Lowassa na mikakati ya kuongeza mapato ya serikali ijayo

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
MIKAKATI YA KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI

Yapo Maeneo Kumi na Tisa Kama Ifuatavyo:


1. Kujenga nidhamu ya matumizi ya serikali na kuachana na matumizi yasiyo na msingi ambayo yamekuwa utamaduni kwenye serikali ya sasa. Kwa mfano, Magari ya kifahari, safari zisizo na tija, posho zisizoeleweka, semina na makongamano yasiyoisha. Vyote hivi vitafikia ukomo.

2. Kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Asilimia Kumi Na Tano (15%) ya pato la taifa na kufikia Asilimia Ishirini kama wenzetu Kenya n.k.

3. Kupunguza misamaha ya kodi kufikia asilimia moja (1%) tu ya pato la taifa (au chini ya hapo) kama inavyoshauriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Wenzetu Kenya na Uganda wameweza. Tanzania inapoteza zaidi ya Shilingi Nne kila Mwaka kutokana na misamaha holela ya kodi.

· Tukilitekeleza hili pekee, tutaweza kulipa Deni la Walimu la Shillingi Bilioni Thelathini na Tatu na bado chenji kubwa ikabaki kuboresha maslahi ya Polisi, Madaktari, n.k.

4. Kuhakikisha kwamba misamaha yote ya kodi inawekwa wazi na inakaguliwa na mamlaka ya kodi (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha Za Serikali (CAG), pamoja na Kamati husika za Bunge.

5. Kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia vibaya mfumo wa kodi kutoa mizigo yao bandarini.

6. Kuhakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inakagua gharama za uwekezaji zinazofanywa na makampuni ya nje ili kutoza kodi sahihi. Udanganyifu wa baadhi ya makampuni husababisha upotevu wa mapato ya serikali.

7. Kuhakikisha kwamba mikoa mingine ya nchi yetu inachangia zaidi kwenye makusanyo ya kodi. Kwa sasa asilimia 70 ya mapato yanayokusanywa na TRA yanatoka Dar es Salaam.

8. Kuongeza idadi ya walipa kodi kwa kuja na sheria mpya ambayo itahakikisha kwamba kila Mtanzania anayefikisha umri wa miaka kumi na nane anasajiliwa kama mlipa kodi na kama ana shughuli ya kumuingizia kipato, analipa kodi inayostahili bila kuonewa.

9. Kuboresha mfumo wa kodi kwa lengo la kuwawezesha wananchi waone faida ya kulipa kodi kwa kuwapatia huduma za kijamii zinazoendana na kodi wanazotozwa.

10. Kujenga mazingira rafiki ya kodi kwa makampuni ya nyumbani ili kuwapa motisha kulipa kodi na kuchangia taifa lao. Kwa mfano, hivi sasa idadi ya idadi ya makampuni yaliyoandikishwa na TRA kulipa kodi ni zaidi ya laki 5, ingawa wanaolipa ni asilimia ndogo sana.

11. Kuongeza ufanisi wa Bandari ya Da-es-salaam ili iweze kushughulikia mizigo mingi zaidi na hatimaye kupata wateja wengi zaidi, hususan kutoka nchi zilizotuzunguka. Bandari zetu ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.

12. Kuhakikisha kwamba Halmashauri zetu zinajitegemea zaidi kibajeti badala ya kutegemea zaidi ruzuku kutoka serikali kuu. Pia kuhakikisha kwamba Halmashauri zetu zinatoa hati fungani kwa ajili ya kujipatia mapato kwa ajili ya miradi maalum ya maendeleo.

· Pia Serikali Ya Edward Lowassa itaangalia sheria zilizopo ambazo zinaonekana kuzibana halmashauri zetu kutafuta au kubuni miradi bila ya ruhusa kutoka serikali kuu.

13. Kurekebisha kodi ya Misitu ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la Serikali.

14. Kuimarisha sekta ya utalii kwa kuhakikisha kwamba nchi inavuna maradufu ya viwango vya sasa. Mkakati mkuu ni kuitangaza zaidi Tanzania nje, hususan kwenye nchi za Asia na Mashariki ya Kati.

15. Kuanzisha Bahati Nasibu Maalum kwa kila mkoa na kila Risiti ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwa ni tiketi ya bahati nasibu hiyo. Pamoja na kuwa chanzo cha mapato kwa Serikali, hii itawavutia wananchi wengi kuanza kudai risiti zao za kodi kila wanaponunua bidhaa na huduma mbalimbali nchini.

16. Kudhibiti biashara nje ya nchi kimagendo maarufu kama Panya Routes (PANYA RUTI).

17. Kutunga sheria kali itakayodhibiti utoroshaji wa fedha nje ya nchi.

18. Kutafuta njia za gharama nafuu za kukopa ikiwa ni pamoja na kupitia hati fungani ya nchi (Sovereign Bond) kwenye masoko ya fedha ya kimataifa badala ya kukopa kwenye vyanzo ghali kama mabenki ya biashara. Riba za mabenki ya biashara ni kubwa na huiumiza nchi.

19. Kuanzisha mfuko maalum wa matumizi ya mapato yatokanayo na gesi (Sovereign Wealth Fund) na kuusimamia kitaalam. Ingawa mapato ya gesi yataanza kuingia baadaye kidogo, fedha zote zitakazopatikana kutokana mirabaha ya gesi asilia zitawekezwa huko na zitatumika kwenye shughuli maalum za maendeleo, na siyo kwenye bajeti za matumizi ya kawaida. Nia ni kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo vinanufaika na uwepo wa maliasili hiyo muhimu hapa nchini. Hatuwezi kurudia makosa ya usimamizi yaliyotokea wakati tulipoamua kuyachimba madini yetu, ambapo sasa hivi tumebakiwa na mashimo tu.


TUNATAKA KUIPELEKA TANZANIA MBELE, NI WAKATI WA MABADILIKO!

 
Ningependa kujua msimamo wa Lowasa kuhusu Sera ya Majimbo ya Chadema na hasa nikiunganisha na hilo la Halmashauri kujitegemea badala ya kutegemea Serikali Kuu.
 
Hii ni sera ya Lowassa au sera yako katika fikra zako?

By the way, mgombea anahutubia kwa wastani wa dakika 10 kwa kila mkutano atatoa wapi muda wa kuzisema sera za kufikirika za CHADEMA?

Yeye anasimama na kusema vipaumbele vyake ni elimu, elimu, elimu na kuomba kura.

Mbowe anataka kutuuzia mbuzi kwenye gunia kama alivyowauzia CHADEMA.

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania achilia mbali udhoofu wake kiafya na kifikra.
 
Back
Top Bottom