Lowassa, Mbowe wamwaga sumu Monduli

Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Messages
1,831
Likes
4,406
Points
280
Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2017
1,831 4,406 280
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa wamesema baada ya kumalizika kwa chaguzi ndogo nchini wataibuka na ajenda ya kudai haki na uhuru.

Wamesema uhuru na haki unavunjwa licha ya Katiba ya nchi kufafanua kwa kina kuhusu mambo hayo.

Wametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Monduli, Yonas Laizer.

Akizungumza katika mkutano huo Lowassa amesema mambo yanayoendelea Monduli anatamani angekuwa na nafasi na uwezo wa kugombea tena ubunge ili kusimama kupinga vitendo vya uvunjaji wa katiba.

“Wana Monduli mambo yanayoendelea kwa sasa nchini yanahitaji Katiba Mpya tena itakayotoa adhabu kwa yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume chake ikiwemo haya ya kuwanyima wapinzani kugombea, kuongoza au kufanya siasa kwa kuwatisha, kuwateka na kuwalaghai,” amesema Lowassa.

“Natamani ningegombea tena mngeona kama haya ningeruhusu ila kwa sababu siwezi basi naombeni mpeni kura Laizer. Nitakuwa nampa mbinu za kufanya na msikubali kuibiwa siku hiyo mkiletewa fujo wamama naombeni pigeni ukunga wa mwizi nasi tutawasaidia.”

Kwa upande wake Mbowe amesema kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, mikutano ya hadhara huku viongozi wa vyama vya siasa wakitishiwa ni uvunjwaji wa sheria, kwamba kwa sasa wanavuta kasi ya kuanzisha ajenda ya kutaka Katiba ya nchi kufuatwa.

“Rais anapoingia madarakani mbali na kuapa kwa kutumia kitabu cha dini yake lakini pia anaapa kulinda, kupigania na kutetea katiba ya nchi,” amesema Mbowe.

“Cha kushangaza ndio kwanza katiba inavunjwa ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge.”

Amesema kwa sasa hata wapinzani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita wanatishiwa, kutekwa huku wenye mioyo mepesi wakilaghaiwa kwa fedha na madaraka.

“Wananchi tunapaswa kufahamu kuwa hakuna aliye juu ya sheria, si kiongozi wala mtawala. Haki na wajibu vinapaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na na wananchi kugombea na kuchaguliwa bila kujali wanawakilisha chama gani wala wao ni dini gani,” amesema.

Amesema anashangazwa na kitendo cha wagombea wa CCM katika chaguzi ndogo kutumia viongozi wa Serikali kuwapigia kampeni sambamba na kutumia magari ya Serikali.
“Baada ya uchaguzi huu tutaanzisha hoja ya kupata maelezo ya chaguzi hizi ni za kisheria au za kihuni hasa mawaziri na viongozi wa Serikali kupigia kampeni wagombea wa CCM,” amesema.

“Pia wagombea wenyewe kutumia magari ya Serikali ikiwemo analotumia mgombea ubunge wa CCM Monduli (Julius Kalanga). Gari hilo ni la mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha vijijini (kutaja aina na namba zake).”

Mbunge wa Chadema Arusha Mjini, Godbless Lema amewataka wananchi kumchagua Laizer ili afichue maovu ya Kalanga ambaye alikuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya Chadema kabla ya kutimkia CCM na kupitishwa kuwania tena ubunge.

Kwa upande wake Laizer amewataka wananchi wa Monduli kumchagua ili kurejesha huduma za maji za uhakika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma Lowassa alipokuwa mbunge wa jimbo hilo

“Nichagueni jamani nihakikishe namuumbua Kalanga juu ya kuwagawia wananchi wasio wa Monduli ardhi ya Monduli,” amesema Laizer.
monduli-2bpic-jpg.865478
 
kidunula1

kidunula1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Messages
1,738
Likes
1,248
Points
280
kidunula1

kidunula1

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2016
1,738 1,248 280

“Nichagueni jamani nihakikishe namuumbua Kalanga juu ya kuwagawia wananchi wasio wa Monduli ardhi ya Monduli,” amesema Laizer. View attachment 865478
Huyo kalanga aligawa ardhi kwa watu wasio wa monduli akiwa nani,mbunge wa CHADEMA au!? Kama ni hivyo kuna haja gani kuichagua CDM iliyoshindwa kumsimamia mbunge wake!?
 
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
12,000
Likes
6,121
Points
280
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
12,000 6,121 280
Sumu ipi wamemwaga? Maana ni kosa kisheria kama wamemwaga sumu sbb itaua wananchi..!! CHADEMA kwanini mnamwaga sumu ili mfanye killings kwanini lakn?
 
sheiza

sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
3,151
Likes
3,153
Points
280
sheiza

sheiza

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
3,151 3,153 280
Huyo kalanga aligawa ardhi kwa watu wasio wa monduli akiwa nani,mbunge wa CHADEMA au!? Kama ni hivyo kuna haja gani kuichagua CDM iliyoshindwa kumsimamia mbunge wake!?
Sio hilo tu..eti wanasema achaguliwe laizer ili afichue maovu ya karanga alipokuwa chadema..inawezekana hawa watu ni wabaya zaidi kuliko hata wa ccm..kwa nini kama walijua anafanya maovu walimuacha tu au nao wana maovu yao ambayo sisi hatuyajui??
 
Carlos The Jackal

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2018
Messages
3,488
Likes
4,771
Points
280
Carlos The Jackal

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2018
3,488 4,771 280
Kama kubeba nchi ilikua ni 2015..Kuanzia Tz mpaka dunian uko walikua tayar.

Mahesabu wakayakosea.
 
T

tzcountry I love

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Messages
397
Likes
327
Points
80
T

tzcountry I love

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2018
397 327 80
Tutashangaa sana nchi itakavyobebwa!
 
K

Kasongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2007
Messages
2,262
Likes
1,528
Points
280
K

Kasongo

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2007
2,262 1,528 280
Kila la heri wana Monduli
 
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
16,135
Likes
9,199
Points
280
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
16,135 9,199 280
Aisee naona Mgombea wa Chadema kiti cha ubunge amekosa priorities maana yeye lengo la kupata ubunge ni kumuumbua mtu na sio kuwapa maendeleo wana monduli.

Sasa nao sijui wana monduli priority yao ni kuumbuliwa kwa kalanga ? Sitaki kuamini hivyo.
 
Troll JF

Troll JF

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Messages
7,053
Likes
10,176
Points
280
Troll JF

Troll JF

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2015
7,053 10,176 280
Sumu ilikua ya Nani😂😂😂😂😂😀😀
 
kidunula1

kidunula1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Messages
1,738
Likes
1,248
Points
280
kidunula1

kidunula1

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2016
1,738 1,248 280
Sio hilo tu..eti wanasema achaguliwe laizer ili afichue maovu ya karanga alipokuwa chadema..inawezekana hawa watu ni wabaya zaidi kuliko hata wa ccm..kwa nini kama walijua anafanya maovu walimuacha tu au nao wana maovu yao ambayo sisi hatuyajui??
Hawa watu bongo zao zishachoka
 
Forum statistics

Threads 1,236,398
Members 475,125
Posts 29,256,698