Lowassa, Mzindakaya wazungumzia Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Mzindakaya wazungumzia Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Lowassa, Mzindakaya wazungumzia Katiba

  Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko; Tarehe: 4th January 2011 @ 23:59


  WATANZANIA wanapaswa kupata elimu ya angalau mwaka mmoja juu ya Katiba, kabla ya kuanza kukusanya maoni yao.

  Ushauri huo umetolewa na Mbunge mstaafu wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya ambaye pia alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kusoma ‘alama za nyakati’ kuhusu Katiba mpya.

  Dk. Mzindakaya alishauri kuwa Tume itakayoundwa na Rais kuanza mchakato wa kupata Katiba mpya, haina budi kwanza kuhakikisha elimu hiyo inatolewa ili wananchi waijue vizuri Katiba na kuwa na fursa nzuri ya kutoa maoni yao.

  Akimpongeza Rais Kikwete alisema uamuzi wake kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba ulitolewa wakati muafaka ili kuepusha vurugu zilizokuwa zikichochewa chini kwa chini na wakati mwingine waziwazi kwa mgongo wa mabadiliko.

  Mwanasiasa huyo mkongwe aliyesema kuwa amestaafu ubunge lakini si siasa, aliponda madai ya baadhi ya wana CCM, kuwa Rais hakupitia vikao vya chama katika kutoa uamuzi huo na kufafanua kuwa siasa inaangalia zaidi muktadha wa jambo husika.

  Alisema hata ndani ya chama hakukuwa na namna ya kukataliwa kwa jambo hilo kutokana na kuwa tayari kuna taasisi nje na ndani ya nchi zilizotaka kutumia suala hilo kuchochea vurugu.

  "Kuna vurugu nyingi nchini, zinatokea kutokana na uchochezi tu, sasa suala hili la Katiba liliishakuwa na msukumo kutoka nje na iwapo Rais angekawia kutoa tamko lingesababisha vurugu ndani ya nchi, hivyo Rais Kikwete alitumia utashi mkubwa wa kisiasa kutoa msimamo,” alisema Mzindakaya.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Viwanja vya Bunge, Mzindakaya alisema uamuzi wa Rais ni wa busara na wenye kuonesha upeo mkubwa, hivyo kilichobaki ni kuacha malumbano na kusubiri Tume itoe mawazo ili yafanyiwe kazi.

  Alisema katika siku za karibuni, wanasiasa,viongozi wa dini na wanataaluma, wamekuwa wakitoa mawazo mbalimbali jambo ambalo si wakati wake, bali ni kutaka kusababisha malumbano ya kutaka serikali ngapi huku jambo la msingi likiwa ni kusubiri Tume.

  Alisema Tume ikishaundwa, ambayo alisema anaamini itakuwa ni kwa maslahi ya nchi, haitakuwa na kazi ya kuandika Katiba bali ni kutoa elimu na kukusanya maoni ya wananchi na kuyapeleka bungeni, hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi.

  Alishauri kuwa muda wa utoaji elimu ya Katiba usipungue mwaka mmoja, kutokana na umuhimu wa jambo lenyewe, kwani Watanzania wa sasa ni tofauti na wa miaka ya nyuma wanaelewa, hivyo watatoa maoni yao.

  Mzindakaya ambaye alikuwa Mbunge kwa miaka 44, alisema Tume itakayoundwa licha ya kukusanya maoni ya watu, pia itaangalia katiba za nchi zingine kwani Rais ameshakubali kuwa na Katiba mpya hivyo hapana sababu ya kuweka viraka.

  Alisema kwa uzoefu alionao kwa kipindi chake cha ubunge, tume mbalimbali ziliundwa
  kukusanya maoni na kupelekwa bungeni na tena kurudishwa kwa wananchi kabla uamuzi haujafikiwa, hivyo hakuna sababu ya hofu na serikali katika kuunda Tume.

  Alisema lazima serikali iratibu mchakato huo kwa kuunda Tume yenye watu watakaoweka maslahi ya nchi mbele, ambapo Serikali, wananchi na Bunge, lazima washirikishwe kwa kiasi kikubwa katika mchakato huo.

  Naye John Mhala, anaripoti kutoka Arusha, kwamba Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amempongeza Rais Kikwete kwa kukubali mabadiliko ya Katiba na kutoa mwito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao wakati ukifika.

  "Rais wetu hakusubiri wananchi waandamane, na ndiyo maana kaamua kutangaza rasmi kuunda Tume ya kuratibu Katiba, naomba wakati ukifika wananchi jitokezeni na kazi hiyo ifanyike kwa amani na utulivu,” alisema Lowassa.

  Alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Manyire, Mlangarini, wilayani Arumeru alipozungumza katika sherehe za kupongeza na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua mgombea wa CCM, Mathias Manga kuwa Diwani wao.

  Lowassa aliwataka wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita, kutekeleza kwa vitendo ahadi walizowapa wananchi, ili kubadilisha hali zao na kuwa na imani na Serikali iliyoko madarakani.

  Aliwataka viongozi kuweka kipaumbele katika kujali matumbo ya wapiga kura wao ikiwa ni pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa kuwakopesha, ili waanzishe miradi ya kujikwamua kiuchumi kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi nchini kwa sasa.

  "Wakati umefika kwa viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kubadilika na kuacha tabia na mazoea ya kujinufaisha wao na familia na jamaa zao na kuhakikisha wanajikita zaidi kutumikia wananchi hususan kujali wanakula nini," alisema Lowassa.

  Naye Diwani wa Kata hiyo, Manga aliwashukuru wananchi kwa kumchagua na kusema hawakukosea na atawalipa kwa utendaji wake, kwa kujitahidi kutatua kero sugu ambazo
  zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Huyu Babu kweli kachoka.......hajui hadi leo kuwa katiba ni mali ya raia wote siyo mali ya JK na kuwa hiyo Tume ya JK haina nguvu ya kisheria kwa sababu Bunge halijashirikishwa.............................Kama Bunge halijashirikishwa je sisi walalahoi huku pembeni itakuwaje.................

  Huyu Babu atueleze Bilioni kumi alizopora pale BOT atazirudihsa lini...........hizi kauli ni shukrani kwa kuruhusiwa kulifanyia maovu taifa hili..............bila ya kuwajibishwa na dola ambayo JK yupo kwenye usukani akipulizia ufisadi uendelee kukolea................
   
 3. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wanasiasa wote wanaanza kudandia dandia hatakama walikuwa wanaipinga hoja awali, ni juz tu nilimsia Werema akisema oh yale yalikuwa maoni yangu tu, mbona kabla alikuwa anakosolewa hivyo hakutoa kauli yake, amesubiri Raisi ametatoa msimamo ndo anatufunga kamba, akae kimya tu tumeshaona ni mtu wa namnagani!
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZEE MZINDAKAYA USIPATE TAABU WATANZANIA TUTAKUSHANGAZA NA KATIBA ZURI HUJAWAHI KUONA, KWA ELIMU ZETU HIZI HIZI ZA NGUMBARU

  Mzee Mzindakaya kapumzike siasa kama ulivyohiari mwenyewe baada ya kucheza sana uwanjani kwa miaka mingi.

  Hakuwa haja ya kutuelimisha Watanzania mpaka tuwe na mi-digrii za sheria ndio tutoe maoni yetu namna gani tunavyotaka tutawaliwe. Na kwa mshangao wa wanaotubeza kwamba kama taifa ni mbumbumbu watashangazwa jinsi tutakavyoandika katiba zuri ya kudumisha haki na amani zaidi nchi kwa kutumia ELIMU YETU HII HII YA NGUMBARU na baadaye mafundi wa sheria kuweka vizuri zaidi bila kupunguza wala kuongeza ladha kwenye maoni yetu ya msingi.

  Jmani Watanzania wenzangu kwa kauli hii ya Mzee Mzindakaya sasa napata fununu kwa nini CCM ilitamani katiba iandikwe na MADALALI BADALA YA SISI WANANCHI WENYE JUKUMU HILO - ni kwamba katika miaka 47 yote chama hiki kinatambua ya kwamba wametukandamiza na kutunyima fursa za kupata elimu nchini isipokua watoto wa wakubwa ndio wanaorushwa midege kwenda majuu kupunga upepo na wakirudi tu na wao pia ni viongozi wetu.

  Hebu mtazame hata naye huyu dogo VIOLET MZINDAKAYA BAADA YA KUSOMA CHUO KIKUU CHA MACHINJIONI VIGUNGUTI naye pia keshaanza minyodo katika taifa ambalo hata msichana wa kazi wa waziri na pia ni waziri.
   
Loading...