Lowassa: Kuna jitihada kubwa sana za kudhoofisha upinzani, lakini hawataweza 2020 watakaa pembeni

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Waziri mstaafu Edward Lowassa anaamini kwamba kuna kila namna inayofanywa na watu fulani ili waweze kuua kabisa upinzani hapa nchini Tanzania, pia ameongeza kwa kusema kwamba Tanzania ni wakati wa kusimia haki zetu.

Akiongea na watu wa moshi mjini Lowassa amesema kwamba pamoja na mambo yanayoendelea na wanayofanyiwa katika kipindi hiki pia na swala zima la kunyiwa kiwanja cha mashujaa na badala yake kupelekwa viwanja vya Majengo, lakini anaamini kwamba shughuli nzima ya kuuaga mwili wa Mh Ndesambuo umeenda vizuri na kumpumzisha katika nyumba yake ya milele.

Mwaka 2020 ni mwaka wetu na tushinde hata kama wanataka kufanya kila njia ya kudhoofisha upinzani
In Lowassa Voice..

Amewashukuru pia mchungaji Gwajima na waziri mstaafu Fredrick sumaye kwa kuongelea swala hilo na kuwahakikishia moshi ushindi mwaka 2020 (Uchaguzi Mkuu)

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu Chadema ambaye bado anaamini kwa mara nyingine tena ifikapo mwaka 2020 atapitishwa na chama chake cha Chadema kugombania urais.
 
Katika upinzani uliokufa ni wa TZ..,,

Mzee pumzika acha vijana wenye nguvu na ndoto zao wazifanikishe,, Huu ni muda wako wa kula mafao sio kuhangaika na vijana wa CDM., Wenzako kina Mnyika magoti yao yamzoea virungu., It was'nt your fate to be PREZIDER big boy......!!!

Kwa nini usiwe mshauri wa mawazo tu babu yangu..?? Utafia barabarani nakuhurumia mzee wangu si nia yangu kukuponda.
 
Huyu mzee hajui kuwa upinzani ameuzoofisha mwenyewe!

CHADEMA ya sasa sio ile CHADEMA ya wakati hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA.

CHADEMA ya sasa imebakiwa wapiga kelele tupu badala ya watenda vitendo sahihi.

CUF ya sasa haijulikani Mwenyekiti wa taifa ni nani?

NCCR-Mageuzi imebaki na Mbatia na ofisi yake huku msuguano wa viongozi ukizidi kuitafuna.

ACT-Wazalendo inapukutika polepole.

UDP haina Katibu Mkuu.

Vyama vingine vimebaki kwenye mikoba ya wenyeviti.
 
Huyu mzee hajui kuwa upinzani ameuzoofisha mwenyewe!

CHADEMA ya sasa sio ile CHADEMA ya wakati hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA.

CHADEMA ya sasa imebakiwa wapiga kelele tupu badala ya watenda vitendo sahihi.

CUF ya sasa haijulikani Mwenyekiti wa taifa ni nani?

ACT-Wazalendo inapukutika polepole.

UDP haina Katibu Mkuu.

Vyama vingine vimebaki kwenye mikoba ya wenyeviti.
Ni kweli mkuu
 
Sehemu kubwa ya Shughuli za Msiba ilikuwa Kampeni ya Uchaguzi 2020 badala ya kumuomboleza Mzee Philemon hii sio sawa nilikuwa natazama hata kwny Media hata coverage kubwa walipewa wanasisa badala ya Wafiwa
 
Lowasa na Sumaye watuambie walifanya nini tusiibiwe madini yetu,maana katika tawala zao ndipo misingi ya wizi huu ulifanyika tumeachiwa mashimo na kuhangaika na mchanga. Lowasa ndio ameua upinzani kabisa,haridhiki na utajiri wake,alitaka urais aje aiuze nchi kabisa. Huko ameenda kujificha kwa kujua hatafanywa kitu kwa falsa ya ufuasi.
 
Edo angejipumzikia tu, naona hata ile team yake ya ulipo tupo wameshang'amua ukweli nakujikatia tamaa
 
Huyu mzee hajui kuwa upinzani ameuzoofisha mwenyewe!

CHADEMA ya sasa sio ile CHADEMA ya wakati hajakabidhiwa kadi ya CHADEMA.

CHADEMA ya sasa imebakiwa wapiga kelele tupu badala ya watenda vitendo sahihi.

CUF ya sasa haijulikani Mwenyekiti wa taifa ni nani?

ACT-Wazalendo inapukutika polepole.

UDP haina Katibu Mkuu.

Vyama vingine vimebaki kwenye mikoba ya wenyeviti.
Hahahaha.!... Mkuu hivi NCCR bado ipo?
 
Back
Top Bottom