Lowassa: Mungu yu pamoja nami! Atumia biblia kubeza wanaomchafua kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa: Mungu yu pamoja nami! Atumia biblia kubeza wanaomchafua kisiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Nov 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  • Atumia biblia kubeza wanaomchafua kisiasa
  • Asema Mungu yu pamoja naye, adai anapumua

  Na Pendo Mangala,Singida

  [​IMG]


  Alisena kutokana na kuwepo na mambo mengi ya siasa, amekuwa akichafuliwa jina lake kupitia vyombo, lakini anamshukuru Mungu amemlinda na kumfariji wakati wote.


  Alisema siku zote watu wengi wamekuwa wakimfuatilia katika mambo ya kisiasa, huku wakimtuhumu kuwa ni fisaidi, lakini kwa kuliamini neneo la Mungu ambalo limekuwa msada mkubwa kwake.

  "Siku moja tulikuwa tumekaa na mke wangu, tunaangalia runinga kipindi cha magazeti, kukawepo na taarifa nyingi za hovyo kuhusu mimi ambazo baadhi ya taarifa hizo mtangazaji alishindwa kuzisoma,"alisema Lowassa.


  Alisema kufuatia kuwapo kwa taarifa hizo, mke wake aliingia ndani na kuchukua Biblia na kumsomea neno kutoka kitabu cha Isaya 40-10.


  Maneno hayo ya Biblia yanasema "Usiogope kwa maana mimi ni pamoja nawe,usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako nitakutia nguvu,naam nitakusaidia, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa hai yangu"


  Pia kitabu cha Warumi 8 mstari wa 31 ambao unasema ‘basi tuseme nini juu ya hayo?Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliye juu yetu,


  "Kwakweli baada ya maneno haya yalinifariji sana na kunitia nguvu na sasa ninaishi kwa amani,"alisema Lowassa.


  Hata hivyo, aliwashukuru viongozi mbalimbali wa dini wakiwemo Waislamu kwa maombi yao ambayo wamekuwa na upendo juu yake kwa kumuombea kila siku.


  Kwa upande wake, Askofu wa Dayosisi, Eliufoo Sima alisema madai ya maskini nchini ni mengi ambayo ni pamoja na mahitaji ya kila siku ambayo wangependa viongozi wayashughulikie kwa umakini mkubwa.


  Alisema kama viongozi hao watashughulikia mtatizo ya wananchi, watakuwa wamepiga hatua kubwa ya kuondoa manung'uniko miongoni mwa watu ambayo yaanaharibu jamii ya Kitanzania.


  Katika harambee hiyo ya ujenzi wa kanisa, Lowassa alichangia Sh 10 wakati kiasi cha Sh 138 zilipatikana kutoka kwa watu mbalimbali.


  Wiki iliyopita, Lowassa alivunja ukimya wakati alipopata nafasi ya kuzungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali zikiwemo tuhuma za yeye kudaiwa kuwa ni fisadi.


  Alikanusha kuhusika na tuhuma hizo na kutaka wale walioneza tuhuma hizo kwa kutumia rasimalia za chama hicho, wachukuliwe hatua akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu Lowassa hafai kuwa rais, anaweka DINI na SIASA ni mtu wa kuogopa kweli

  Atatuweka kwenye hali mbaya haswa, ukishaanza kuchanganya DINI na SIASA inaashiria UMEFILISIKA KISIASA
   
 3. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  basi tuseme nini juu ya hayo?Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliye juu yetu, Mungu hawezi kuwa upande wa mwizi, fisadi na mtu mbinafsi kama Lowasa. Kama anadhani alionewa ni kwa nini aliamua kuacha ulaji wa uwaziri mkuu na kubaki kusumbuana na kina Nape? Kwangu mimi Lowasa ni Mwizimwizi tu kama wezi wengine ambaye hata asafishwe na brashi gani hasafiki abadani!
   
 4. n

  nyabina Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: May 29, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nyie siyo Mungu kukaa na kumhukumu mtu.Hata akiwa mwizi,wewe ambaye unamnyooshea kidole mwenzako,angalia ni vidole vingapi vimekugeukia wewe,embu tujifunze kuwa si wepesi wa kumnyooshea/kuwanyooshea mtu/watu vidole.Tumpende Lowassa na kumwombea,ni kiongozi tayari na hilo halina ubishi,kumbukeni maombi ya mwenye haki mmoja huliponya taifa,basi mimi au wewe tuwe mmoja wa wenye haki,tuwaombee viongozi wetu na Mungu ataliponya taifa letu,tusiwe wa kwanza kulaumu.Mungu hapendi lawama,tuko jangwani kumbukeni.
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ushahidi mkuu vinginevyo utakuwa unamshuhudia jirani yako uongo
   
 6. d

  daniel_mollel Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa hiyo wanasiasa waachane na dini zao?
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... Be MINDFUL with Holy Books!!!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sio waache Dini zao wasiambatanishe Dini zao na kuwania Madaraka...

  Sio kwamba Mungu ndiye aliyeashiria awe Rais, ni nia ya mtu yoyote kama Raia wa Tanzania kuwa Rais

  Nchi Nyingi zinazoweka DINI pamoja na SIASA zina matatizo; Ulisha wahi kumsikia Nyerere kuashiria uongozi wake ni wa Mungu?
   
 9. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wa tz tunajulikana sana kwa kuzungumza. ukibishana na mtz utashindwa lakini ukweli utabaki palepale. Mh. Lowasa amechafuliwa sana lakini pengine ndiye atakayetufaa katika taifa kutuondoa kwenye umasikini na ujinga. Tumuombe Mungu tu; kama hatamtaka huyu Mh. aje kuwa raisi basi tutapata jibu na kama atakuwa ameamua kumpitisha kwenye kikaango cha wa Tz kabla ya kumpa uraisi basi wazandiki wataipata pata kwa maana nadhani jamaa ana hasira sana.:juggle:
   
 10. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hata shetani mambo yalipokuwa magumu, ali-quote mistari kadhaa ya BIBLIA; Lakini haikusaidia kumlainisha Yesu Kristo.
   
 11. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Achana na story za vidole wewe bwana mdogo! Nani anamhukumu EL? Anajihukumu mwenyewe kwa matendo yake. Kwanini 'nyie' hamshtuki, mbio za kuelekea Ikulu mapema namna hii??Ikuku kunani?
  Shauri yenu-kalaghabaho!
   
 12. R

  Renegade JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,760
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Du!!! Kazi kweli kweli.
   
 13. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu mmasai mwenzako anachanganya dini & siasa, hakuna aliyesema aache dini yake bana!
   
 14. K-killer

  K-killer Senior Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa kama alikua anajua tokea mwanzo kua Mkuu wa nchi anampotosha,na mikataba ni feki na kwamba alimshauri rahisi lakini rahisi hakumsikiliza ikam'bidi ye afate maagizo.Sasa kwanini kama aliona kuna hayo mapungufu kwanini asinge re-sign from the beggining mpaka alipopewa tuhuma na kuambiwa ni fisadi ndo aka resighn alafu leo hii anatuambia alichafuliwa,Kama anania nzuri angekua wakwanza kulitangazia taifa kua kuna matatizo na ameamua ku re-sign,Sio mpaka watu wamshitukie ndo anatuletea habari yakua alichafuliwa
   
 15. N

  Nyadunga Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Jamii ikioza hata makanisa ni sehemu ya jamii hiyo.Acheni lowassa atakaswe na kuwa mtakatifu na baadae kututawala!
  Hata mungu anaemwabudu naamini anawasamehe wenye dghabi kama Lowassa. Je aw-Tanganyika tutamsamehe?
  Njia inaonekana ni nyeupe kwenye chama cha magamba. Labda tumzuie huku upande wa pili CDM
   
 16. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Lowassa lowassa lowasssa,haki ya mungu laana ya mungu itakuandama!!!!!!ulishakataliwa na mwenye nchi!!wewe unang'ang'ania kwa kila namna!!!!!
   
Loading...