Lowassa: Nimechoka kuzushiwa

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Lowassa: Nimechoka kuzushiwa
• Mwanaye ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha

na Mwandishi wetu


WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ameeleza kushangazwa na mwenendo wa kisiasa wa siku za hivi karibuni ambao unaliingiza jina lake katika matukio makubwa ya kisiasa yanayotokea.
Mbali ya kueleza mshangao wake huo, Lowassa alikwenda mbele zaidi na kusema alikuwa amefikia hatua ya kuchoshwa na aina ya siasa zinazomhusisha na mambo yasiyo na ukweli wowote.
“Nimechoka kukaa kimya kila mara zinapotengenezwa habari za uongo juu yangu. Imefika mahali sasa nimeamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale ambao kwa makusudi na kwa nia mbaya wanafinyanga uzushi dhidi yangu na wakati mwingine dhidi ya familia yangu,” alisema Lowassa aliyezungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana.
Akitoa mfano, Lowassa ambaye alitafutwa ili kutoa maoni yake kuhusu muundo wa baraza jipya la mawaziri lililotangazwa hivi karibuni, alieleza kushangazwa na uamuzi wa baadhi ya watu kufikia hatua ya kumtuhumu kwamba alikuwa akishinikiza ateuliwe katika nafasi kadhaa za uwaziri jambo ambalo halina ukweli wowote.
“Rais anaunda baraza la mawaziri kwa utashi wake na si kwa kushinikizwa na mtu yeyote. Jambo la kushangaza imefikia watu wanasema uongo wa wazi kwamba eti Lowassa alikuwa akishinikiza na wengine wakafikia hatua ya kudai kulikuwa na msukumo mkubwa wa kutaka niteuliwe. Huu wote ni uzushi,” alisema Lowassa.
Alisema ni jambo la ajabu kwamba jina lake ndilo linaloonekana kuwa katikati ya mjadala wa uteuzi huo wakati kila mmoja akijua kuwa wako mawaziri wakuu wastaafu wengine ambao wangeweza kuteuliwa katika nafasi za ubunge na uwaziri ambao hawakuteuliwa ingawa majina yao hayatajwi.
Ingawa Lowassa hakutaja jina la mtu yeyote, mawaziri wakuu wastaafu ambao wapo ni Frederick Sumaye, John Malecela, Joseph Warioba, Cleopa Msuya na Salim Ahmed Salim.
Ukimuacha Malecela ambaye alionyesha dhamira ya kuendelea kuwa bungeni kabla ya kushindwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mawaziri wakuu wastaafu wengine wote wako nje ya wigo wa siasa za mikikimikiki.
Kwa sababu hiyo, mwanasiasa huyo alieleza kusikitishwa na hatua ya watu aliowaita wachimvi waliofikia hatua ya kukielezea kitendo cha rais kutomteua katika nafasi yoyote ya uwaziri kuwa ni cha kumtosa kisiasa.
“Mimi ni mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, bado ninazo fursa nyingi za kuendelea kutoa mchango wangu wa kisiasa kwa chama changu na kwa taifa langu kwa njia nyingi.
Nafasi za uongozi nilizonazo zimetokana na ridhaa ya chama changu. Haiingii akilini kusema nimetoswa au nimefikia ukomo wa kisiasa,” alisema Lowassa kwa masikitiko.
Alisema iwapo Kikwete au CCM wangekuwa wamemtosa kisiasa, basi jina lake lisingeweza kupitishwa kugombea ubunge, kwani rais ndiye mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.
Mbali ya hilo, Lowassa alisema, watu wasiomtakia mema, ambao hata hivyo hakuwataja, wamefikia hatua ya kuanza kuipaka matope hata familia yake katika mambo ambayo si ya kweli.
Lowassa alikuwa akizungumzia habari zilizomhusisha mtoto wake Frederick Lowassa katika tuhuma za kuchunguzwa na taasisi za ndani ya nchi na zile za nchini Uingereza kwa madai ya kusafirisha fedha nje ya nchi katika mazingira yenye utata.
Habari hizo zilizoandikwa katika gazeti moja linalochapishwa mara moja kwa wiki, zilimhusisha Frederick na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban shilingi bilioni moja) ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.
“Habari hizo zinazomhusu Frederick na ambazo zililitaja pia jina langu hazina ukweli wowote. Nimechoka kuzushiwa na kushambuliwa kwa mambo ambayo si ya kweli. Nimekuwa kimya na sasa wameanza kuichafua hata familia yangu. “Nimewasiliana na Frederick mwenyewe ambaye amenihakikishia kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua za kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya kimaadili na kisheria kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na mahakamani ili kulisafisha jina lake,” alisema Lowassa.


Ujumbe: Ukiwa mashuhuri kuwapaka matope wenzio nawe ukipakwa matope uwe jasiri kuvumilia. Nguruwe pita sina mkuki. hahahahaha
 
Nanukuu tu.... "Haiingii akilini kusema nimetoswa au nimefikia ukomo wa kisiasa,"....yaelekea hajakata tamaa mang'ati huyu
 
Nanukuu tu.... "Haiingii akilini kusema nimetoswa au nimefikia ukomo wa kisiasa,"....yaelekea hajakata tamaa mang'ati huyu

Ni kweli kwamba Lowasa hajakata tamaa na ana roho ya paka.
Hakati tamaa kirahisi hata siku moja.
Tutarajie mengi kutoka kwake kwani hajali kuchafuka kwake.
 
Alipotajwa kwenye orodha ya mafisadi hakwenda mahakamani, na nina hakika hata sasa hakuna kati yake au mtoto wake anayeweza kukanyaga mahakamani.
 
Haahaaaaaaa walikuwa wakichafua wenzio sasa his turn anang'aka nini? kwanzani kuchafuliwa huku au kufichuliwa ....! tutajua
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa]

Hii ndo shida ya makanjanja wa bongo na wahariri wao, hivi mtu aliye jiuzuru kwa makosa yake ni Mstaafu? Kama sikosei tunao mawaziri wakuu wastaafu watano tu ambao ni SAS, Warioba, Malecela, Msuya na Sumaye, huyu Laiboni ni mharifu tu wala siyo mstaafu!
 
Lowassa: Nimechoka kuzushiwa
• Mwanaye ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha

na Mwandishi wetu


......"Habari hizo zinazomhusu Frederick na ambazo zililitaja pia jina langu hazina ukweli wowote. Nimechoka kuzushiwa na kushambuliwa kwa mambo ambayo si ya kweli. Nimekuwa kimya na sasa wameanza kuichafua hata familia yangu. "Nimewasiliana na Frederick mwenyewe ambaye amenihakikishia kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua za kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya kimaadili na kisheria kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na mahakamani ili kulisafisha jina lake," alisema Lowassa.

Du! Kweli huyo ndo Edy Lowasa,

Can he account for his abundant wealth? Where did he got the capital - which grows every day kama sio wizi wa mali ya umma?

Can he come out clean with a Tax Clearence Certificate?

Hivi huyu bwana anafikiri akitishia kwenda mahakamni ataachwa aendelee kufanya madudu? Ni vizuri saana wapelelezi makini wameanza kuangalia source za mapesa ambayo anaenda kununulia nyumba Ulaya, kwa nini asijenge kwao Monduli?

Alishundwa kumshtaki Dr. Slaa alipomtaja Mwembe Yanga kweamba ni fisadi ataweza hili lenye ushahidi? Ngoja tusubiri na tuone.
 
Lowassa: Nimechoka kuzushiwa
• Mwanaye ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha

na Mwandishi wetu


WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ameeleza kushangazwa na mwenendo wa kisiasa wa siku za hivi karibuni ambao unaliingiza jina lake katika matukio makubwa ya kisiasa yanayotokea.

Waandishi wengine wananitia kichefuchefu na kwa hakika wanaidhalilisha fani /taaluma yao aidha ni wapambe wa kimya kimya.
Unawezaje kumwita Mstaafu??.Waandishi na waomba msitu wekee historia ya uongo huyu bwana alijiuzulu na tena kwa tuhuma nzito.
 
Mara baada ya Tume (NEC) kutangaza matokeo ya Uchaguzi mkuu mwaka huu Mh. EL, alimkejeli DR. SLAA kwa kusema......." hajui siasa za Tanzania....."

Swali kwa Mh. EL, je, yeye anayezijua siasa za Tanzania analalamika nini????????
 
Hii ndo shida ya makanjanja wa bongo na wahariri wao, hivi mtu aliye jiuzuru kwa makosa yake ni Mstaafu? Kama sikosei tunao mawaziri wakuu wastaafu wanne tu ambao ni SAS, Warioba, Malecela, Msuya na Sumaye, huyu Laiboni ni mharifu tu wala siyo mstaafu!

Nashawishika kuwa hawa pekee ndio Mawaziri Wakuu Wastaafu, waliacha kugombea ubunge wakati wakiwa Mawaziri Wakuu na hivyo kukiacha cheo cha Uwaziri Mkuu,hao wengine ni Mawaziri Wakuu wa Zamani unless tuwaite Waliostaafishwa kwa manufaa ya umma.
 
Namshauri this time awahi kukimbilia mahakamani. Kutishia nyau hakuna msaada wowote.
 
Edward Lowasa si waziri Mkuu mstaafu tu
Edward Lowasa ni Waziri Mkuu mstaafu kwa maslahi ya Umma/Taifa.

Akae akijua Hilo
 
Hii ndo shida ya makanjanja wa bongo na wahariri wao, hivi mtu aliye jiuzuru kwa makosa yake ni Mstaafu? Kama sikosei tunao mawaziri wakuu wastaafu wanne tu ambao ni SAS, malecela, Msuya na Sumaye, huyu Laiboni ni mharifu tu wala siyo mstaafu!

Umemsahau Judge Warioba
 
To @ axn there is an = and opp rxn! Atambue kuwa yanayomsibu yeye na jk ni sehemu ya malipo ya dhambi walizowatendea kina SAS na wagombea wengine wa Urais. Mwambie nasi tumechoshwa na kuchoshwa kwake. Tunataka hasiichie kusema amechoka tu, aende mahakamani tena akianza na Dr. Slaa
 
Maskini mungu amsaidie ila tatizo akienda mahakamani siri nyingi zitaibuka anyway wacha tusubiri tuone.
 
Wakuu

Lets be fair and grown ups!!!

There were too many unnecessary rumors na hasa yale ya kusema kangangania wizara nne, sijui atakua PM etc

We cant build our country through rumors
 
Back
Top Bottom