Lowassa ni aibu kwa utawala Monduli, wanafunzi wafukuzwa kwa shinikizo lake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa ni aibu kwa utawala Monduli, wanafunzi wafukuzwa kwa shinikizo lake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibaya-kenya, Oct 27, 2012.

 1. k

  kibaya-kenya JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakubwa jana nilihudhuria sakata la wanafunzi kidato cha tano na sita walio fukuzwa kunako tarehe 5/10/2012 katika shule ya sekondari Engutoto katika wilaya ya Monduli, wanafunzi hao wameteseka sana juu ukosefu wa maji,chakula kibichi na mlinzi kuwapiga na kuwakagua usiku, tena wamelipa pesa ya remedial kila mmoja 50,000/= halafu ikatumika vinginevyo, mbali ya matumizi ya kuwalipa walimu wa masomo ya ziada.

  Jana nimehojiana na baadhi ya walimu wakaniambia hiyo pesa ndio inatumika kuwalipa walinzi, wapishi na matumizi mengine maana shule haina pesa, wanafunzi bila mafanikio yeyote walijaribu kumuuliza mkuu wa shule akawa mbogo, jana kwenye kikao cha wazazi akapiga propaganda mbaya juu ya tishio la wanafunzi kuchoma shule, na kuwapiga walimu pamoja kutishia wanafunzi wengine.

  Aibu kubwa huyu mkuu wa shule akasema wameandamana hadi kwa DC na kukataa kuongea na walimu. Kasuku huyo wa ccm akasema bodi ya shule imekaa na kuchunguza, hitimisho akatusomea waliofukuzwa watoto wa wanyonge wasio na hatia juu ya uongozi mbaya wa Engutoto sekondari huku wakifanya siasa shuleni. Kuna wazee na wakina mama wameangua kilio hapo jana kwenye bwalo la Engutoto majira ya saa kumi jioni.

  Nilichojifunza jana: Wanafunzi wamefukuzwa kutokana na amri ya Fisadi lowassa mkuu wa shule amekiri kwamba ameitwa na mbunge na kwake ni aibu shule zake wanafunzi kuandamana hivyo linamharibia kisiasa mana shule zake zina kila kitu.

  Pili waliofukuzwa wapo wa kidato cha sita ambao tumeelezwa kwamba watakuja kufanya NECTA/mitihani tuu hapo februari MWAKANI na wa kidato cha tano wameambiwa watafute shule zingine mara moja.

  Tatu, Bodi haiwezi kumfukuza mtoto bila kuwa na historia mbaya ya ukorofi au bila kuwasiliana na mzazi kwa mienendo ya mwanao.

  Nne wakuu wote wa shule sekondari na msingi katika wilaya ya Monduli wanateuliwa kutokana na utashi wa Fisadi lowassa kuna walimu wengi na wafanya kazi wa halmashauri wamefukuzwa kazi kutokana na kutompenda lowassa hivyo Engutoto wamewafukuza watoto kutokana na kuitwa na Low has, aibu kubwa kwa mbunge kushinikiza maamuzi ya kisiasa kwa idara nyeti kama hii ya Elimu.

  Tano, walimu wengi wa engutoto hawa kuunga mkono watoto kufukuzwa kutokana na udhaifu wa mkuu wa shule na mazingira ya rushwa kwa michango ya wanafunzi.

  Sita, kuna kikundi kimeundwa na LOW HAS kwa ajili ya kueneza propaganda kwamba wamasai wanamuunga mkono kuwa RAHISI WA TZ,hawa wanagawa pesa na kushawishi waandishi wa habari kuwahoji hawa vibaraka wa LOW HAS.

  Saba, huyu jamaa amewahonga viongozi wa kimila ili achaguliwe kuwa laigwanani ambapo ktk desturi ya kimasai hakuna laigwanani mkuu, hichi ni fake ili watz wamuone kama ni kiongozi mashuhuri.

  Nane, Lowassa ni masai ni mmeru waliohamia monduli miaka 1940's hivyo anawahadaa watz wamkubali kwa uroho wake wa madaraka.

  Tisa, Monduli kwa sasa huwezi kuwa kupata nafac ya kazi bila kujipendekeza kwa Lowassa na vibaraka wake halafu huyu hataki vijana waliosoma WA VYUO VIKUU angalia madiwani na viongozi wengi hapo halmashauri aibu tupu. Wamasai wa monduli wamebaki nyuma ktk swala la elimu kinacho fanyika na siasa tu.

  WanaJF, kuhusu huyu Fisadi ntaendelea kuwaletea habari zake kupitia vibaraka wake na wamasai ktk maeneo mbalimbali ya monduli, lakini hili jana la wanafunzi kufukuzwa kwa shinikizo lake nimeniuma sana, hafai kuwa chochote ktk nchi hii kumbukeni maneno ya Nyerere juu yake 1995.
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mungu tu aweza kutuponya na walafi hawa
   
Loading...