Lowassa Kuhojiwa Na Kamati?

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kamati Ya Bunge Ya Kuchunguza Sakata La Umeme Wa Dharura Wa Richmond Development Cororatiion Llc, Itawahoji Wahusika Wote Wakiwamo Wajumbe Wa Task Force Iliyondwa Na Waziri Mkuu E.lowassa.

Je, Na Yeye Aliyeiunda Ataitwa? Wajumbe Wa Kamati Hiyo Walikua Ni Gray Mgonja (katibu Mkuu Hazina), Patrick Rutabanzibwa (alikua Katibu Mkuu Nishati Na Madini, Sasa Katibu Mkuu Maji) Na Johnson Mwanyika (mwanasheria Mkuu)
 
Kamati Ya Bunge Ya Kuchunguza Sakata La Umeme Wa Dharura Wa Richmond Development Cororatiion Llc, Itawahoji Wahusika Wote Wakiwamo Wajumbe Wa Task Force Iliyondwa Na Waziri Mkuu E.lowassa. Je, Na Yeye Aliyeiunda Ataitwa? Wajumbe Wa Kamati Hiyo Walikua Ni Gray Mgonja (katibu Mkuu Hazina), Patrick Rutabanzibwa (alikua Katibu Mkuu Nishati Na Madini, Sasa Katibu Mkuu Maji) Na Johnson Mwanyika (mwanasheria Mkuu)

What is the source of your info kuhusu hili? Nadhani bado haijawekwa wazi kamati itafanyaje kazi au nimepitwa,jamani? Kuuliza si ujinga!
 
Wasipomhoji watakuwa wanacheza katika hiyo kazi yao, maana huyu ndiye aliye kwenye centre ya issue nzima hii. So, kwangu mimi kumhoji siyo news, itakuwa news kama hawatamhoji!
 
akihojiwa itakuwa ni kazi ya bunge inatimia kwani wao wanakazi ya kuisimamia serikali .

Naamini kuwa kama wakiweza kumhoji basi itakuwa ni hatua ya kwanza kwenda mbele ila wasipomhhoji bado tutaendeleza ule u mungu mtu pale mmojaq wetu anapokuwa kiongozi basi anakuwa juu ya sheria za nchi
 
Wasipomhoji watakuwa wanacheza katika hiyo kazi yao, maana huyu ndiye aliye kwenye centre ya issue nzima hii. So, kwangu mimi kumhoji siyo news, itakuwa news kama hawatamhoji!

Unasema kweli kaka, isije ikawa wakafanya ya TAKUKURU ya kuisaisha kwa kusema, "Waziri Mkuu, kwa madaraka aliyopewa na sheria, aliunda kamati ili kuharakisha upatikanaji wa umeme, kwa hiyo kama kamati ama kampuni ilizembea hayo hayatakua tena makosa ya Waziri Mkuu.. Kamati ya Bunge imebaini kwamba, kuchelewa ama kuzuiwa kwa malipo ya awali yaliyokua yalipwe Richmond ndio chanzo cha kuchelewa kwa mitambo kufungwa.... LABDA sasa tuunde kamati ingine kuchunguza ni nani aliyezuia malipo"..... Hapo watapata kigugumizi maana aliyezuia malipo ni JK baada ya kuambiwa kwamba Richmond ni wasanii
 
Nilishauliza ni wapi katika sheria ya manunuzi ya Serikali (public procurement) panapo mpa Waziri Mkuu uwezo wa kuingilia utoaji na upatikani wa tenda za serikali.
 
Kulingana na tuhuma zilizopo ambazo pia na ofisi yake ilisha ingia marumbano ya moja kwa moja na wanahabari, kama LUwasa hatahojiwa basi kamati itakuwa na mapungufu makubwa mno na haitakuja na kipya zaidi ya yale yanayojulikana.
 
[QUOTENilishauliza ni wapi katika sheria ya manunuzi ya Serikali (public procurement) panapo mpa Waziri Mkuu uwezo wa kuingilia utoaji na upatikani wa tenda za serikali.[/QUOTE]

Tatizo la utawala wetu ni kiongozi kujisikia ana mamlaka juu ya jambo lolote bila kujali sheria zinasemaje!. Ndio tatizo hilo hilo lilo mpelekea pia PM aitume TAKUKURU itoke na taarifa ya kuisafisha RICHMOND, kitu ambacho kimeishusha hadhi sana Taasisi hii!

Nina wasi wasi kwamba tatizo hili hili, pia litaifanya kamati ama ishindwe kumuhoji PM ama ikimuhoji ipindishe maelezo ili asionekane hamnazo mbele ya jamii! Subirini tuone...kama kweli kamati hii itaweza muita nyoka, nyoka na si mjusi mkubwa!
 
Bunge tu lisijekuwa sehemu ya kusameheana kama walivyofanya kwa Mengi na Malima!
 
Kamati yaanza kuichunguza Richmond, watu maarufu wahojiwa

Muhibu Said na Mwanaid Omary

KAMATI Teule ya Bunge ya Kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa Kampuni ya Richmond Development (RDC), imeanza kuwahoji watu maarufu, akiwamo Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA).

Wengine waliokwisha kuhojiwa na kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ni Msajili wa Makampuni na Ofisa kutoka Kampuni ya Usajili katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko (BRELA).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe, alisema walianza kazi hiyo kwa kukusanya na kupitia nyaraka muhimu zinazohusiana na Richmond.

Alisema wanatarajia kuendelea na kazi hiyo iliyoanza Novemba 15, mwaka huu kwa wiki mbili zijazo kwa kufanya uchunguzi katika taasisi mbalimbali za serikali, ikiwamo Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).

Dk Mwakyembe alisema mikutano ya utendaji kazi wa kamati hiyo, inafanyika kwa sura ya kimahakama kwa wanaohojiwa kuapishwa na wanaohitajiwa na kamati kupelekewa hati maalum ya wito.

Aliwataka wananchi ndani na nje ya nchi wenye taarifa au nyaraka zozote kuhusu Richmond waziwasilishe katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, ushauri utakaowasilishwa, utalindwa chini ya sheria za Bunge.

"Tupo hapa (Ofisi za Bunge) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni," alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa hawategemei kusafiri kwa kuwa nyaraka zote muhimu wanazo.

Hata hivyo, alionya atakayewasilisha taarifa au nyaraka za uongo, kutia chumvi au za kughushi, atakuwa amefanya kosa la jinai kwa mujibu wa sheria.

Pia aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha taarifa zote zinazohusu kamati hiyo watakazozitangaza zinatoka katika vyanzo vya kuaminika.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stella Manyanya ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum, alisema kamati hiyo haitaficha ukweli na itakuwa tayari kuuarifu umma hata kama itabainika kuwa kigogo alihusika.
 
Maelezo haya ni mazuri sana hila pia kati ya kamati yenye kazi rahisi sana ni hii na pia kamati yenye kazi ngumu katika kutoa maamuzi yake ni kamati hii.

Hivyo wanakamati hii wakae wakijua kuwa wanakazi ya kumfunga paka kengele.
 
sasa ndiyo uzuri wa Kamati ya Bunge, kwani inafanya kazi kama mahakama, na ukiitwa ni lazima uende vinginevyo polisi wanaweza kukubeba mzoba mzoba.. ile ya kina Simba ni mazingaombwe tu..
 
Waheshimiwa,mimi naona hakuna haja ya kupoteza muda kwa kuundwa hizi kamati.Kulikuwa na wataalam kutoka kada mbalimbali na hata mwanasheria mkuu,kwa hiyo tulitarajia wangelifanya kazi yao kwa uaminifu.

Kama walienda kinyume na utaratibu wa wajibu wa kazi yao,basi na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Richmond wawajibishwe na na ikionekana kuwa kulikuwa na hujuma basi na aliyeunda tume hiyo kwa wakati huo (EL)awajibike bila kungoja shinikizo lolote.

Tufike mahala tuwe waadilifu,tukae pembeni kupisha sheria ichukue mkondo wake.Tusing'ang'a nie madaraka kama huyu mkulu wa BOT.

Naomba kutoa hoja.
 
Hoja yako imepokelewa Tatizo ni kuwa watawala wetu hawana mtu wa kufanya hayo kwani akipelekwa mahakamani Mwanasheria Mkuu ana uwezo wa kufuta kesi ..
 
Nasubiria kwa hamu kusoma kipengele cha mwisho cha ripoti ya TUME ambacho bila shaka kitasome "....tunaliomba bunge lako tukufu kuwachukulia hatua zinazofaaa wafuatao...."
 
Back
Top Bottom