Lowassa kutumia sh bilioni 70 kujenga gorofa 25 Dar City Centre!

Kwa mujibu wa gazeti la DIRA la leo toleo la Novemba 29 - Desemba 5, 2010, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, amebomoa jengo la kihistoria la Nyumba ya Sanaa pale karibu na Movenpik Hotel Dar city centre na sasa atajenga gorofa 25 kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mradi huo utagharimu dola za kimarekani $45.5 million, sawa na takriban shilingi bilioni 70!.

Mradi huo wa jengo unajengwa kupitia kampuni ya Lowassa inayoitwa Integrated Property Investment (Tanzania) Limited.

Kuna tuhuma kuwa huu ni mradi wa kifisadi. Wasanii walilalamika mpaka Ikulu kwa Kikwete kujaribu kuzuia Nyumba ya Sanaa isivunjwe na kampuni ya Lowassa wakashindwa.

Kampuni hiyo ya Lowassa ndiyo iliyohusika na kashfa ya kununua nyumba huko London kwa karibu shilingi bilioni 1. Kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA la wiki iliyopita, mtoto wa Lowassa, Frederick, anachunguzwa na polisi wa Uingereza kutokana na kashfa hiyo.

* Je, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa civil servant ametoa wapi 70bn/- kujenga gorofa hilo?

* TAKUKURU inasemaje kuhusu utajiri wa kutisha wa PM huyu wa zamani haswa baada ya yeye kuhusishwa na ufisadi wa Richmond na baadae TAKUKURU kumkosha?

* Huyu ndiye mtu anayetaka kuwa Rais baada ya Kikwete 2015 "by any means necessary" kwa kushirikiana na Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Manji, Yusuf Makamba, Kingunge Ngombale Mwiru, etc. Nchi hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itapona kweli?

Bla bla bla, bla bla bla. Jee uliwahi kujiuliza utajiri wa Mbowe aliupataje?
 
Wana JF mbona tunakuwa wasahaulifu kiasi hiki? Lowasa kapata wapi fedha!!!! Je hamkumbuki zile 256 m kwa siku kwa zaidi ya miaka miwili ya RICHMONDULI? Inasikitisha ,sasa anataka kuzipa uhalali kwa kuziwekeza kama vile ni fedha safi na halali.
Angalieni msipoteze kumbukumbu.Waliowageni humu,aidha kwa kuelewa ama kwa kutoelewa msitupotezee ukweli.
Mbwa mwindaji hapotezi harufu.
Hivi TRA wanaweza wakaonyesha kodi ktk makampuni ya Lowasa inalipwaje, huenda pia halipi maana ni tabia yao hao.
 
Njimba Nsalilwe So my Dear Tanzanian we encourage people to invest in TZ with corrupt and thieved monies!! Are you serious. Hatuna shida na kuinvest TZ but the source this income. Sio mtu anaibuka eti anawekeza Tanzania shamba la bibi. Atupe source ya this exobitant cash reserve,from which bank, company,financial inst, NGO AND THE TYPE OF BUSINESS.
For what period of time,to aquier that type of whealthy. Hivi TAKUKURU wako wapi, wana kazi gani????
Mbona vitu vingine viko wazi.Jamani tuwe na katiba mpya ili tuwe na Lumumba wetu TZ!!! Waulize Ndg zetu wa Kenya(INTEGRITY CENTER KUNA LUMUMBA MOTO UNAWAKA).
 
Last edited by a moderator:
Me sijui hizi taasisi zetu kama pccb zinafanya kazi gani wkt kazi wanazopaswa kufanya kama hii hawazifanyi..! Wao wanasubiri tu wasikie mtu kaajiriwa juzi after three month kanunua vits wanaanza kumfuatilia hasa wa huku kwetu vijijini kumbe kakopa benk....! kwa mtu kama huyu ambaye maisha yake yote amekua civil servant haiwezekani kuwa na hela au dhamana ya kukopea 70b hata kama angekua kalipwa kiinua mgongo chake na tunajua bado hajalipwa...! hahahaa kweli hii inachekesha sana na kusikitisha hasa wakina hosea jinsi walivyo kimya na ambavyo wako tayari kumtetea kwa any costs...! its gud ameamua kuinvest bongo but its really disturbing kuaona huyu muheshimiwa anaendelea kutuibia na tunakaa kimya tu kama hamna kinachoendelea...!:whoo:
 
wacheni ajenge tu! Atatoa ajira na kuchangia kodi. Si Kama Chenge aliyehamishia nje
 
Hivi kwa nini hwa viongozi hwatki kuwekkeza kwenye kilimo kufanya hayo mapinduzi ya kilimo. Jibu Jepesi ni kuwa hizo pesa za Rich Man of Monduli ni Mkopo.

Sumaye alionyesha mfano watu wakampinga. Sasa uti wa mgongo Taifa letu umebaki kuhubiriwa bungeni. wenye mapesa wanataka kujenga tena kujenga dar london na geneva.

Kwa nini hii kilimo kwanza isiwahamaishe hawa aviongozi wawe na mashamba ya mifano.

Any way wayalete tu hayo magorofa.
 
Every day wananchi wanaona madudu mengiiiiiiii, we are like this now :A S-confused1::A S-confused1:
muda si mrefu tutakosa wote :smash::frusty::grouphug::A S-danger::A S-danger:
 
definatelly kwa mradi mkubwa kama huo ni benki.........

sasa jamani whats a big deal.....kama mkataba unaonesha perfoming theatres zitakuwa restored tena kubwa .....na wasanii wakaweza kuwa na stalls za kuonesha vitu vyao....tuacheni mawazo mgando!!!....nadhani pia board of trustee wa nyuma ya sanaa wamemshirikisha yule mama wa ki nordic aliyejenga lile jengo na kumkabidhi mwalimu...

tuacheni kuwabana watu wanapoamua kuwekeza pesa zao......nyie ndio mnafanya watu wanaenda kuwekeza ulaya......au south afrika.....waacheni wawekeze hapa..ili turudishe pesa yetu kwenye kodi na ajira...

Kaka nakuamini lakini hii vita hatutashinda kama tutawapongeza watu kwa kutuibia na kuja kuwekeza nchini. Utetezi nitakaokubaliana nao ni jinsi gani wamepata mtaji mkubwa kiasi hicho, je ni Alphatel tu walioinua mtaji wao? Vyombo vya dola viangalie na kujiridhisha si watu kama wewe na wengine humu JF kuhalalisha kiongozi ambaye amefikia ngazi ya Uwaziri Mkuu na akahusishwa na kashfa akawekeza na tukamuita mwekezaji, hii HAIKUBALIKI KABISA JAMANI musitake tukasema mengi humu. Kuna mambo ambayo lazima tukubaliane, mfano Lowassa alikuwa anaendesha Corolla Dodoma akiwa Mbunge, sasa huu utajiri wa ghafla ameutoa wapi?
 
So my Dear Tanzanian we encourage people to invest in TZ with corrupt and thieved monies!! Are you serious. Hatuna shida na kuinvest TZ but the source this income. Sio mtu anaibuka eti anawekeza Tanzania shamba la bibi. Atupe source ya this exobitant cash reserve,from which bank, company,financial inst, NGO AND THE TYPE OF BUSINESS.
For what period of time,to aquier that type of whealthy. Hivi TAKUKURU wako wapi, wana kazi gani????
Mbona vitu vingine viko wazi.Jamani tuwe na katiba mpya ili tuwe na Lumumba wetu TZ!!! Waulize Ndg zetu wa Kenya(INTEGRITY CENTER KUNA LUMUMBA MOTO UNAWAKA).

Hey my dear Tanzanians, let us face it!

Nchi hii imepoteza dira hili inabidi tulikubali. Sheria hakuna hapa!
Ngoja niwaulize swali moja, Mzee wa Visenti, ametamka hadharani kuwa ana haki ya kumiliki vihela kidogo na hakuna mtu aliemuuliza amezipataje! Leo hii mnapoteza muda hapa wa kujiuliza eti Lowassa amepata wapi hela? Mbona mnashangaza?

Ok! Kesho Lowassa akitoka na kusema nae ana haki ya kumiriki hela mtamfanya nini? Chenge mmefanya nini?

Let us face it, nchi imepoteza heshina ya good governance, viongozi wetu ni matajiri wa kupindukia na hakuna sheria inayowabana. Hayo maswali yatunzeni mpaka mtakapo pata serikali ya ukweli. But for now let us give credits for those who decide to invest in our own country. Angalau tukipata mtu makini atawauliza walizipataje!

There are more than one way of skinning a rabbit!

Philemon Michael, amewaambia kuna viongozi wamedhurumiwa mali zao nje ya nchi kwa unafiki huu huu toka kipindi cha awamu ya kwanza. Walihubiri ujamaa lakini mali wanaficha nje. Wajanja wakawazidi.

Waacheni wazilete. Siiku moja zitarudi serikalini.

ONLY WHEN YOU AND I WILL DECIDE TO VOTE WISELY!
 
Watanzania tunamalizana wenyewe tunawaachia wageni wantamba kwenye uchumi...........that is being hypocrtic at the highest level.....chukulia mfano Pale kuna Invester anajenga uhuru peak ...ghorofa 30...wale jamaa walikuja hapa wakaaza kununua pamba ....kwa kukopeshwa na benki ...wakajenga maviwanda ..sasa wamepata mkopo nje na ndani na pesa zao wanajenga lile ghrofa refu kuliko yote tz.......so kwa kuwa ni wahindi ...no body cares....
wengine wamekuja wakimbizi toka somalia ...tumewapa mitaji haapa hapa ...wameinuka..,tatizo pesa akiishika mbantu ..kila mtu ana haha....tuacheni utumwa wa fikra!!!!.......naamini kabisa kwa mradi wa size ya nyumba ya sanaa na kwa dunia ya leo ..yenye intergrated actions against ufisadi lazima ni mkopo...tu!!!...na kama ni mkopo sioni ajabu!!!!

kwenye nchi za wenzetu you can own any asset you want kupitia mkopo ..ili mradi uwe na defined repayment strategies and plans!!

Hata wewe mpambanaji Phillemon Mikael tunakujua kila siku unapingana na ufisadi leo hii unaunga mkono kitendo cha civil servant kuwekeza kwenye mradi wa 70bn/-? Kiongozi wa umma anapata wapi pesa hizi? Si suala na uhindi na uzawa, ni suala la maadili ya uongozi wa umma. Huyu Lowassa kawa tajiri mkubwa sana kwa haraka akiwa ndani ya serikali. Kuna biashara gani alifanya akiwa waziri wa ardhi na baadaye waziri mkuu? Hebu tufahamishe
 
Kaka nakuamini lakini hii vita hatutashinda kama tutawapongeza watu kwa kutuibia na kuja kuwekeza nchini. Utetezi nitakaokubaliana nao ni jinsi gani wamepata mtaji mkubwa kiasi hicho, je ni Alphatel tu walioinua mtaji wao? Vyombo vya dola viangalie na kujiridhisha si watu kama wewe na wengine humu JF kuhalalisha kiongozi ambaye amefikia ngazi ya Uwaziri Mkuu na akahusishwa na kashfa akawekeza na tukamuita mwekezaji, hii HAIKUBALIKI KABISA JAMANI musitake tukasema mengi humu. Kuna mambo ambayo lazima tukubaliane, mfano Lowassa alikuwa anaendesha Corolla Dodoma akiwa Mbunge, sasa huu utajiri wa ghafla ameutoa wapi?

Mkuu,

Kwa sasa hatuna ujanja, inabidi tujipange mpaka pale tutakapo kuwa na uwezo wa kuwajibisha.
Tunapopiga kelele hazisaidii hata wale wanaotaka kuzileta hela zao wanakaa kimya.

Maboutu alificha hela nyingi sana nje, leo amekufa zimebaki huko huko! Je angeitwa FISADI na akajenga majumba na mabenki ZAIRE, je yasinge kuwepo leo?

Think wise GREAT THINKER! KNOW YOUR STRENGTH AND WEAKNESS kabla hujaa pambana na mtu.

NN
 
You are missing the point my friends. Is Lowassa a civil servant au multi-million dollar investor? Surely, he can't be both! The overriding question is, where does a person who spent all his career working as a civil servant get the money to invest in a $50m project? How can a civil servant afford to buy a 1 billion shilling apartment in the UK?

Have you tried getting a bank loan lately? Even if you have the best writtten business plan, they won't loan you even $100,000 let alone $4.5 million. You need to have some serious cash flow and millions of dollars in your name to get such kind of a loan.

This is a major scandal!

Kwa hili nimekugongea thanks!
 
The fact that has decided to invest in Tanzania, I think he should be credited for that. There are many Tanzanians who are going to be employed up there. If there is a contract between Nyumba ya Sanaa and his company, what is the problem? After all, he has not changed the use of the area only improved!

Hey, Tanzanians, let us encourage our own people to invest in Tanzania. It is for the benefit of all Tanzanians.

Do you want him to invest elsewhere?
Yale yale ya kuibiwa 10M na mwizi akaja kukupa pole ya 1M unaanza kumwona mwizi ni mwema.............Lol........JF ze grit thinker...........!!!! Nina mashaka na wewe
 
I am suprised there are people in this forum supporting Edy. The question is where did he get this money? Its not the matter of investing in Tz is the matter of how clean is the money invested in Tanzania? We dont want investors with dirty money.
 
Kwa mujibu wa gazeti la DIRA la leo toleo la Novemba 29 - Desemba 5, 2010, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, amebomoa jengo la kihistoria la Nyumba ya Sanaa pale karibu na Movenpik Hotel Dar city centre na sasa atajenga gorofa 25 kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mradi huo utagharimu dola za kimarekani $45.5 million, sawa na takriban shilingi bilioni 70!.

Mradi huo wa jengo unajengwa kupitia kampuni ya Lowassa inayoitwa Integrated Property Investment (Tanzania) Limited.

Kuna tuhuma kuwa huu ni mradi wa kifisadi. Wasanii walilalamika mpaka Ikulu kwa Kikwete kujaribu kuzuia Nyumba ya Sanaa isivunjwe na kampuni ya Lowassa wakashindwa.

Kampuni hiyo ya Lowassa ndiyo iliyohusika na kashfa ya kununua nyumba huko London kwa karibu shilingi bilioni 1. Kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA la wiki iliyopita, mtoto wa Lowassa, Frederick, anachunguzwa na polisi wa Uingereza kutokana na kashfa hiyo.

* Je, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa civil servant ametoa wapi 70bn/- kujenga gorofa hilo?

* TAKUKURU inasemaje kuhusu utajiri wa kutisha wa PM huyu wa zamani haswa baada ya yeye kuhusishwa na ufisadi wa Richmond na baadae TAKUKURU kumkosha?

* Huyu ndiye mtu anayetaka kuwa Rais baada ya Kikwete 2015 "by any means necessary" kwa kushirikiana na Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Manji, Yusuf Makamba, Kingunge Ngombale Mwiru, etc. Nchi hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itapona kweli?

Kwenye blue
Wawekezaji wanaokuja Tanzania kuwekeza hawaji na magunia ya pesa, pesa ziko benki zimejaa tele; jifunze kibuni na kuandika miradi utapata mkopo wa kugharamia mradi wako
 
Back
Top Bottom