Lowassa mzee wa mabadiliko ana nyota inayonga'aa hili halina ubishi. Wanaobisha watabisha kwa kuwa wamezoea kubisha. Kati ya wanasiasa watano wenye mvuto Tanzania Lowassa ni mmoja wapo. Sasa je Lowassa ana nafasi yoyote ya kutekeleza azma yake yakuwa kiongozi wa taifa hili? Kwa maoni yangu hapana.
Lowassa ni kama Raila Odinga...hawatakuja kuwa viongozi wa juu wa mataifa yao. Raila atatumia mbinu na nguvu zote lakini hawezi kuwa kiongozi wa Kenya. Sasa basi nini hoja yangu. Kwakuwa Lowassa hatatimiza azma yake, namshauri arudi Monduli akaandike kitabu juu ya maisha yake. Ni muhimu sana kuweka historia yake kwenye maandishi kwa ajili ya vizazi na vizazi.
Watanzania wangependa kujua kuhusu urafiki na 'uadui' wake na Kikwete, sakata la Richmond na yeye alicheza nafasi gani, na kubwa zaidi, watanzania wangependa kujua jinsi 'alivyoinunua' CHADEMA. Je ni kiasi gani alitoa na kwa kina nani? Kitabu hiki kama kitaandikwa kitakuwa ni BEST SELLER. Hapa ndipo Lowassa atarudisha mabilioni yake aliyoyapoteza kwenye uchaguzi uliopita.
Baba Lwaigwan nakuomba utafakari hili na ulifanyie kazi.