William Ngeleja (nasikia huyu familia zao zina uhusiano wa kindoa.. sijajua)
Mheshimiwa William Mganga Ngeleja(MB) ni nani?
Niseme wazi kwamba namfahamu Mheshimiwa Ngeleja kwa Takribani Miaka 25 hivi,Ni Mzaliwa Wa Bitoto Sengerema na Ana Shahada Ya Sheria kutuoka Chuo kikuu cha Dar es salaam,pia an Stashahada hiyo hiyo kutoka chuo hicho cha Mlimani.Ameoa na Ana Mtoto mmoja tu.Mkewe ni Mtu wa Ukerewe na anafanya Kazi katika Benki moja jijini Dar es salaam,na hana uhusiano wowote wa kindoa kati yake na Mheshimiwa Lowassa.
Kuhusu Mheshimiwa Ngeleja kufahamiana na Lowassa,yawezekana wanafahamiana kikazi tu wakati Mhemiwa Ngeleja akiwa Mwanasheria Wa Vodacom,kama ujuavyo Alphatel ni mmoja wa Mawakala wa Vodacom na kutokana kna kazi aliyokuwa nayo Mhe. Ngeleja ya Mwanasheria wa Vodacom(yaani Regulatory and Legal Manager) ni rahisi kufahamiana na Bwana Lowassa kwasababu ya kupitia Mikataba yote ya Kampuni ya vodacom ambayo ilikuwa ikiingiwa na kampuni zingine.
uhusiano uliopo ni ule Naibu Waziri na Waziri Mkuu,na ikumbukwe Ngeleja alianaza kuwa Naibu waziri wa Nishati wakati suala la RDC lilishafanyika,aliingia sababu ya utendaji kazi wake,ni watu wa style ya Mheshimiwa Waziri Mkuu Mpya Mizengo Pinda.aliachwa tu 2005 ila ni watu waliotakiwa kuwmo katika Baraz ala Mawaziri toka Mwaka huo.
Uadilifu Mheshimiwa William Ngeleja(WAZIRI)
Mhemiwa Ngeleja ni Mwadilifu,mchapa kazi na Mpole anayechukia Rushwa,na hata ukiuliza wafanyakazi walioko pale Waizara ya Madini watakueleza jinsi ya utendaji wake,amekuwa akifanya kazi mpaka Siku za Jumapili ili kuhakikisha shughuli zinaenda vizuri.na hata kama uakumbuka wakati dr. Mwakyembe anafunga semina ambayo wabunge walikataa mswaada wa Madini alisema,"naomba nimuite Naibu waziri aje afunge Mkutano huu,wabunge wakasema hapana..akawajibu hata huu ambaye mlikuwa naye kipindi chote mkiwasiliana vizuri".ina maanisha Dr. Mwakyembe alimwaamini Mhe. Ngeleja ni Mwadilifu.Hata kamati ya Mwakyembe haikuonesha kwamba yeye ni mtu Fisadi.
Ripoti ya Mwakyembe haikumhusiha na suala la RDC kwenda Dowans,hii inaonesha kwamba yeye si mmoja wa waliliingiza taifa katika matatizo ya kupand akwa Umeme.
Utendaji kazi wa Mheshimiwa Ngeleja(Mbunge)
Mheshimiwa Ngeleja amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika Jimbo lake,na imefikia hata kuacha familia yake kuwatumikia wananchi wake.Mfano wakati wa sikukuu ya Krismasi nna Mwaka Mpya alikuwa jimboni kwake akitatua matatatizo ya wanajimbo lake na akiacha familia yake.hii inaonesha anavyojali matatizo ya wananchi wake.Ameweza kuhakikisha kivuko cha kigongo feri ambacho kimekuwa kero kwa muda wa miaka 15 kinaleta na kufungwa,na hivi karibuni kitafunguliwa na Mhe. Rais,amweza kuhakisha anasomesha wanafunzi wasiojiweza kuendelea na Elimu ya juu hasa sekondari natayari kuna mfuko wa kuendeleza suala hilo unaosimamiwa na wananchi wenyewe.
Hitimisho
Aliyekupa habari hizo,kwa namna moja ama nyingine ana lengo la kumchafua Mheshimiwa Ngeleja kisisasa,na wameamua kukutumia Mzee Mwanakijiji kwasababu wamejua una sauti mbele ya watanzania na si jambo zuri kuchafua Wanasiasa vijana wa Umri wetu amabo wana lengo la kuondoa kero na matatizo ya wananchi wake,Mhe. Ngeleja ni mwanasheria na nina uhakika atashughulikia kwa makini suala linalohusika mikataba mibovu ambayo serikali imeingia kipindi cha nyuma.na hana uhusiano wa kifamilia na Mhe. Edward Lowassa.Nataka kusema Hivi Mheshimiwa Ngeleja hana Mahusiano yoyote na Lowassa zaidi ya Mahusiano ya kikazi tu.!
"Kama tukianza kuchafuana ,sidhani kama kuna mwanasiasa yoyote ambaye anayeweza kubaki.."Lowassa
Naomba kutoa hoja.