Lowassa na kofia mbili, Zitto na udhaifu wa Mbowe

S

SDP_TZ_Mpya

Senior Member
Joined
Jun 21, 2013
Messages
166
Likes
3
Points
0
S

SDP_TZ_Mpya

Senior Member
Joined Jun 21, 2013
166 3 0
Wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM ngazi ya taifa mwezi Oktoba 2012, Lowassa alikuja na mkakati ambao baadhi ya wana-CCM waliukubali. Hoja ilikuwa zitenganishwe kofia ya uenyekiti wa chama taifa na Urais ili kuimarisha uwajibikaji. Kambi ya Kikwete ilimtumia vizuri mzee Yusuph Makamba kuzima 'uasi' huo hasa siku ya uchaguzi huku wazee wakitumika kumpoza Lowassa kuwa amwachie tu rafiki yake amalize salama. Hivyo mambo yakapita kwa Kikwete kupata 99% (kura 2 zilisema hapana) huku Shein na Mangula wakizoa zote. Ikumbukwe pia ni marufuku CCM kumpinga Mwenyekiti aliyeko madarakani ambaye anataka kuendelea. Pia, ni marufuku kumpinga Rais aliyeko madarakani huku bado na tamaa ya kuendelea na mhula wa pili.

Katika kesi zote mbili za uenyekiti na Urais CCM husema "fomu iko moja tu na imeshachukuliwa" - Nape.

Kwa upande wa Zitto, nae anadai Mbowe ni dhaifu sana kiuongozi na ni haki yake kugombea. Licha ya waraka kukiri kuwa Mbowe na Slaa wameingia madarakani kukiwa na wabunge 5 tu wa CHADEMA na sasa wako 49 yaani wameongeza wabunge kwa asilimia karibu 1,000% na madiwani lukuki huku kura za Urais wakifikia mamilioni.

Bila kujali ukongwe wa chama na Mazingira yanayokizunguka CDM, Zitto anaona bado haki yake ni bora hata km CDM italipa gharama kubwa kutokana na ukweli kuwa CCM inaiwinda CDM usiku na mchana.

Vyama vyote vikiwemo CCM na CDM (ingawa viko kwenye hatua tofauti sana ya uhai) vina mahitaji ya ndani yanayovifanya viwe makini kwenye kubadilisha uongozi. Sikushangaa kufa kwa "mkakati wa kofia mbili" CCM na km vile Zitto, Mwigamba na Kitila wanavyodhihirika kukihujumu chama chao cha CDM kupitia "mkakati wa ushindi 2013". Hata hivyo, CDM iko kwenye uchanga zaidi wakati CCM iko kwenye kujifufua, hali inayovifanya vyama hivi kuwa makini na kila uamuzi unaohusisha badiliko la uongozi.

Kama ambavyo Lowassa alistahili kufukuzwa CCM, CDM wamepata fursa ya kum-offload Zitto na washirika wake. Madhara ya kuunda vikundi mkakati ndani ya Chama ndiyo yatakayoleta mpasuko na kukiua CCM 2015 hasa wakati na baada ya uteuzi wa mgombea Urais. CCM wamechelewa ila CDM muwahi haraka kwani Zitto anaonekana kuyaficha mengi na tayari mtandao wao walishaujenga kila alipoenda kwenye za peke yake (km anavyokiri kufanya) na unafanya kazi.
 
S

SDP_TZ_Mpya

Senior Member
Joined
Jun 21, 2013
Messages
166
Likes
3
Points
0
S

SDP_TZ_Mpya

Senior Member
Joined Jun 21, 2013
166 3 0
Hata hivyo demokrasia inahubiriwa zaidi CHADEMA kwenye uenyekiti na CCM haishughulishwi. Not so easy to comprehend hasa unapoona wanaoshupalia demokrasia ndani ya CDM ni watu wa CCM.
 
L

london

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2010
Messages
223
Likes
2
Points
0
L

london

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2010
223 2 0
Hee mbona mimi chama changu cha CCM sikielewi. Majuzi Zitto alivuliwa uongozi CHADEMA lakini viongozi wangu km Nape na wengineo walikuwa wa kwanza kusema kuwa Zitto alivuliwa madaraka yake kwa vile alitangaza nia ya kuutaka umwenyekiti wa Chadema. Siku nyingi hazijapita tumemsikia Lowassa akitangaza ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania kupitia CCM lakini ameshambuliwa kikwelikweli na Nape pamoja na Mangula. Wote Nape na Mangula wakidai kuwa wanaotangaza nia ya kugombea urais kupitia ccm wamekosa sifa za kuteuliwa lakini Mangula akadai wote hao wataitwa ktk vikao vya chama, watahojiwa na watachukuliwa hatua za kinidhamu. Sasa mimi sielewi km chama changu kinafanya siasa za mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu? Nikimaanisha kuwa swala km hilo wanaliona ni sawa likifanywa kwenye vyama vya upinzani lakini linakuwa siyo sahihi kwenye chama chetu tawala cha ccm.

Mimi sioni tatizo la Lowassa kutangaza ndoto yake ya kutaka kuwa rais wa Tanzania kwa sababu iwayo yote nafasi ya urais iko wazi mwaka 2015. Lowassa hajatangaza kutaka kumng'oa Kikwete wakati huu akiwa madarakani! Kwani Kikwete anamaliza musimu wake wa pili kwa mujibu wa sheria na hivyo hatakuwa na sifa tena za kugombea urais kwa mujibu wa katiba ya sasa. Kwa hiyo Lowassa kutangaza nia yake tena bila kuwananga viongozi walioko madarakani si uhaini na haki yake kabisa ili watu wapate muda wa kumtathmini. Pengine ni tofauti ni Zitto ambaye yeye amekuwa akitangaza ndoto yake ya urais na uenyekiti wa chama chake kwa kuwaponda viongozi waliopo na kushusha ufanisi wa chama chake kupitia blogs, facebook, media na mikutano ya hadhara. Lakini km Zitto angefanya mambo yake bila kuwadhalilisha viongozi au chama chake sidhani kungekuwepo mtafaruku baina ya Zitto na chama chake au viongozi wenzake wa chadema.

Sr. Magdalena

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Messages
803
Likes
105
Points
60
Sr. Magdalena

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2011
803 105 60
Mods piga ban, MEANDU,
hawa vijana wa Bavichwa Gongo itawauwa
 
Mkuu vipi umeshafika Maryland bar, nasikia jana ulipita hapo, na ulikuwa unalalamika kusimamishwa kazi, pole sana
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,900
Likes
10,116
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,900 10,116 280
Kwahili tu mnyonge mnyongeeni haki yake mpeni ccm wako wakomavu kisiasa kuliko CDM
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,900
Likes
10,116
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,900 10,116 280
Hee mbona mimi chama changu cha CCM sikielewi. Majuzi Zitto alivuliwa uongozi CHADEMA lakini viongozi wangu km Nape na wengineo walikuwa wa kwanza kusema kuwa Zitto alivuliwa madaraka yake kwa vile alitangaza nia ya kuutaka umwenyekiti wa Chadema. Siku nyingi hazijapita tumemsikia Lowassa akitangaza ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania kupitia CCM lakini ameshambuliwa kikwelikweli na Nape pamoja na Mangula. Wote Nape na Mangula wakidai kuwa wanaotangaza nia ya kugombea urais kupitia ccm wamekosa sifa za kuteuliwa lakini Mangula akadai wote hao wataitwa ktk vikao vya chama, watahojiwa na watachukuliwa hatua za kinidhamu. Sasa mimi sielewi km chama changu kinafanya siasa za mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu? Nikimaanisha kuwa swala km hilo wanaliona ni sawa likifanywa kwenye vyama vya upinzani lakini linakuwa siyo sahihi kwenye chama chetu tawala cha ccm.

Mimi sioni tatizo la Lowassa kutangaza ndoto yake ya kutaka kuwa rais wa Tanzania kwa sababu iwayo yote nafasi ya urais iko wazi mwaka 2015. Lowassa hajatangaza kutaka kumng'oa Kikwete wakati huu akiwa madarakani! Kwani Kikwete anamaliza musimu wake wa pili kwa mujibu wa sheria na hivyo hatakuwa na sifa tena za kugombea urais kwa mujibu wa katiba ya sasa. Kwa hiyo Lowassa kutangaza nia yake tena bila kuwananga viongozi walioko madarakani si uhaini na haki yake kabisa ili watu wapate muda wa kumtathmini. Pengine ni tofauti ni Zitto ambaye yeye amekuwa akitangaza ndoto yake ya urais na uenyekiti wa chama chake kwa kuwaponda viongozi waliopo na kushusha ufanisi wa chama chake kupitia blogs, facebook, media na mikutano ya hadhara. Lakini km Zitto angefanya mambo yake bila kuwadhalilisha viongozi au chama chake sidhani kungekuwepo mtafaruku baina ya Zitto na chama chake au viongozi wenzake wa chadema.

Point of clarification,EL kautaka uraisi na sio uenyekiti wa chama chao ccm
Hivyo ni vitu viwili tofauti sana,kama lowassa ana kosa basi ashitakiwe na Jamhuri kwa kujiandaa kufanya uhaini(mapinduzi kabla ya 2015)
 
Asprin

Asprin

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Messages
57,364
Likes
38,748
Points
280
Asprin

Asprin

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2008
57,364 38,748 280
Point of clarification,EL kautaka uraisi na sio uenyekiti wa chama chao ccm
Hivyo ni vitu viwili tofauti sana,kama lowassa ana kosa basi ashitakiwe na Jamhuri kwa kujiandaa kufanya uhaini(mapinduzi kabla ya 2015)
Anautaka urais ifikapo 2015 kama ambavyo zitto alikuwa anautaka. uhaini ni kutaka kumpindua rais aliyeko madarakani. Kikwete hatakuwa madarakani 2016 kwa hiyo rais mpya lzm apatikane 2015. Its either Eddo au candidate toka CDM, Kazi ni kwako.
 
N

nghang

Member
Joined
Apr 3, 2013
Messages
18
Likes
0
Points
3
N

nghang

Member
Joined Apr 3, 2013
18 0 3
nape na mangula hawana ubavu wa kumwadhibu lowassa labda mangula amesahau kilichomkuta baada ya jk kutwaa madaraka 2005 nahisi amekumbuka kilimo cha nyanya huko iringa.....maana anaingia kwenye bahari yenye kina kirefu ambacho hawezi kuvuka!!!
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,900
Likes
10,116
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,900 10,116 280
Kuna watu wanatumia mwavuli wa nia ya mbio za kuwania uraisi wa Tanzania kwa aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa JK, Mh E Lowassa (mb) kulilinganisha na sakata la Zitto kabwe kuutaka uenyekiti wa chama chadema
Naomba tutumie akili kidogo kutofautisha urais wa nchi na uenyekiti wa chama,watu wanaofanya hizi propaganda wana nia moja tu ya kutaka kutuaminisha kuwa CCM hamna demokrasia kama chadema na hivyo basi kutimiza adhima yao ya kufanya udikteta kwa kumfukuza ZZK kwakua kaonyesha nia yote ya kuutaka uenyekiti huo na hivyo basi kuwa tishio kwa Mh mbowe ambaye anajipanga kujitosa tena kwa hila ya kuondoa kipengele cha ukomo wa madaraka katika katiba ya chama
Ni lazima ikumbukwe kuwa kitendo cha Lowassa kuutaka urais kisheria kingetafsiriwa kuwa ni uhaini(mpango wa mapinduzi ya nchi)kwa sababu suala hilo linahusu nchi zaidi rather than chama chao CCM
Rai yangu:ili cdm tujipambanue kuwa ni chama cha siasa na tuko tofauti na ccm ni lazima misingi ya demokrasia ya kweli izingatiwe pratically ikiwemo kupokea changamoto za mitazamo tofauti ndani ya chama bila kusahau kuruhusu uwanda mpana wa kupiga kura za kuchaguliwa viongozi wake wa chama

Nawasilisha-ningefurahi sana watu washushe facts,points na sio maneno ya kukaririshwa na matusi ya udhaifu wa kukosa hoja ya ku counterattack my point
 
sixgates

sixgates

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Messages
3,974
Likes
112
Points
145
sixgates

sixgates

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2011
3,974 112 145
Kuutaka urais ccm is synonymous to kuutaka uwenyekiti... Ndani ya CCM uwenyekiti unakuja automatically baaada y kuwa rais, ningemuona Lowass mwendawazimu angesema anautaka uwenyekiti....By the way inaelekea siasaa umeanza huna muda mrefu. Karibu
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
74
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 74 145
Kuutaka urais ccm is synonymous to kuutaka uwenyekiti... Ndani ya CCM uwenyekiti unakuja automatically baaada y kuwa rais, ningemuona Lowass mwendawazimu angesema anautaka uwenyekiti....By the way inaelekea siasaa umeanza huna muda mrefu. Karibu
Nini tafsiri yako katika majibu yako haya?
 
Mtoboasiri

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2009
Messages
5,104
Likes
105
Points
0
Mtoboasiri

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2009
5,104 105 0
Mods piga ban, MEANDU,
hawa vijana wa Bavichwa Gongo itawauwa
Hapo tu ndipo buku 7 fc mnaponicha hoi: kukwepa kujibu hoja na kurukia "hoja" za "gongo, uzinifu, kuiba wake za watu" etc, etc, etc. For once, jitahidi kujibu hoja zilizopo kwenye maada! Ni bora ushindwe kwa hoja kuliko "kushinda" kwa viroja!

Btw: Angalau umekiri kuwa BAVICHA ni VICHWA!
 
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Messages
902
Likes
482
Points
80
Age
39
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2011
902 482 80
Lowassa ana haki ya kugombea urais kama mtz yoyote,mbona membe,january,sitta na wengine wasikemewe? Mangula kanuni za ccm ni kwa ajili ya lowassa tu? Nilisema tokea mwanzo.kuwa mangula kwa siasa za sasa hana.jipya ni bora akaendelee kulima nyanya
 
L

london

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2010
Messages
223
Likes
2
Points
0
L

london

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2010
223 2 0
Kuna watu wanatumia mwavuli wa nia ya mbio za kuwania uraisi wa Tanzania kwa aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa JK, Mh E Lowassa (mb) kulilinganisha na sakata la Zitto kabwe kuutaka uenyekiti wa chama chadema
Naomba tutumie akili kidogo kutofautisha urais wa nchi na uenyekiti wa chama,watu wanaofanya hizi propaganda wana nia moja tu ya kutaka kutuaminisha kuwa CCM hamna demokrasia kama chadema na hivyo basi kutimiza adhima yao ya kufanya udikteta kwa kumfukuza ZZK kwakua kaonyesha nia yote ya kuutaka uenyekiti huo na hivyo basi kuwa tishio kwa Mh mbowe ambaye anajipanga kujitosa tena kwa hila ya kuondoa kipengele cha ukomo wa madaraka katika katiba ya chama
Ni lazima ikumbukwe kuwa kitendo cha Lowassa kuutaka urais kisheria kingetafsiriwa kuwa ni uhaini(mpango wa mapinduzi ya nchi)kwa sababu suala hilo linahusu nchi zaidi rather than chama chao CCM
Rai yangu:ili cdm tujipambanue kuwa ni chama cha siasa na tuko tofauti na ccm ni lazima misingi ya demokrasia ya kweli izingatiwe pratically ikiwemo kupokea changamoto za mitazamo tofauti ndani ya chama bila kusahau kuruhusu uwanda mpana wa kupiga kura za kuchaguliwa viongozi wake wa chama

Nawasilisha-ningefurahi sana watu washushe facts,points na sio maneno ya kukaririshwa na matusi ya udhaifu wa kukosa hoja ya ku counterattack my point
Km nia ya Lowassa ni swala la nchi kutaka kufanyiwa uhaini basi ccm wangekaa kimya badala ya kumpiga mkwala wa kunyimwa nafasi ya kugombea.
 
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
2,264
Likes
12
Points
0
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
2,264 12 0
Point of clarification,EL kautaka uraisi na sio uenyekiti wa chama chao ccm
Hivyo ni vitu viwili tofauti sana,kama lowassa ana kosa basi ashitakiwe na Jamhuri kwa kujiandaa kufanya uhaini(mapinduzi kabla ya 2015)
Huyu Ngoyayi alivyokomalia kutenganisha Uenyekiti wa Chama na Urais unafikiri alichokuwa anakitaka ni nini? Wewe unasubiri aseme "nataka Uenyekiti" ndio uthibitishe kuwa kweli anautaka?
Be serious plse!
 
L

london

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2010
Messages
223
Likes
2
Points
0
L

london

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2010
223 2 0
Point of clarification,EL kautaka uraisi na sio uenyekiti wa chama chao ccm
Hivyo ni vitu viwili tofauti sana,kama lowassa ana kosa basi ashitakiwe na Jamhuri kwa kujiandaa kufanya uhaini(mapinduzi kabla ya 2015)
Sidhani km umesoma kwa umakini na kuelewa nilichoandika.
 
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Messages
1,964
Likes
229
Points
160
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2013
1,964 229 160
Hayo ni mawazo yako
 
Forum statistics

Threads 1,252,134
Members 482,015
Posts 29,797,628