Lowassa: Mkapa alikuza uchumi, JK punguza matumizi

Anazungumzia uchumi.............anakiri kwamba serikali imefanya kazi kubwa sana..........miundombinu n.k........maeneo ya kushughulika hasa inflation................tusiwalazimishe watu wauze mazao arusha kutoka songea...wapate nafasi ya kuuza kwa uhuru..............Kuhusu mafuta kwamba serikali kununua mafuta kwa wingi na serikali kupunguza matumizi.

Kusimamia kilimo cha mashamba makubwa na kilimo cha umwagiliaji itapunguza inflation
 
Zamani nilikuwa namuona anaweza kuleta mabadiliko lakini hakuna kitu. Anazungumzia vitu vingi ambavyo hana maamuzi navyo na sijui kigezo gani kimetumika kumualika katika kipindi.
Pia ametumia fursa vizuri kumshambulia hasimu wake Membe kuwa hafanyi maamuzi magumu kununua nyumba za ubalozi na kuzikarabati. Kwa ujumla hana mpya na hajaonesha kitu cha ziada kwa mtu anayeutaka urais.
 
Siasa kweli ni mahesabu makali. Sasa lowassa ameamua kuelekeza makombora yake kwa Membe! Nchi hii tutafika kweli.
 
Mbona anaongea kama yeye ni mkuu sana hapa nchini??

Anaongelea nyumba za serikali kwenye balozi mbali mbali.

Huko washngton wanataka USD 1mil ili wakarabati waweze kupangisha.

Wanataka NSSF iwe inakopesha serikali kujenga nyumba nje ya nchi.

Duh!

Huyu jamaa ukimsikiliza unaweza jiuliza anafaa hata kuwa Dc?
 
Leo tarehe 20/08/2012 saa 3.00 Usiku Edward Lowassa atakuwa ndani ya dakika 45 za ITV. Je kuna jipya? Natarajia atajibu hoja za JK kwamba wanaozungumzia vita kati ya Malawi na Tanzania ni wapinzani.

Source: Radio One

Ujue mpaka sasa huo usemi wa jk sijajua bado alikuwa akitaka kumaanisha nini
 
tulete matrekta, matrekta matrekta!

Hata enzi za Bwana Yesu walikuwa wameacha jembe la mkono.

Walete meengi zaidi, mvua je?

Leo kapita wanapouza akakuta yameisha akafarijika sana.
 
hapo mtakuwa mnambebesha mzigo usiokuwa wa kwake maana hakuna jambo la richmond alilolifanya ambalo rais alikua halifahamu. :car:

Swala sio kama Rais alikua anajua au hajui swala ni ule mgao wake kashaurudisha? Au anamsubiri mzee nae arudishe mgao wake kwanza
 
Bora LOWASA AONGELEE HILI, maana naona mkuu kashindwa kazi kaogopa!!!!! Lowassa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama...ongea bwana hao Malawi wasitutanie. Siwa letu afu wanatuchezea kisa....nanukuu 'udhaifu wa rais wetu'

Teh teh eti siwa, kwani hata Tz wakipewa lote si bado mafisadi ndo watakaofaika huku walala hoi tukishindia miayo
 
Namsikiliza kwa makini sana!

Bahati mbaya nimekikosa kipindi hicho muhimu. Bila shaka, utanijuza angalau kwa ufupi maudhui ya jumla ya maelezo ya Lowassa. Nimeambiwa kwamba ameanza kwa kuponda utendaji kazi wa wizara ya nje na uhusiano wa mimataifa. Kwa harakaharaka naanza kuamini maneno ya watu kwamba Membe na Lowassa ni kambi mbili uchaguzi 2015 zinazokinzana waziwazi.
 
anaongelea vitalu vya gesi.

Jamani hivi kweli huwa wanaperuzi hata kidogo kuhusu biashara fulani inavyoendeshwa??
 
If I were his daughter, I would advise him to retire from active politics and concentrate more on improving his deteriorating health. His seemingly irresistible presidential ambitions, which seem now to be really beyond his reach, only serve to beguile him of his body strength.
 
Waziri mkuu mstaafu EL akizungumza na suleiman semunyu katika kipindi cha dakika 45 kirushacho na ITV.Amezungumza mambo mengi.Swali ni je alipo kuwa waziri mkuu kilimshinda nini?.Nawasilisha.
 
Huyu mtangazaji wa hiki kipindi uwezo ni mdogo sana wa kuuliza maswali. Anauliza yale ya kumfurahisha Lowassa tu, sijui ameishaweka bahasha mfukoni!? Nahisi maswali aliishayaandaa Laigwanan jamaa anatimiza wajibu tu
 
Back
Top Bottom