Uchaguzi 2020 Lowassa na Mkewe wamdhamini Rais Magufuli ili atete kiti cha Urais katika Uchaguzi wa Oktoba 2020

Membe ajifunze kwa Lowasa leo hii anavyotukanwa na wapinzani.
Chondechonde Membe usiende upinzani siku ukirudi CCM watakutukana kama anavyotukanwa Lowasa na vitoto vya graduate zero.
Kurudi upinzani sio issue , anatukanwa kwakua ni Kigeugeu...amewaumiza watu sana walio ccm na hata nje
Lowassa huyu leo watu walikufa kwa ajili yake
watu vilema kwa ajili yake
watu wamefilisiwa kwa ajili yake
Leo hii ccm na chadema kuna watu wanaitwa wa Lowassa hawaaminiki tena kote
Lowassa huyu kuna watu wako ndani kwa maumivu yake
Lowassa huyu hadi Mkwewe yuko ndani
Lowassa huyu hadi watoto wake wamekasirika kwa kukosa msimamo
Lowassa huyu binti yake kila siku analia mumewe yuko ndani na hata ahadi mwaka umepita ...
lowassa huyu amekuwa kama kibwetere , yule mtumishi wa Mungu aliyeangamiza wafuasi yeye akatoroka
Hakuna mfuasi wa lowassa hata mmoja leo hii hana maumivu yote hii kwa kumfuata yeye ..
wako wapi wakina Guninita na wazee wengine ambao leo hii wanaishi maisha ya Tabu kwa kumuunga yeye mkono

Viongozi ni Kina Raila .....kabla hajaingia deal ya Kisiasa anaweka kipengele cha kuwahusisha wafuasi wake wote ....sio watu wameteseka kwa ajili yake unabebwa kama mkoba na Rostam na wewe ni kiongozi ndio umewafikisha wenzako hapo walipo unaamua kuunga mkono juhudi kwa kuwa mbinafsi na tumbo lako .....angejenge heshima kama angehakikisha deal lake linahusisha msamaha kwa wafuasi wake wote especially ndani ya CCM ambao leo wanateseka .....

Heshima Yake Iko Wapi leo >?
 
Kurudi upinzani sio issue , anatukanwa kwakua ni Kigeugeu...amewaumiza watu sana walio ccm na hata nje
Lowassa huyu leo watu walikufa kwa ajili yake
watu vilema kwa ajili yake
watu wamefilisiwa kwa ajili yake...
Ndo mana mimi sioni umuhimu wa Membe kwenda upinzani.kwa kuwa uchaguzi ukiisha atarudi CCM na mtamtukana kama Lowasa hivi sasa.
 
Nafurahi kumuona mzee wetu Lowassa pale alipoamua KUJITAMBUA KUBADILIKA NA KUACHA MAZOWEA. Nitakuwa mtovu wa shukrani iwapo nitamshambulia mzee wetu huyu kwani BINAFSI NILIMUUNGA MKONO SANA KIPINDI KILE KABLA HAJAIHAMA CCM....
Nilikesha kwenye TANURI LA FIKRA Facebook kuinadi VISION YAKE,comrade SAID Sambala anajua(naye kaacha MAZOEA) Mussa Abdallah anajua(naye kaacha MAZOEA) mh.Hussein Bashe anajua(naye kaacha MAZOEA). Duuh jamani NI VIJANA wenzangu wa CCM wengi Sana tena Sana(WAMEACHA MAZOEA).

KIU ILIYOWASUKUMA KUWA NA LOWASSA KIPINDI KILE HAJAHADAIKA KUKIMBIA CHAMA ILIKUWA NI KUCHOSHWA NA CCM ILIYOKUWA NA MAJUNGU NA ILIYOKOSA UDHIBITI WA KIUONGOZI.

Hatukumuunga mkono mh.Lowassa ndani ya CCM eti kwa SABABU TULIKUWA TUNAKWENDA KULA NYAMA KULE OLPURKWA MONDULI nope Bali SISI VIJANA TULIOKUWA TUNAIONA NAKISI YA KIUONGOZI TULITAKA TUWE NA MTU MUUNGURUMAJI na alhamdulillah BWANA amesikia kilio Cha watanzania...MWANAUME WA CHATO NDIYE MSHIKA HATAMU WA CHAMA CHETU NA MUUNGURUMAJI HASWA.

NIWAKUMBUSHE kuwa mh.Lowassa aliporudi CCM alisema maneno machache mno yafuatayo.
1.Assalama aleikum
2.Tumsifu Yesu Kristo
3.NIMEREJEA NYUMBANI
4.MSINIULIZE KWA NINI

JITAMBUE BADILIKA ACHA MAZOWEA TEMBEA NA MAGUFULI 2020.

Popote ulipo Maalim Seif Abalhassan mbeba mikoba ya MJANJAMJANJA WA MJINI Zitto Zuberi Kabwe,nakusalimu in Ridhiwani Kikwetes voice kwi kwi kwi kwi
 
Ndo mana mimi sioni umuhimu wa Membe kwenda upinzani.kwa kuwa uchaguzi ukiisha atarudi CCM na mtamtukana kama Lowasa hivi sasa.

Mbona Sumaye hatukanwi.......Lowassa ni tofauti kuna watu wengi wanateseka kwa kumuunga yeye mkono hasa ndani ya ccm ....heshima yake ilikuwa kuacha siasa tu na kubakia Mzee kama kina Cleopa Msuya .
 
View attachment 1487688

Kutoka kuwa kamanda hadi kulazimika kumdhamini mtu ambaye huamini falsafa yake ni jambo la kuhuzunisha mno !

labda Kwa faida ya wanajf na wengine wasiojua ni kwamba Mzee Lowassa ni miongoni mwa wengi waliosalimu amri baada ya kusomeshwa namba na utawala wa awamu ya 5 , Mpaka naandika haya Mkwe wake yuko selo kwa kesi ya kutakatisha pesa .

Natoa wito kwa watu wote kwamba ukishajiona wewe ni legelege usijaribu kushiriki siasa za upinzani , utajuta .
Huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono!!!
 
Fisadi ni fisadi tu na amerudi kwao alipotoka manake asingeweza kukaa CHADEMA mtu kama huyu.
 
safi sana, kwahio unamaanisha upinzani walishindwa kumuajibisha lowasa na mkewe mpaka ameenda ccm ndo wamemuajibisha! mnakwama wapi cdm
Upinzani watamuwajibishaje!
Wenye uwezo huo ni DPP na TAKUKURU kwa njia ya kumshtaki mahakamani
 
Mbona Sumaye hatukanwi.......Lowassa ni tofauti kuna watu wengi wanateseka kwa kumuunga yeye mkono hasa ndani ya ccm ....heshima yake ilikuwa kuacha siasa tu na kubakia Mzee kama kina Cleopa Msuya .
Sumaye hana carier kama ya Edlow na Membe.japokuwa pia alitukanwa ila sio saana.
Minachosema Membe akienda upinzani uchaguzi ukipita piga ua lazima atarudi home.sasa hapo ndo mabomba ya matusi yatakapo funguliwa.ni bora akubali yaishe.
 
Upinzani watamuwajibishaje!
Wenye uwezo huo ni DPP na TAKUKURU kwa njia ya kumshtaki mahakamani

kama cdm mlikua mnajua hayo yote mmeshindwa kufungua kesi mahakamani bali mkaona sahihi ni agombee uraisi kupitia cdm! kweli mmefikia hapa?
 
Sumaye hana carier kama ya Edlow na Membe.japokuwa pia alitukanwa ila sio saana.
Minachosema Membe akienda upinzani uchaguzi ukipita piga ua lazima atarudi home.sasa hapo ndo mabomba ya matusi yatakapo funguliwa.ni bora akubali yaishe.
Hata mimi nilikua na maoni hata kabla lowassa hajahama 2015 kuwa ingekua bora angebakia ccm ..isingebadilisha kitu Chadema wangeendelea na Slaa wao ...ila yeye angebaki na heshima yake na asingewagarimu wafuasi wake kupata mateso wanayopitia
 
kama cdm mlikua mnajua hayo yote mmeshindwa kufungua kesi mahakamani bali mkaona sahihi ni agombee uraisi kupitia cdm! kweli mmefikia hapa?
All criminal cases zinafunguliwa na DPP na kuendeshwa na DPP hivyo watu binafsi kama wapinzani hawawezi kufungua kesi za jinai mahakamani.
 
Back
Top Bottom