Lowassa ni next level na anaijua siasa ya Tanzania

Sasa kama wamesema nchi haina njaa hayo mahindi wanayotaka kuyasambaza wanawapelekea ng'ombe kule Chato??
hakuna njaa..hivi wewe unaijua njaa au unasema tu sababu watu fulani wamesema .....njaa nenda somalia.nenda Ethiopia utajua kweli watu hao wana njaa.
Ebu acheni siasa
 
Mfungeni si mna jeshi,polisi,wanasheri,mahakimu,magereza yote yenu mkituimbia wimbo wa fisadi nyangumi au papa wakati uwezo wa kumkamata mnao watu wenye akili hawawezi kukuelewa labda wale kati 1.4 ukiwemo na wewe uliyeandika
Safiiii
 
Huyu mtu ni muhimu sana kwa watanzania wa Leo...hasa katika uhitaji wa mabadiliko

Kweli huyu mtu muhimu, lakini wale wanaomfuata nyuma yake hawajijui umuhimu wao.
Wangekuwa wanajijua umuhimu wao, baada yule Mzee kwenda kule kwenye maafa (sijui kuwapa pole sijui kuwasanifu) wao wasingejitokeza, kila mtu angetulia nyumbani kwake kumuonesha umuhimu wao.
Matokeo yake uliona, walijitokeza kwa wingi na bado wakamwagiwa shombo kwa mara nyingine.
Usishangae kile chama kikapata kura nyingi zaidi 2020 kwa sababu wanaopiga kura wanapoenda kwenye Sanduku hawajui wanaenda kufanya nini.
Watanzania pasua kichwa.....
Kile chama tawala tu ndio kinawajua watanzania ni nani.
Mtu mwingine tofauti huwezi kumjua mtanzania.
 
Post hii imeletwa na mtu anayemjua sana Lowassa inawezekana akawa na lengo Naya kwa Lowassa lkn ukweli Utabaki kuwa ukweli.
 
Baba yetu kutoka monduli.jina lako ni balaa,ufalme wako usiwepo duniani, mapenzi yako yashindwe ,utupe leo yote uliyotuibia na riba juu. Kwa kuwa tamaa yako ni kubwa mno.Eeemen!
 
Hata polisi wanajua kuwa Lowasa ndie kiongozi bora mfano wameonesha juzi huko Geita, mwingine aliongea weee mpaka akapanda juu ya gari akaongea na kiligha lakini polisi walimpotezea tu, Lowasa kupita tu kabla hata hajaongea wakamchukua kumuongezea ulinzi. Lowasa ni zaidi ya kiongozi.
 
hakuna njaa..hivi wewe unaijua njaa au unasema tu sababu watu fulani wamesema .....njaa nenda somalia.nenda Ethiopia utajua kweli watu hao wana njaa.
Ebu acheni siasa
Mkuu umejitahidi sana kutetea lakini nadhani umesahau kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha. hizo njaa za Somalia, Ethiopia hazikuanza kwa ghafla na kwa kukurupuka bali zilianza taratibu, pia naomba unisaidie tabia na sura ya nchi kwa nchi tajwa hapo juu kuwa zina hali gani ukilinganisha na nchi yetu. Kingine bila ya kusahau kuwa inabidi ujikune unapofikia kwani ukitumia mti utaumia kila mmoja anayasemea magumu kwa yale yaliyomkuta.
Mfano, mtoto wa drs la saba huwa anahofia mtihani wa Taifa kutokana na ugumu wake ambao yeye anauhisi, hivyo huwezi kumkanushia madai yake eti kwa sababu wewe umeufanya mtihani wa kidato cha sita na kujiona wewe una haki zaidi ya kuelezea ugumu wa mtihani wako. Kila mmoja ana haki ya kuelezea matatizo na changamoto zinazomkabili yeye au watu wake anao wawakilisha. Nadhani tungekubaliana tu kuwa kuna watu kweli wana njaa(hao huwaza mwaka jana mvua zilikuwa nafuu kiasi, hivyo nilipata kiasi fulani cha mahindi lakini kwa mvua hizi za mwaka huu hata hii akiba hainitoshelezi,mwanangu ni mgonjwa na hospitali siku hizi cheti tu elfu kumi dawa zenyewe nikanunue mwenyewe sijui na vipimo itakuwaje huko bora tu nimchemshie majani kiganja kimoja ya mwarobaini....vipi watu km hao wewe huwajui?? na kuna watu kweli wao hawaijui njaa (hao huwaza kesho nitanunua gari.nyumba au hata boti gani,, we watu km hao huwajui??),na km watu km hao wote huwajui basi wewe utakuwa raia wa Marekani na siyo TZ au utakuwa una uraia pacha wa Ethiopia na wa huko Somalia.. mifano kwa hili ipo mingi tu ila yapaswa kuangaaliwa wengi ni wepi kati yao.
SAMAHANI SANA MKUU KAMA NIMEKUKWAZA LAKINI HAYA NI MAONI YANGU TU...
 
Uzuri ni kwamba wapiga dili wote wamehamia jamii forums. Wanapata ahueni kwa kutoka hasira zao. Magufuli ameshasema habadiliki hatatoa mwanya wowote kwa wizi tena. Kila anayetumbuliwa anahamjlisha mashambulizi jamiiforums.
Magu kaza Uzi hivyo hivyo mwisho hata hela ya kununua MB itaisha. Kwa sasa bado wanamalizia zile walizoiba tra na kwingineko. Jamiiforums haina maana tena siku hizi hamna tena critical analysis Bali kutetea wahuni tu akina mbowe wanaiibia nhc.
Badilikeni jamani magu hatabadilika hata mpige kelele namna gani. Mlipiga kelele ya sukari akaisolve faster sasa hii ya njaa ikiisha sijui itakuwaje.
Mi naamini kabisa chadema na ukawa mjiandae kupokea makapi yaliyotumbuliwa. Uzuri wananchi wengi wanamkubali magu sema hawaji kupiga kelele humu
Jamaa unaakili sana tena we mzalendo sana.

Nasikia mkuu alisolve tatizo la sukari bei ikashuka inauzwa Buku sikuizi.
 
Eti ''Lowassa anaweza kubadili njano kuwa nyekundu''. Unachekesha kweli.

Kama anaweza kubadili njano kuwa nyekundu, mbona hakuweza kuingia Ikulu? Au njano kuwa nyekundu haziwezi kutumika kwenye kura ili aingie Ikulu.

Tanzania kuna vituko.
Wewe acha kuweweseka. Mbona mnasambaza Chakula ilhali hakuna njaa. Wewe hajabadili kitu. Msemajiukweli gani mwongo?
 
Huyu mtu ni muhimu sana kwa watanzania wa Leo...hasa katika uhitaji wa mabadiliko
Acha bangi wewe! Lowassa alete mabadiliko gani MTU alifukuzwa Uwaziri Mkuu! Alikuwepo zaidi ya miaka 30 Serikali hiyo mnayosema haijafanya kitu ( kama ni kweli haijafanya kitu). Yeye anagombea Urais kwa tamaa na malengo binafsi! Enyi Bavicha ni nani aliyewaloga? Mbona mnakuwa kama Wagalatia....????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom