Lowassa ndani ya Mbeya ktk Harambee ya Moravian

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Waziri Mkuu aliyejiuzuru, EL amewasili Jijini Mbeya leo asubuhi tayari kwa kuendesha zoezi la harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana ya Chuo kikuu cha Moravian TEKU. Aidha EL alikataa kufanya harambee hiyo ndani ya uwanja wa CCM wa kumbukumbu ya Sokoine kwa madai kuwa hataki kuhusisha ujio wake na chama. Kitu cha kushangaza, ni kuwa wakati anatua uwanja wa ndege, alilakiwa pamoja na viongozi wa kanisa, walikuwepo viongozi wa CCM mkoa na wilaya.

Naona kaka ndo anaanza tambo za kutambulika nyanda za juu kusini ktk safari ya kuelekea 2015.
 
Naona ameamua kufia kanisani sasa maana ndani ya NYINYIEMU hamna matumaini kwake
 
nenda lowasa,watumikie wananchi,watsema sana lakini mwenyezi Mungu yu pamoja nawe,tunakuombea maisha marefu
 
Ameenda kufanya corporate social responsibility ili kugawana faida aliyoichuma kupitia ufisadi uliofanyika akiwa waziri mkuu.
 
Katika nchi maskini kama Tanzania mwenzetu unakuwa milionea, twambie umepata wapi huo utajiri?.....Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Semeni msiseme Lowassa bado ataendelea kubarikiwa kwa kazi za jamii anazozifanya, nyie semeni tuu mkijua mnambomoa kumbe mnamjenga siku hadi siku.
 
fanya linalokutuma kufanya mzee EL, wasiokupenda daima wanakuombea mabaya lkn kwa kuwa umesimama kwenye ukweli na upendo kwa wa TZ wenzako Mwenyezi Mungu atakulinda , wako wengi wenye mali kidogo kama wewe lkn hawajitoi kwa jamii yao kama wewe ni kwa sababu ni wachoyo ,maneno machafu na kupakana matope kusikukatishe tamaa, watu wenye kukuhitaji wana kiu na wewe usirudi nyuma.
 
Back
Top Bottom