Lowassa, Mbowe wapongezwa kwa kuwabana BAVICHA

Dnashon

Member
Feb 19, 2016
58
33
Kumsifia Rais kwa utendajiwake Ni jambo la hekima na busara kubwa. Si rahisi kwa wapinzani kufanya hili jambo.

Hongereni Sana, dhana kuwa wapinzani kazi Yao Ni kupinga Kila kitu kweni imekuwa tofauti.

Hongereni sana

=======

LOWASSA NA MBOWE WAPONGEZWA KUWABANA BAVICHA

DODOMA - Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepongezwa kutokana na upevu wa kisiasa wanao onesha baada ya kuwapiga stop vijana wa BAVICHA wasiende kutibua mkutano mkuu wa CCM mjini hapa.

Pongezi hizo zimetolewa na wanachama wa CCM mjini hapa kutokana na utulivu uliopo na kauli za viongozi wa CHADEMA ili kuhakikisha CCM wanafanya mkutano wao kwa amani.

"Tunampongeza Mhe Freeman Mbowe na Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Mhe Edward Lowassa kuwazuiya vijana wao kuja hapa. Hata hivyo wangeishia kuchezea mkong'oto wa karne kama wangekaidi kutowasikikiza viongozi wao," alisema mwanachama mmoja hapa Dodoma.

Kiongozi mmoja wa UVCCM amesema, " tunawapongeza BAVICHA kwa kutii amri ya wakubwa zao, kuacha ujinga wa siasa za kitoto na kuamua kufuata siasa za kiukomavu kama alivyowaasa kamanda wao Lowassa," alisema kiongozi huyo.

Alionya kuwa maandalizi ya kuwakabiri vijana hao kutoka vyombo mbalimbali vya dola yako vizuri na kuwa vyombo hivyo vimejipanga vizuri sana."

Alisema walioko Dodoma wasijemsukuma mtu hata mmoja la sivyo watawaharibia hata wenzao walioko hapa Dodoma au wanaopita kwa shughuli binafsi au za kiofisi, alionya.

"BAVICHA wanaoeneza uvumi wa kijinga kuwa wanakuja Dodoma, itawaletea majanga wapita njia wa Chama hicho kuangukia mikononi mwa vyombo vya Dola, waache mara moja," alisisitiza.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma tayari imetoa maelekezo kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwa wasiwapangishe watu wasiowajua.

Nipashe imeripoti kuwa nyumba za kulala wageni 306 na nyumba 3,331 tayari vimechukuliwa na CCM.

Nao viongozi wa CCM walioko mjini hapa wamesema maandalizi yanaendelea vizuri sana na hali ni shwari kabisa.

"Tunajianda kumuaga Mwenyekiti wetu na Sekretariati yake na pia kumkaribisha Mwenyekiti mpya na timu yake ya ushindi wa 2020," walisikika wakisema.

Alisema uongozi huu unaong'atuka chini ya Mh Kikwete na Kamanda Kinana, ulifanya kazi nzuri sana iliyoleta ushindi wa uongozi wa Serikali iliyoko madarakani.

"Ni heshima kubwa sana kwa viongozi wanaong'atuka, wameiletea CCM heshima kubwa ya ushindi wa kishindo. Tunawaaga kishujaa hawa majemadari wetu, walisema.
 
Kiongozi wa chadema ni Mzee Mtei...pale Mbowe amechomekwa kwa kupitia mgogo wa "mkwe"...mwenye chama yupo Tengeru
Haya majungu yenu CCM dhidi ya wapinzani huwageuka mnajikuta mnapigana majungu wenyewe kwa wenyewe ndani ya CCM kwasababu mmekariri dawa ya anayekupinga ni majungu.
 
Kumsifia Rais kwa utendajiwake Ni jambo la hekima na busara kubwa. Si rahisi kwa wapinzani kufanya hili jambo.

Hongereni Sana, dhana kuwa wapinzani kazi Yao Ni kupinga Kila kitu kweni imekuwa tofauti.

Hongereni sana

=======

LOWASSA NA MBOWE WAPONGEZWA KUWABANA BAVICHA

DODOMA - Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepongezwa kutokana na upevu wa kisiasa wanao onesha baada ya kuwapiga stop vijana wa BAVICHA wasiende kutibua mkutano mkuu wa CCM mjini hapa.

Pongezi hizo zimetolewa na wanachama wa CCM mjini hapa kutokana na utulivu uliopo na kauli za viongozi wa CHADEMA ili kuhakikisha CCM wanafanya mkutano wao kwa amani.

"Tunampongeza Mhe Freeman Mbowe na Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Mhe Edward Lowassa kuwazuiya vijana wao kuja hapa. Hata hivyo wangeishia kuchezea mkong'oto wa karne kama wangekaidi kutowasikikiza viongozi wao," alisema mwanachama mmoja hapa Dodoma.

Kiongozi mmoja wa UVCCM amesema, " tunawapongeza BAVICHA kwa kutii amri ya wakubwa zao, kuacha ujinga wa siasa za kitoto na kuamua kufuata siasa za kiukomavu kama alivyowaasa kamanda wao Lowassa," alisema kiongozi huyo.

Alionya kuwa maandalizi ya kuwakabiri vijana hao kutoka vyombo mbalimbali vya dola yako vizuri na kuwa vyombo hivyo vimejipanga vizuri sana."

Alisema walioko Dodoma wasijemsukuma mtu hata mmoja la sivyo watawaharibia hata wenzao walioko hapa Dodoma au wanaopita kwa shughuli binafsi au za kiofisi, alionya.

"BAVICHA wanaoeneza uvumi wa kijinga kuwa wanakuja Dodoma, itawaletea majanga wapita njia wa Chama hicho kuangukia mikononi mwa vyombo vya Dola, waache mara moja," alisisitiza.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma tayari imetoa maelekezo kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwa wasiwapangishe watu wasiowajua.

Nipashe imeripoti kuwa nyumba za kulala wageni 306 na nyumba 3,331 tayari vimechukuliwa na CCM.

Nao viongozi wa CCM walioko mjini hapa wamesema maandalizi yanaendelea vizuri sana na hali ni shwari kabisa.

"Tunajianda kumuaga Mwenyekiti wetu na Sekretariati yake na pia kumkaribisha Mwenyekiti mpya na timu yake ya ushindi wa 2020," walisikika wakisema.

Alisema uongozi huu unaong'atuka chini ya Mh Kikwete na Kamanda Kinana, ulifanya kazi nzuri sana iliyoleta ushindi wa uongozi wa Serikali iliyoko madarakani.

"Ni heshima kubwa sana kwa viongozi wanaong'atuka, wameiletea CCM heshima kubwa ya ushindi wa kishindo. Tunawaaga kishujaa hawa majemadari wetu, walisema.

NYUMBU huwa wanaelewa kweli utashangaa 23 hao barabarani mpaka bomu ndo litakalo wazindua
 
Back
Top Bottom