Lowassa ni elimu, cheki vipaumbele kabambe vya Dk. Slaa

JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
630
502
Wadau Mh.Lowasa anakuja na kipaumbele cha Elimu Kwanza nazani pia atakuwa vipa umbele vingine .Ingawa hatujui anataka kuja na style gani mpya ya maboresho kwenye sekta hii ya Elimu maana katika utawala wa Mkapa ilianzishwa program ya MMEM(Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi) na MMES (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari)ambao ulilenga kujenga shule za sekondari kila kata,maabara kwa kiwango fulani ilianza kuonyesha kufanikiwa hata hivyo awamu inayoisha haikuiendeleza kwa uzito unaostahiki program hizi

Sasa hebu tucheki baadhi ya vipaumbele vya Dr.Slaa kwa Watanzania:

Fursa kwa kila Mtanzania kupata elimu bora,
Fursa kwa kila Mtanzania kupata huduma bora za jamii,
Wajibu wa serikali kufanikisha Kilimo bora,
Fursa kwa kila Mtanzania kumiliki uchumi imara na shirikishi,
Wajibu na fursa kwa kila Mtanzania katika kupata uongozi bora na mfumo mpya wa utawala,
Fursa kwa kila Mtanzania kupata ajira na ujira bora.
 
Tunataka ajira za mkataba serikalini ili kila mmoja awe na nafasi ya kuajiriwa.
 
Umepiga viroba vya lema;
matokeo yake ndo aya;
bavicha; mnakunywa viroba vya arusha ; bora bangi ya songea
 
Mkuu wingi Wa vipaumbele sio tija...swala LA msingi ni kuwa na vipaumbele vichache vinavyotekelezela.
Kwa kipaumbele cha Mh.EL nadhan kazingatia ukwel kwamba elimu ndio chachu ya maendelea yote katika jamii ya watanzania. Kwan hatutaweza kuwa na elimu bora, afya bora, kilimo bora n.k bila kuwa na elimu bora..!! Education triggers all developmental aspects Mkuu..!!!
 
Wewe badala ya kuumiza kichwa utajiajirije unawaza tu kazi za serikalini. Tatizo hapo ni moja tu. Umepitia katika elimu duni ambayo haikukujenga kuwa mbunifu badalayake ilikuandaa tu kusubiri kuajiriwa na serikali. Pole sana ndugu.

Nafasi ndiyo hii sasa. Chagua kiongozi mwenye dalili za kufanya mabadiliko katika ajira.
 
JERRY

Jambazi hili la Richmonduli litaleta mapinduzi gani wewe??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wingi Wa vipaumbele sio tija...swala LA msingi ni kuwa na vipaumbele vichache vinavyotekelezela.
Kwa kipaumbele cha Mh.EL nadhan kazingatia ukwel kwamba elimu ndio chachu ya maendelea yote katika jamii ya watanzania. Kwan hatutaweza kuwa na elimu bora, afya bora, kilimo bora n.k bila kuwa na elimu bora..!! Education triggers all developmental aspects Mkuu..!!!

Alishindwa nini kuishauri ccm juu ya hayo alipokuwa PM na hata akiwa mbunge? Binafsi sijawahi kumuona akisimama kuyaongelea wala kuwatetea wananchi bungeni.Au shida yake ni urais tu ndiyo maana anatumia mapesa kuusaka?
 
JERRY

Mbona umeacha kipaumbele muhimu ncha kuwakumbatia matajiri?Wakati naweza kumwelewa anapozumgumzia matajiri wa kuigwa kama Mengi na Bakhresa, sikubaliani na Karamagi.

Huyu si ndiye alisaini mkataba wa kuuza mgodi wa dhahabu peke yake hotelini huko majuu na kuja kutudanganya eti ni project na siyo mine, Utajiri wa aina hiyo ni mfano wa kiugwa kweli?
 
Last edited by a moderator:
Mh.Rais ni lazima ashiriki kampain za kumnadi mgombea...???Kama akitofautiana kwa kura za kumteuwa mgombea Chamani ie yeye anamtaka X na wajumbe wengi wanamtaka Y na wakampigia kura hivi kweli kutoka Moyoni kama ni wewe utamfanyia Y kampain....???Msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom