Lowassa kuvuliwa cheo cha uzee wa ukoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa kuvuliwa cheo cha uzee wa ukoo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jan 20, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  ALIYEWAHI kuwa waziri mkuu Edward Lowassa huenda akavuliwa cheo cha ukuu wa kimila (Olaigwanani) na ukuu wa `malaigwanani baada ya jopo la wazee wa kimila kukaa vikao na kupanga siku ya kumuita na kumvua cheo hicho kikubwa kwa mila za kimaasai.


  Wazee hao ambao wamekaa katika vikao mara tatu kumjadili, walikuwa wakijadili juu ya Mbunge huyo wa Monduli kupewa cheo kikubwa `ukuu wa malaigwanani``cheo ambacho walidai kuwa hakipo na kwamba hata walipompa cheo hicho walikiuka miiko ya kimila.


  Ilidaiwa ya kuwa katika mila ya kabila la kimaasai kuna cheo cha Olaigwanani na pia

  cheo cha uzee wa `Boma` na kitendo cha Lowassa kupewa cheo cha ukuu wa `Malaigwanani ` kimewashangaza wazee hao.


  Katika kikao kilichofanyika Monduli Januari saba mwaka 2009 kuanzia saa tano

  asubuhi mpaka saa tisa alasiri, jopo la wazee hao lilijadili taratibu za Lowassa

  kupewa cheo hicho na kwamba waligundua mapungufu ikiwa ni pamoja na kutokupewa taarifa kwa wazee wote wenye vyeo ya kimila.


  Walidai yakuwa awali kabla ya kusimikwa kuwa mzee wa ukoo (Olaigwanani) taarifa

  hupelekwa kwa katibu wa ukoo na pia taarifa hizo husambazwa kwa wazee wote Afrika Mashariki na kuchinjwa kwa mbuzi dume sita na pia msimikwaji awe Mmasai halisi kitu ambacho walidai wana mashaka na kabila lake.


  Pia wazee hao katika mukhtasari wa kikao chao walisema kuwa katika mchakato mzima wa kumpatia Lowasa ukubwa wa wazee wa ukoo ni batili na kwamba mwezi Februari mwaka 2009 wataandaa mkutano mkubwa wa kimila akiwamo Mbunge huyo na kuangalia taratibu za kumvua cheo hicho na kwamba ikibainika ni Lowassa anapaswa kupewa cheo hicho atapewa.


  Pia wazee hao walisema kuwa kama kweli Lowassa alipewa cheo hicho kwa haki na

  taratibu zote alipaswa kusuluhisha mgongano ulitokea kati ya mbunge wa Simanjro

  Christopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya.


  Akizungumza kwa njia ya simu saa tatu na dakika 20 asubuhi, mbunge wa Monduli Edward Lowassa alisema kuwa hawezi kuanzisha malumbano katika magazeti na yote

  atakayoyasikia yeye atakaa kimya.


  "Mimi nimekusikia ndugu mwandishi kwa yote uliyonieleza na kuniuliza,lakini kwasasa sipo tayari kuzusha malumbano magazetini, nakaa kimya, muandike msiandike mimi sintojibu kitu,"alisema Lowasa .
   
 2. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #2
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakati akiwa PM suala la Ukabila wake halikuwepo,
  sababu ni utaratibu, ukabila, Sendeka vs millya au kuna kingine?
  OBAMA vs OSAMA kwa WATZ na WAKENYA
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamii ya Kimasai hasa wazee wa Mila wamestushwa na vurugu mbalimbali zinazotokea katika jamii hiyo na hivyo kuona kuna haja ya kumvua uongozi wa mila hiyo Mbunge wa Monduli Mh.Edward Ngiyai Lowassa ambaye hata hivyo ni wa kabila la wameru.Tangu apewe cheo hicho kumekuwa na magomvi mbalimbali tofauti na maana ya nafasi hiyo ambapo mhusika hutakiwa kuleta mapatano katika jamii.Mfano ugomvi wa Ole Sendeka na Millya kiongozi huyo alitakiwa asuluhishe ugomvi huo kwani ndiye aliyeitisha kikao kilizaa ugomvi huo lakini alikataa kwa kusema hawezi kuingilia jibu hilo moja kwa moja ni kielelezo cha kushindwa kazi hiyo kwani itamaanisha kuchochea ugomvi huo badala ya kupatanisha wahusika.Maana ya Laiguanani na kazi zao wa JF mnaofahamu mtufahamishe.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hawa wazee wanachanganya mila na siasa...hawana issue kabisa.
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  je angeendelea kuwa waziri mkuu angevuliwa hicho cheo? wazee walikuwa wanajipendekeza wakati Lowasa akiwa juu!!!!
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kumbe ni "huenda," lakini kwenye kichwa cha habari umetuambia "Lowassa kuvuliwa cheo..."

  "Kupanga siku ya kumvua," halafu baadae chini utakuja kutuambia wakikuta cheo ni halali wanaweza wasimvue...!

  Hao wazee wamesema waliompa cheo hicho ni kina nani? Ni wao peke yao ndio wana nguvu ya kuvika na kuvua? Kama sio wao peke yao, maana kuna wengine walimvika, je wana haki ya kumvua? Vipi wale wakija tena wakamvika? Kwa standards za hao original wazee wengine?

  Wameanza kushangazwa kuanzia January 7? Bada ya muda wote wa kushika cheo hicho ni nini kime trigger the change of heart, kuna mzee alileta hoja binafsi?

  Atapewaje cheo batili?

  Agenda ya mkutano mkubwa wa February umetuambia ni kuangalia taratibu za kumvua. Halafu hapo hapo unasema kama anapaswa kupewa cheo hicho atapewa. Cheo batili!

  "Kama Mugabe angekuwa amechaguliwa kwa mujibu wa taratibu za kikatiba angekuwa ametatua tatizo la kipindupindu na mfumuko wa bei"!

  Hai make sense, right?

  Basi waulize hao wazee haya maswali utuletee news report inayo make sense!!!!!!!

  Ngongo unanukuu maneno yale yale ambayo hapo hapo umeyatasfiri kwa maneno yale yale!

  Mkuu wa Ukoo Lowassa we kaa kimya, ni poa tu, maana ki-stori chenyewe haki make sense, na hao wazee wako wamesha lose their marbles. Cheo chako Lowassa walichokupa inawezekana ni poa tu.

  [​IMG]
   
 7. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazushi tuuu hao, mbona nasikia hata hicho kikao walichokaa wamefadhiliwa na the same dude, EL. Waseme kwamba wanataka kwenda kuongea nae kuhusu yatakayojiri 2015
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Eee bwanaee, inaelekea maji huteremka bonde, na Edo anateremka kwa kasi ya ajabu!
   
 9. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hebu vuteni kumbukumbu zenu. Alipewa cheo hicho baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu kama sehemu ya ule mkakati wa kumsafisha niliouanika hapa JF. Lakini alipewa na kikundi cha watu wachache, sasa Sendeka na Mengi wanaanza kuiibua tena hii ajenda ya kumvua.

  PM
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Siasa ya TZ inakoelekea sio kuzuri, haya mambo yote ni kuelekea uchaguzi wa 2010. Itafikia wakati tunashughulikia na kuangalia chaguzi tu, badala ya kuangalia maendeleo ya nchi yetu.
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kwi kwi kwi kama hili ni kweli basi umaskini hauna aibu. Yaani wamefadhiliwa na EL ili wakae wamjadili EL...hii kali...only in Tanzania.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  No hawajafadhiliwa na EL, watakuwa wamefadhiliwa na Ole Sendeka baada ya kuvuta fungu toka kwa Ole Mangi. Hii ni kampeni ya Ole Mangi kumtokomeza Ole Ngoyayi kwa vile anamtetea Ole Milia kukitia mchanga kitumbua cha Ole Sendeka.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Siasa bwana kaaaazi kweli kweli, wadau wakijua umerosto kisiasa,hata panya wanachezea sharubu!
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawakujipendekeza bali walishawishiwa na fedha za Lowassa kwani si Mmasai halisi.Ubunge wa Monduli anaweza kugombea yeyote kama alivyowahi kugombea Mikidadi Mohamood lakini Olaiguanani wa wamasai lazima awe mmasai halisi hivyo kigezo kilichotumika kumpa Lowassa cheo hicho ni cha kisiasa zaidi kuliko kigezo cha kijamii(Mmasai halisi).
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunapochangia tujikite katika uhalisia,aliyeitisha kile kikao cha mila na kukifadhili ni nani kama si Lowassa,mbona watu walipogombana kwenye kikao alichoitisha anakataa kusuluhisha eti kwamba haingilii ugomvi,sasa maana na cheo alichokikubali ni nini kama si usuluhishi katika jamii.Suala lililoongelewa kwenye kikao ni mambo ya ardhi,mbona Lowassa hakusikika akiwasaidia wamasai kuhusu ardhi alipokuwa Waziri Mkuu na mbona enzi hizo ndio kulikuwa na magomvi mengi ya ardhi Monduli na katika jamii ya wamasai kwa ujumla.Mfano Ngorongoro,Serengeti na zingine nyingi.Ole Millya ni kijana mdogo sana kwa umri ukilinganisha na Ole Sendeka na Laiguanani wanatakiwa kuhimiza heshima hasa kwa wadogo kuheshimu wakubwa sasa mbona Lowassa hakukemea Ole Millya kumbeza Ole Sendeka tena mbele ya wazee.Kama ingefuatwa mila za kimasai Ole Millya hafai Uongozi wowote kwa kuwa hana adabu ila ni mpayukaji kwa wakubwa zake tena kwa kusema uongo.Ukifuatilia historia ya Ole Millya tangu Tumaini University utabaini mengi zaidi.
   
 16. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Dhamana ya kiongozi wa dola ina mipaka na heshima kuu kwa wote, ole sendeka alipo abuse dhamana hiyo tena hadharani anapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika ambayo ni sheria ya nchi, ole sendeka hakumtandika millya kwa sime au fimbo ya kichungaji ktk ngoma ya asili bali ktk mkutano uliowahusisha watu wa kada zote ktk himaya ya umasaini, kiongozi anaapa kulinda sheria za nchi halafu anazivunja hadharani tumchekee!!!
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Hivi Lowassa kumbe ni Mmasai? Sikujua hilo!
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  huyo ndiye aliyerithi kiti cha ubunge cha Sokoine.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,258
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  njaa zinawaua
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu FM,
  Nadhani kuwa kiongozi kwa jamii ya kimasai si lazima uwe mmasai sana sana unatakiwa uwe na pochi la kutosha.Tumeshuhudia hata mmachame R Mengi akizawadiwa cheo cha Olaigwanani.
   
Loading...