikaa chini lini wakaamua?
 
Kimoyomoyo

Naoma unaniquote kujifurahisha na kujibu huwezi. Pia ujue tupo tunaoishi na hatuchukii binadamu kwa ajili ya hasira na wivu au tamaaa kama mlizojaza nyie wengi. Tukutane siku ya kushangilia

2020 ya Magufuli.
 
ndio maana mbowe mmachame mwenzie aliamua kumpa ugombea uraisi sasa naanza kuelewa kwa nini magazeti ya Mengi MA ITV walimbeba Sana Lowasa aiseee kumbe Lowasa mchaga alikulia umasaini eeeeeeee.Ndio maana hana tabia za kimasai Masai sio mafisadi wala tuhuma za ufisadi huwa hawana ufisadi si hulka ya wamasai.Lakini kama ni mchaga naweza amini aiseee
ILA TBC ilipo mbeba magufuli ilikuwa sawa,viwavi ni viwavi tu mkiona post ya Lowassa mavi yanawabana
 
Ufisadi wake unaweza kuutolea ushahidi ukiitwa mahakamani kweli? usiwe mtu wa kukurupuka kuropoka! Ulizaliwa mwaka gani? nahisi kama ni miaka baada ya uzazi wa mpango kuanza basi ni condom ilipasuka kwa bahati mbaya ndio maana upo duniani.
Kwahiyo ile list of shame ni ya uongo?? na walio iandaa na kuisaini hawafai tena?? au walikuwa matapeli??? toa majibu haraka saaanaa
 
Baada ya kumaliza mambo ya kufariji jamii ya wafiwa, Waziri Mkuu mstaafu na Kiongozi wa CHADEMA Mh. Edward Lowassa ametoa tamko rasmi kwamba chama chake KINAUNGA mkono kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili ya Mh. Rais Uhuru Kenyatta kuwa rais wa Kenya tena.

Katika mahojiano na gazeti moja maarufu nchini Kenya "the Nation", Lowassa alisema Kenyatta ndiye anayeweza kuongoza nchi na wala si Raila Odinga. Maana Raila anaungwa mkono na rais Magufuli.

Wachambuzi wa kisiasa wanaunganisha na kauli ya Mh. Mbowe aliyokuwa amewahi kuitoa juzijuzi kuwa, katika UCHAGUZI wa mwaka 2013 waliimuunga mkono RAILA.

Lakini katika UCHAGUZI wa Tanzania wa mwaka 2015 Raila aliwageuka na KUMUUNGA MKONO rais wa sasa wa Tanzania Mh. John Joseph Pombe Magufuli.
Kwa hivyo nao wameamua KULIPIZA KISASI.

UCHAGUZI wa mwaka huu nchini Kenya umeleta mtafaruku wa Kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Wakati Kenya inapozidi kudai kuwa Raila ameruhusiwa kuweka mitambo ya Tallying center/Kituo cha Kujumlisha matokeo ya uchaguzi nchini Tanzania na kudai mara yako sijui kiko wapi.

Mara sasa kinadaiwa kiko nje kidogo ya Dar. (Huu ni UVUMI usio na msingi hata kidogo.) ambao hautasaidia katika kujenga uhusiano bora wa ujirani mwema.

Kutokana na madai hayo Serikali ya Tanzania kupitia BALOZI wake wa mambo ya nje na Afrika Mashariki Mh MAHIGA.

Mwanzoni mwa mwezi huu ilibidi ATOE TAMKO rasmi la KISERIKALI kuwa Tanzania HAINA kituo kama hicho nchini Tanzania kama jinsi ambavyo Kenya inavyodai.

Tamko la Lowassa la kuunga mkono Uhuru Kenyatta kumeongeza sintofahamu katika UHUSIANO kati ya nchi hizi mbili hasa BAADA YA UCHAGUZI!

Uhusiano huu ambao otherwise ulikuwa umeanza kuwa Mzuri.
Ni heri basi Lowassa baada ya Mazishi angerudi nyumbani badala ya kutuchonganisha na jirani zetu kwa KUHOJIWA NA MAGAZETI na kutoa KAULI TATA!
 
Ni vema kuonesha msimamo kama chama.Ila ikulu inamuunga mkono Raila

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Watajiju hao wakenya wanao kubali uchaguzi wao kuingiliwa na watu kutoka nje

Sisi Tanzania mwaka 2020 hatutaki shobo za namna hiyo

Uhuru Kenyata pokea tu misaada ya Edward Lowassa ilimradi tu 2020 usitie pua yako
 
Ni vema kuonesha msimamo kama chama.Ila ikulu inamuunga mkono Raila

Post sent using JamiiForums mobile app
Chadema kuna mtafaruku mkubwa hivi chama Kama chama kilikaa kikao lini cha kutoa matamko Ya kumuunga mkono Kenyatta na kumtambua lowasa Kama mgombea uraisi 2020? Niwaonye chadema siasa za kenya ngumu Kama wamehama kambi ya odinga na kwenda kwa Kenyatta wajue wametangaza vita na wajaluo wote wa kenya na Tanzania chadema majimbo waliko wajaluo watayapoteza yote na pia wakienda kenya kampeni wawe makini na usalama wao
 
Ni vema kuonesha msimamo kama chama.Ila ikulu inamuunga mkono Raila

Post sent using JamiiForums mobile app
SIDHANI kama kuna TAMKO rasmi la rais Magufuli, ama Magufuli kama mtu binafsi la kumuunga mkono RAILA Odinga. Labda ni urafiki ndo waleta dhana.
 
Back
Top Bottom