Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Pengine wana ccm wanajua ama hawajui adui yao mkuu katika kilele cha kushika dola ya nchi hii tajiri huku wakaazi wake ni MAFUKARA totoro.
Tangu rais wangu kipenzi Jakaya wa Musoga ashike hatamu za uongozi mwaka mwaka 2005, chama kilianza kupoteza umaarufu ndani na nje ya nchi, niukweli uaiopingika kuwa JK alikikuta chama kikiwa katika mwangaza mkuu wa kisiasa, chama kikijinadi chenyewe, chama kikisikika hata kwa walioenda vidatu, chama kikisikika hata kwa walio peponi.
Fikiria sana mwanaccm, nini sababu za ccm kutoweka moyoni mwa Watanzania? Jiulize sana, je Jakaya ni sababu? Tafakari zaidi mwana ccm, harakati za raisi JK za kuelekea magogoni na kampeni za urais wake wa mwaka 2005 ziliratibiwa na kufanikishwa kwa fedha kharamu, nasema kharamu kwa ukweli ulio wazi,
Labda nirejea kidogo mapito ya KAGODA=CCM, MEREMETA=CCM, DEEP GREEN=CCM nk. Hayo yote makampuni yalizaliwa kwa lengo la kufanikisha ushindi wa ccm,
Hivyo rais wa Tanzania ni moja ya maadui wa ccm kushinda 2015 kwakuwa ametokana na zao la ufisadi, kamwe hawezi kunyoshea kidole mafisadi waliomuweka madarakani, zaidi atawasamehe na kuwaambia warudishe pesa hizo huku wananchi wakishindwa kuthibitisha kama kweli zimerudi au laa, Watanzania sio wajinga, wanaelewa na wataijibu ccm 2015, na jibu litakuwa na kishindo kikuu.
Baada ya kuingia madarakani Jk alimteua SWAHIBA wake Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu wa Nchi, Malengo ya wawili hawa na mazingira yao ilikuwa waje wapokezane kijiti, na walikula nadhiri kabisa hata kujipambanua mbele za umma kuwa urafiki wao HAWAKUKUTANA barabarani ni (urafikimaalumu)
Mwaka 2007 tofauti za wawili waliokula nadhiri maalumu ilianza kuonekana hasa baada ya kuanza kuingizana mjini, wanaiba wote mwisho wasiku mmoja anajifanya hahusiki, Lowasa alichukia sana akawa mweusi tiiiiii, yaani kwa tuliobahatika kumtizama kupitia runinga ya TBCccm pale Dodoma siku ile nae anaamua kumwaga mboga (kujiuzuru) tulifaidi kuona hasira ya waliokula nadhiri.
Tangu siku hiyo Lowassa aliamua kuingia msituni kukivuruga chama cha mapinduzi, kuivuruga serikali na kuifanya nchi isitawalike. Katika hili amefanikiwa kwani tangu mwaka 2007 alipoachia madaraka, ndipo umaarufu wa ccm ulipoanza kuporomoka kwa kasi, makundi masilahi yakaibuka, serikali ikanza sasa kuishi kwa maruhani ya akina Mwaisapile, kila kukicha linaibuka hili mara lile, rais akaugua ghafla ugonjwa wa kusafiri hataki kabisa kuishi ikulu,
Hayo yakitendeka kwa kasi Lowasa kila siku yupo misikitini na makanisani kuwania Baraka za Muumba huku ccm na serikali yake wakiweweseka na CHADEMA, eti ndicho kinafanya nchi isitawalike? Kinaongoza migomo? Kinaiyumbisha ccm? Kinaleta makundi ndani ya ccm?
USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.
Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mda uliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyo mkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI, Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani,
Hakuna njia yamkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchi iingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamoja inatimia.
Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE na EDWARD LOWASA
Mkifaulu kuwaunganisha hawa wakawa na malengo sawa hata kama hawataongea, chama kitashinda 2015,
Njia nyingine muhimu na yaharaka ni kuwanyang'anya uanachama Jakaya Kikwete na Edward Lowasa!
Muwaambie warudishe kadi zenu, wakaendelee na madili yao nje ya chama!
Kumbukeni kuwa Lowasa ana nusu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm ambao wanaishi wa PESA yake.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
IN CHADEMA WE TRUST