Lowassa kuweka kambi Arumeru Mashariki kupangua mikakati yote ya CHADEMA

Duh,Mgombea ni Mkwewe,mwenyekit wa Tume ya uchaguzi ni shemejiiiiiiiii,viongoz wa dini ndo hao wanapigwa 'semina elekez' na mkwe,Sioi akishindwa utakuwa ni muujiza wa kwanza wa kisiasa Tz!
 
Tusubiri matamko ya wazee! Na wachungaji wasipokuwa makini watajikuta makanisa yao yanabaki tupu. That will teach them a lesson.
 
kama ni kweli sioi atatangazwa mshindi'nafikiri keshasoma situation nzima na anajua kinachotakiwa ni pesa peke yake kushinda
 
HABARI ZA KUAMINIKA TOKA ARUMERU.

EDUARD NGOYAYE LOWASSA AJITOSA
RASMI KWENYE KAMPENI ZA SIOI.

Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC CCM Amejitosa rasmi kwenye kampeni za ubbunge Arumeru Mashariki.

Habari za kuaminika zinasema leo ni siku ya Tatu tangu mzee Lowassa ajitose kwenye kampeni hizo za 'mkwewe'.

Tangu juzi alianza kukutana na Wazee wa Mila (Washili) Na jana kakutana na Wachungaji wa
Kipentecoste zaidi ya 120.

Na jana pia akakutana na Maaskofu na
wachungaji wa KKKT.

Na huenda Leo akakutana na Malaigwanan na makundi mengine yote Muhimu.

Ila haijasibitishwa na vyazo vyetu kama ataanza kupanda rasmi jukwaani kwenye wiki ya lala Salama..

Na pia kumeanza mkakati wa kampeni ya
Nyumba kwa nyumba,
Chumba kwa chumba,
Kitanda kwa kitanda,
Na mpaka shuka kwa
shuka.

Habari zaidi mtaendelea kupashwa hapa hapa..

'TANURI LA FIKRA'
'Think twice'

Kama Alishindwa kumuokoa batilda buriani kwa kutumia hizo pesa leo ana nini kipya, anajinunulia presha ikomae iwe stroke labda wale maprofessor wa kijerumani watajipatia fedha halali kuliko ile aliotuambia wanamuangalia jicho ili kujiridhisha.
 
CHADEMA wanatakiwa waongeze majeshi, madhabahu kwa madhabahu.
 
Simpendi Lowassa, lakini siwapendi zaidi chadema kwasababu ya chuki zao kwetu..

so bora hata huyo lowassa
 
juhudi za lowassa arusha hazikufua dafu arusha mjini ngoja tusubiri arumeru ambapo anapambana na cdm na ccm!
 
Eduwadi asimikwe kua asikofu mkuu wa makanisa yoto ya tanzani sababu akuna askofu anae subutu kunyenyua mdomo juu yake.amekua akitoa pesa alie ibia wavuja jasho makanisani na madrii na wachungaji wakua wakipokea,bila kumwambia lelote,pia wata tumika kumchagua mtu wasie mpenda kwakuhongwa pesa ambazo wameibiwa wavuja jasho wakitanzia,kweli atufiki kama adi viongozi wa dini watatokwa imani kiasi ichi,tulitegemea wao ndio watakemea maovu,chaajabu wametusaliti.EWE MWENYEZI MUNGU TUANGALIE WATANZANIA.
 
Arumeru hakuna msikiti

Mkuu Mungi,
Vipi tena si ulisema kapigwa marufuku na Nape, kufika Arumeru ukaleta na ushahidi wako!

Jamaa ndio kaishafika Arumeru na leo alikua na Ole Sendeka, wakiongea na wazee wa kimila.

Wamasai na Wameru wanacheka cheka tu walivyomuona Lowassa.
 
Simpendi Lowassa, lakini siwapendi zaidi chadema kwasababu ya chuki zao kwetu..

so bora hata huyo lowassa

Kiongozi Topical, signature yako inasomeka hivi: "Mbowe for Presidency 2015"". Sasa soma hapo kwenye red kwa pamoja na hiyo signature! baridi au moto?
 
Wanabodi.
Habari za uhakika ambazo zimethibitishwa na marafiki wa Lowassa, zinasema mbunge huyu wa Monduli amejipanga kuweka kambi Arumeru Mashariki katika wiki ya mwisho ya lala salama ya kampeni.

Hilo litakuwa kombora la mwisho la kuimaliza Chadema huko Arumeru Mashariki.

Kwenda kwa Lowassa, Arumeru ni wazi njia itakuwa ni nyeupe kwa mgombea wa CCM, Sioi kutokana na umahiri wa mwanasiasa huyo, si tu katika kuratibu kampeni, bali hata kukubalika na kuheshimiwa na wananchi wa jimbo hilo jamii ya Kimasai na Wameru.

Inasemekana Lowassa ndio alikuwa akiratibu kampeni za kila siku mgombea wa CCM.

Kwa mujibu wa makada wa Chadema waliopo Arumeru wanasema hata kabla ya ujio huo wa Lowassa, Chadema kimekuwa kikikumbana na upinzani mkali kinapojaribu kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kutokana na wananchi jamii ya Wamasai na Wameru kuwagomea si tu kuingia ndani ya nyumba zao kwa ajili ya kampeni, bali hata kuwasogelea.

Lowassa akifika Arumeru Mashariki si ndio itakuwa balaa kwa Chadema.

Jipime mwenyewe na ujirekebishe kabla hujawa unreliable.
 
Back
Top Bottom