Lowassa, Mbowe wabeba siri nzito

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Chama cha demokrasia na maendeleo, chadema chini ya Freeman Mbowe, kinakabiliwa na mtihani mkubwa mbele yake unaokitaka kuamua kuanzia sasa muelekeo wa siasa zake.

Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya chama chadema zinasema, Mwenyekiti Mbowe anakabiliwa na mtihani wa kuendelea na siasa za kiuharakati kama ilivyo kwa asili ya siasa za chama hicho au
kubadilika na kukubali siasa za kistaarabu na nguvu ya hoja kama anavyotaka aliyekuwa mgombea wao urais, Edward Lowassa.

Kwa mujibu wa habari hizo,
mvutańo wa kiuongozi kwa sasa miongoni mwa vïgogo wa chadewa, unahusu kutafuta kuelekea mwaka 2020, kwa maana kuendelea na siasa za kiuanaharakati au siasa
za kistarabu zinazoelezwa
kulindwa na nguvu ya hoja.

Baadhi ya vigogo wa ndani ya chadema wamewekazi kwamba mwenyekiti wao Mbowe anaumizwa na mambo wawili kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa chama hicho kuelekea mwaka 2020 wa ama kukubaliana na ushauri wa mtu mmoja Lowassa au kukubaliana mtazamo wa waliowengi, wakiwamo wanachama na viongozi wenzake wa asili.

"Hii ndio siri nzito iliyobebwa na viongozi wetu wawili, Mbowe na Lowasa. Mmoja anataka moto wa chadema uendelezwe kama iliyo asili yake, mwingine anataka siasa za kistaarabu katika nchi hii na nguvu ya hoja" anasema kigogo mmoja wa chadewa ambaye hakutaka jina lake litajwe na kuongeza:

"Msimamo wa Mbowe ni kwamba tukifanya siasa
za kistarabu katika nchi hii hatutapata haki zetu za kisiasa, lakini Lowassa anasema haki za kisiasa kwa chama zipo pale pale kwa sababu zinalindwa kikatiba ya nchi na hata kama
hazitatolewa leo, kesho
au ukifika muda muafaka zitatolewa tu.

Kwa maana ya mtazamo huo wa LLowassa, yeye anataka chama chetu kikae tu bila kufanya mikutano ya hadhara na maandamano yenye lengo la kuamsha watu watuunge mkono, baada yake tusubiri kufanya kampeni mwaka 2020.

Chanzo Tazama.
 
Una gene za ulumumba?
Kama huna hao vigogo wa CHADEMA ni kina nani na unaimani na IQ yako?
1998
 
Hiyo "tazama" ni gazeti? Kama ni hilo gazeti hata ukipewa bure nakushauri likatae. Hakuna siasa za CHADEMA ambazo hazijawahi kuwa zisizo na ustaarabu. Siku zote zimekuwa za kistaarabu. Hizi propaganda hazitawasaidieni CCM.
 
Anayechangi Uzi huu kwa kusapoti mawazo ya mtoa hoja, akili zake zinahitaji kubadilishwa
Anayechangia uzi huu kwa kupinga ni vyema akawahishwa Milembe mapema maana hawezi hata kufanya uchambuzi na kujua ukweli wake kwa kuwa kashikiwa akili na wenye chadema.
 
Naona Lusinde kaamua kuja kuvingine humu jamvini.......Mbowe atawapa presha Lumumba.
 
Siasa za nguvu ya hoja kwa nchi kama tanzania zenye watu wasioelewa hazitaleta mafanikio maana hoja inaweza kuhalibiwa na nguvu ya propaganda. Huyo lowasa anaogopa kuwekwa lumande, akumbuke wakati anajiunga kuna mmoja wao alimtahadhalisha kuwa huku ulikokimbilia uwe makini maana kuna mabomu ya machozi na maji ya kuwasha!!Alifikiri utani.

Siasa za harakati ndio siasa nzuri kwa nchi zisizo na wasomi kama tanzania. Maana watanzania wanapenda matukio zaidi.
Lakini!! Halakati zao zisiwe za vulugu, wajalibu kuwaelimisha watu kwa kutumia vipepelushi wa vijarida nk, wawe wabinifu wakubadilisha mbinu za kuwaelimisha watu.

Siasa za hoja ndio zilizoimaliza tlp, na siasa za harakati ndio zilizoiamsha cuf na cdm, ndiomaana hata zito anaenda kiharakati tena ni jeshi la mtu mmoja tu.

(kwa sasa hakuna hoja ambayo lowassa ataitoa kwa watanzania na ikawa na nguvu ya kuibomoa ccm, na ccm wakashindwa kuishidhibiti)
 
Tazama bila.kumuandika Mbowe .....gazeti halijakamilika ,hiv hili gazeti nani analinunua ?
 
Chama cha demokrasia na maendeleo, chadema chini ya Freeman Mbowe, kinakabiliwa na mtihani mkubwa mbele yake unaokitaka kuamua kuanzia sasa muelekeo wa siasa zake.

Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya chama chadema zinasema, Mwenyekiti Mbowe anakabiliwa na mtihani wa kuendelea na siasa za kiuharakati kama ilivyo kwa asili ya siasa za chama hicho au
kubadilika na kukubali siasa za kistaarabu na nguvu ya hoja kama anavyotaka aliyekuwa mgombea wao urais, Edward Lowassa.

Kwa mujibu wa habari hizo,
mvutańo wa kiuongozi kwa sasa miongoni mwa vïgogo wa chadewa, unahusu kutafuta kuelekea mwaka 2020, kwa maana kuendelea na siasa za kiuanaharakati au siasa
za kistarabu zinazoelezwa
kulindwa na nguvu ya hoja.

Baadhi ya vigogo wa ndani ya chadema wamewekazi kwamba mwenyekiti wao Mbowe anaumizwa na mambo wawili kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa chama hicho kuelekea mwaka 2020 wa ama kukubaliana na ushauri wa mtu mmoja Lowassa au kukubaliana mtazamo wa waliowengi, wakiwamo wanachama na viongozi wenzake wa asili.

"Hii ndio siri nzito iliyobebwa na viongozi wetu wawili, Mbowe na Lowasa. Mmoja anataka moto wa chadema uendelezwe kama iliyo asili yake, mwingine anataka siasa za kistaarabu katika nchi hii na nguvu ya hoja" anasema kigogo mmoja wa chadewa ambaye hakutaka jina lake litajwe na kuongeza:

"Msimamo wa Mbowe ni kwamba tukifanya siasa
za kistarabu katika nchi hii hatutapata haki zetu za kisiasa, lakini Lowassa anasema haki za kisiasa kwa chama zipo pale pale kwa sababu zinalindwa kikatiba ya nchi na hata kama
hazitatolewa leo, kesho
au ukifika muda muafaka zitatolewa tu.

Kwa maana ya mtazamo huo wa LLowassa, yeye anataka chama chetu kikae tu bila kufanya mikutano ya hadhara na maandamano yenye lengo la kuamsha watu watuunge mkono, baada yake tusubiri kufanya kampeni mwaka 2020.

Chanzo Tazama.
Mimi nilifikiria umeandika la mbolea kumbe zile PUMBA TALKING ZENU/MBOJO after the STOMACH IS FULL.
Haya kadake mshiko,kakojoe then umbonji shala usiangalie hata nyuma wala kudai nyongeza ya mshaharawa buku 7/day.
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia "try to interrogate your sources before you decide to believe them or not."
 
Chadewa una maana chadema au ni chama kingine kimeanzishwa ndani ya chadema ??
 
Back
Top Bottom