Lowassa kurejea CCM: CHADEMA imepata penati dakika za lala salama!

Kwahiyo unataka kutwambia kuwa baada ya lowasa kurudi ccm ufisadi umeondolewa na mahakama ndiyo maana mmempokea?
Huyu ambaye alisema lowasa ni fisadi kisha akasema sio na anafaa kuwa rais ambaye tena ni wazi sasa hivi anaenda muita ni fisadi?
Mnyika anatakiwa apewe chama yeye. Ndio mtu pekee aliyeonyesha kuwa hakufurahishwa na ujio wa lowassa ndani ya chadema.

In God we Trust
 
Lissu anafaa kuwa rais wa kudumu wa Tanzania
Hapo ndipo mnapokosea - si wakati wa kusema apige nani - huyu mnayempigia debe TL ikitokea baada ya matibabu akaamua kuhamia CCM si mtakuwa mmekwaa kisiki tena?

What so important kwenu ni kujenga taasisi imara yenye falsafa makini kisha watu wakione CDM kama chama chenye nia ya kushika dola badala ya kuendelea kuwa chama chenye lengo la kulipiza visasi - LISSU Hafai kuwa Rais kamwe!!

In God we Trust
 
CCM wanatumia hila za Simba Sport Club, huwa wanamchukua mchezaji anayewafunga, hivyo wanaona Lowasa atawapa taabu wameamua kumsajili hata baada ya kutangaza kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Lakini Lowasa hana cha kupoteza ndani ya Chadema kwani ndoto yake ya kuwa raisi anaiona haitimii na kiuchumi kakabwa koo, bora arudishe majeshi chamani. Siasa za vituko zinawafanya watu kukosa imani na kila mwanasiasa, kwa hiyo kila mtu na akili yake tusiwe washabiki damu wa kuwapigania wanasiasa, huwa wanageuka kuliko kinyonga.
Tunaomba siasa iwe miongoni mwa michezo inayoshindaniwa kwenye Olimpic.
 
Bao la mkono la Diego Maradona lilifuatiwa na bao bora kabisa kuwahi kufungwa na mkongwe huyu. Aliwapiga chenga defense nzima ya timu ya uingereza kabla ya kufunga goli.
giphy-5.gif

Mabeki waCCM watabaki wanakimbiiza Mwenge
 
Mpiga penati wa chadema ni Mbowe tu hata 2015 yeye ndio alipiga
 
Uko sahihi sana, CDM wakichanga karata vizuri wanaweza kufanya kitu kitakachoitetemesha CCM.
Na bahati mbaya na ukweli ni kuwa, siku zote maximum achievement yao inakuwa ni hiyo, “Kutetemesha CCM”.
 
Huyu ambaye alisema lowasa ni fisadi kisha akasema sio na anafaa kuwa rais ambaye tena ni wazi sasa hivi anaenda muita ni fisadi?
Mnyika anatakiwa apewe chama yeye. Ndio mtu pekee aliyeonyesha kuwa hakufurahishwa na ujio wa lowassa ndani ya chadema.
Bahati mbaya kwako umekutana na waelewa ngoja nikueleze ili ujue unaongea na watu wa level zingine ni hivi kazi ya wapinzani/Wenye mawazo mbadala ni sawa na kazi ya mshika kibendera kwenye mpira wa miguu anamsaidia refa kama Kuna sehemu refa hajaona faul, wapinzani walinyosha kibendera kuashiria Kuna tatizo (faul) lakini refa (serikali) ikapeta/ikapuuza na unajua refa(serikali) ndiye mwamuzi wa mwisho sasa ulitaka wapinzani wafanye nini?
 
Bahati mbaya kwako umekutana na waelewa ngoja nikueleze ili ujue unaongea na watu wa level zingine ni hivi kazi ya wapinzani/Wenye mawazo mbadala ni sawa na kazi ya mshika kibendera kwenye mpira wa miguu anamsaidia refa kama Kuna sehemu refa hajaona faul, wapinzani walinyosha kibendera kuashiria Kuna tatizo (faul) lakini refa (serikali) ikapeta/ikapuuza na unajua refa(serikali) ndiye mwamuzi wa mwisho sasa ulitaka wapinzani wafanye nini?
Utetezi mbovu sana huu.
 
Kwakuwa siupendi unafiki, nakiri kufarijika na kitendo cha Lowassa kurejea CCM Jana. Nilikuwa kati ya watanzania Wa mwanzo kupinga kitendo cha Lowassa kuhamia CHADEMA. Sikupinga wala sasa sifarijiki kwakuwa ni mwanachama au mshabiki Wa CHADEMA.Sikuwahi kujiunga na chama chochote cha siasa hapa Tanzania au kwingineko.

Lakini, natamka wazi hapa kuwa Mimi ni muumini Wa demokrasia ya ushindani na ya kushindana kwa hoja. Furaha yangu wakati wote ni kuona kuna chama tawala imara na vyama vya upinzani imara. Watawala wakiwa imara na wapinzani dhaifu, kutakuwa na tatizo. Halikadhalika, upinzani imara unapaswa kuendana na watawala imara.

Sijifichi kusema kuwa Lowassa, tangu ahamie CHADEMA 2015,amekuwa kigingi cha ustawi Wa chama hicho. Kujiimarisha kwake kulikuwa kila kukicha kitisho kipya kwa CHADEMA. Nilikuwa nasikitika na kuisikitikia Sana CHADEMA ikizingatiwa kuwa ndio viongozi Wa wapinzani nchini. Yaani, CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani.

Kuondoka kwa Lowassa CHADEMA ni fursa adhimu kwa chama hicho kujipanga upya na kujiimarisha vya kutosha. Ni Kama kupata penati wakati Wa dakika za nyongeza. Lowassa Si mwanasiasa Wa kitaasisi. Yeye hujijenga na kujiimarisha binafsi.

Kazi kwenu CHADEMA, mkipaisha mmekwisha!

Leo umetoa point, endelea hivyo hivyo
 
Cha msingi hapa ni chama kujipanga na kuweka mikakati ya ushindi mapema ,Mungu kawapa cdm golden chance ,washindwe tu kuitumia jiwe kabugi step once more .
 
Back
Top Bottom