Lowassa, Lissu na Dr. Mashinja Kuwanoa Bavicha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
EDWARD Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatarajia kuhudhuria kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Dodoma, LOWASSATundu Lissu, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni pia Mbunge wa Iramba Mashariki ni miongoni mwa wageni wanaotarajiwa kwenye kongamano hilo ambalo Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema ndio mgeni rasmi.
Kwenye uzinduzi wa kongamano hilo, kutakuwepo na mada tatu ambazo ni nafasi ya vijana katika siasa na hali ya ajira katika taifa ambayo mchokoza wa mada hiyo ni John Heche, Mwenyekiti Mstaafu (BAVICHA) pia Mbunge wa Tarime Vijini.

Mada ya pili itakuwa utawala wa sheria katika Serikali ya Awamu ya Tano ambapo Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini atakuwa mchokonozi.

Mada ya tatu itakuwa wa watumishi wa umma na wanavyuo katika siasa na haki ya kupiga kura ambapo mchokoza mada hiyo ni Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari Manyanya Marambaya Manyanya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Dodoma amesema, vijana hao kwa kushirikiana na Umoja wa Wananchadema Vyuo Vikuu (CHASO) wameandaa kongamao hilo kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana na jamii juu ya mustakabali wa taifa.

Manyanya ameeleza kuwa, kwa sasa katika uongozi wa awamu ya tano kuna sheria nyingi na haki za binadamu zinavunjwa kutokana na utawala uliopo madarakani jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom